Swala la ardhi ya Bagamoyo ni strategy ya kisiasa tu, lakini kiuhalisia serikali ya Zanzibar haimaanishi kile ilichoongea

Mr Dudumizi

JF-Expert Member
Sep 9, 2020
6,880
12,320
Habari zenu wana JF wenzangu,

Kuna mshituko mkubwa umetukumba watanganyika, hasa kuhