Swali fikirishi: Kuna ubaya endapo baadhi ya nafasi Serikalini zitajazwa na wageni?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2023
4,694
6,396
Sababu mojawapo iliyosaidia Korea Kusini kuendelea ni viongozi wake kutambua mapema walichokuwa wanakihitaji na kutumia kila fursa waliyoipata kuifukuzia. Inawezekana, hata sisi tungefanya kama wao, nchi yetu ingekuwa kama yao, au zaidi.

Hilo ndilo limenipelekea kufikiria kuwa ikiwa tutawaazima baadhi "yao" watusaidie kuongoza baadhi ya Wizara kwa muda, inaweza ikatusaidia?

Kama hilo lingewezekana, ningependekeza yafuatayo.

1. Nafasi ya Uraisi, Umakamu wa Rais, na Waziri Mkuu wasipewe wageni.

2. Wizara zote isipokuwa ya Ulinzi, Mambo ya Ndani, na ya Katiba & Sheria isiongozwe na wageni.

3. Wizara zingine zote zilizobakia, Waziri wake na Katibu Mkuu wawe wageni, ila nafasi zilizobaki kama Naibu Waziri, Naibu Katibu Mkuu ndiyo ishikiliwe na Watanzania.

4. Utaratibu huo ungetumika kwa miaka mitano au kumi tu. Baada ya hapo, wageni wote wtarudi kwao.

Zifuatazo ni Wizara na Mataifa ambayo watu wake wangepewa hizo fursa ya uongozi wizarani kama Waziri na Katibu Mkuu:
1. Elimu - Finland

2. Kilimo - Muisraeli

3. Viwanda - Japan/ South Korea

4. Uchumi, Mipango na Uwekezaji - Msingapore

5. Sayansi na Teknolojia - Mkorea Kaskazini/ Muiran/ Mrusi

6. Biashara na Uwekezaji - Muingereza

7. Nishati - Muistralia

8. Madini - Mkaburu

9. Usafirishaji - Hong Kong

10. Fedha - Mswizi

11. Diplomasia ya Kimataifa - Mmarekani

12. Utalii na Utamaduni - Mmalaysia

13. Afya - New Zealand

14. Uvuvi na Mali Asili - Mcanada

15. Makazi na Mipango Miji - Mjerumani

Pia, Wakuu wa hizi taasisi na viongozi wake waandamizi wawe ni wageni watakoonekana wanakidhi vigezo:
(A). TRA
(B). Mamlaka za Maji Safi na Maji Taka Kitaifa na Mikoani
(C). TANESCO
(D). Bandari
N.k. Natamani kuweka Magereza na Uhamiaji lakini kwa sababu ni mojawapo ya taasisi nyeti kiusalama, nimeamua kuziacha.

Japo huu ni mfano tu, unafikiri tungeamua kama nchi kufanya hivyo kwa kipindi cha miaka mitano au kumi tu ingekuwa na athari gani?
 
Hizo nchi zinazotekeleza Sera kama hiyo ni zina Idara ya Usalama imara pamoja na Jeshi imara na wazalendo ndomaan hawaogopi kuwaweka Wageni katika Wizara tofaut tofaut Serikalini,

Sisi na hii idara yetu ya usalama wa Taifa ambayo Mtu akipewa bahasha tu anaweza fanya lolote hata Kuua Nduguye,... Au hawa wanajeshi ambao Kazi yao kubwa ni Kuonea raia na Kulinda Watawala ambao ni wezi,

Ndo unataka Tuwaweke wageni kweny Wizara wakati idara ya usalama wa Taifa ni uhuni mtupu plus jeshi lenyewe Linaonea raia na kuwaogopa watawala,

Ikitokea mmewaweka wageni kwenye Wizara tofauti tofauti alaf wakaanza Kutoa bahasha kwa Viongozi wa Jeshi pamoja na Viongozi kadhaa wa Idara ya usalama ili wapindue Serikali ya Wazawa, unafkiria Kitakachofuata ni nini kama sio kuludi utumwani mara ya pili ??

Kiufupi mabadiliko ya Taifa lolote lenye nguvu unaloona saivi duniani msingi wake ulianza kwenye Idara ya usalama wa Taifa ikifuatiwa na Mfumo mzuri wa Elimu, kiufupi tuimarishe kwanza Mfumo wa Elimu na mabadiliko makubwa yafanyike kwenye Idara ya Usalama wa Taifa.
 
ni vyema wengine wote tukawa raia tu, nyadhifa zote ziwe na wazungu, wahindi, waarabu, wachina nk. Ikiwezekana tuwe jimbo la USA tu.
 
Hapo kwenye kuwa jimbo la USA ndiyo tutakua tumesummarize thread yote.
 
Mimi nilikuwa na mawazo ya wapinzani kupewa wizara zenye changamoto zaidi kama ½ ya Baraza la Mawaziri .
 
Hizo nchi zinazotekeleza Sera kama hiyo ni zina Idara ya Usalama imara pamoja na Jeshi imara na wazalendo ndomaan hawaogopi kuwaweka Wageni katika Wizara tofaut tofaut Serikalini,

Sisi na hii idara yetu ya usalama wa Taifa ambayo Mtu akipewa bahasha tu anaweza fanya lolote hata Kuua Nduguye,... Au hawa wanajeshi ambao Kazi yao kubwa ni Kuonea raia na Kulinda Watawala ambao ni wezi,

Ndo unataka Tuwaweke wageni kweny Wizara wakati idara ya usalama wa Taifa ni uhuni mtupu plus jeshi lenyewe Linaonea raia na kuwaogopa watawala,

Ikitokea mmewaweka wageni kwenye Wizara tofauti tofauti alaf wakaanza Kutoa bahasha kwa Viongozi wa Jeshi pamoja na Viongozi kadhaa wa Idara ya usalama ili wapindue Serikali ya Wazawa, unafkiria Kitakachofuata ni nini kama sio kuludi utumwani mara ya pili ??

Kiufupi mabadiliko ya Taifa lolote lenye nguvu unaloona saivi duniani msingi wake ulianza kwenye Idara ya usalama wa Taifa ikifuatiwa na Mfumo mzuri wa Elimu, kiufupi tuimarishe kwanza Mfumo wa Elimu na mabadiliko makubwa yafanyike kwenye Idara ya Usalama wa Taifa.
Mbaya zaidi elimu yetu inapoteza ari na tija kila uchwao. Walimu wanagugumia kwa maumivu moyoni. Maslahi kidogo na mazingira ya kazi ni magumu.

Elimu yetu inachezewa na watawala. Vyeti feki vimerudi tena mtaani. Vyuo vikuu vinagawa Master degree na PhD kwa wanasiasa kama mimba.

Nchi ina uozo kila mahali. Namuonea huruma Rais
 
Sababu mojawapo iliyosaidia Korea Kusini kuendelea ni viongozi wake kutambua mapema walichokuwa wanakihitaji na kutumia kila fursa waliyoipata kuifukuzia. Inawezekana, hata sisi tungefanya kama wao, nchi yetu ingekuwa kama yao, au zaidi.

Hilo ndilo limenipelekea kufikiria kuwa ikiwa tutawaazima baadhi "yao" watusaidie kuongoza baadhi ya Wizara kwa muda, inaweza ikatusaidia?

Kama hilo lingewezekana, ningependekeza yafuatayo.

1. Nafasi ya Uraisi, Umakamu wa Rais, na Waziri Mkuu wasipewe wageni.

2. Wizara zote isipokuwa ya Ulinzi, Mambo ya Ndani, na ya Katiba & Sheria isiongozwe na wageni.

3. Wizara zingine zote zilizobakia, Waziri wake na Katibu Mkuu wawe wageni, ila nafasi zilizobaki kama Naibu Waziri, Naibu Katibu Mkuu ndiyo ishikiliwe na Watanzania.

4. Utaratibu huo ungetumika kwa miaka mitano au kumi tu. Baada ya hapo, wageni wote wtarudi kwao.

Zifuatazo ni Wizara na Mataifa ambayo watu wake wangepewa hizo fursa ya uongozi wizarani kama Waziri na Katibu Mkuu:
1. Elimu - Finland

2. Kilimo - Muisraeli

3. Viwanda - Japan/ South Korea

4. Uchumi, Mipango na Uwekezaji - Msingapore

5. Sayansi na Teknolojia - Mkorea Kaskazini/ Muiran/ Mrusi

6. Biashara na Uwekezaji - Muingereza

7. Nishati - Muistralia

8. Madini - Mkaburu

9. Usafirishaji - Hong Kong

10. Fedha - Mswizi

11. Diplomasia ya Kimataifa - Mmarekani

12. Utalii na Utamaduni - Mmalaysia

13. Afya - New Zealand

14. Uvuvi na Mali Asili - Mcanada

15. Makazi na Mipango Miji - Mjerumani

Pia, Wakuu wa hizi taasisi na viongozi wake waandamizi wawe ni wageni watakoonekana wanakidhi vigezo:
(A). TRA
(B). Mamlaka za Maji Safi na Maji Taka Kitaifa na Mikoani
(C). TANESCO
(D). Bandari
N.k. Natamani kuweka Magereza na Uhamiaji lakini kwa sababu ni mojawapo ya taasisi nyeti kiusalama, nimeamua kuziacha.

Japo huu ni mfano tu, unafikiri tungeamua kama nchi kufanya hivyo kwa kipindi cha miaka mitano au kumi tu ingekuwa na athari gani?
Jazeni "WAARABU!"
 
Back
Top Bottom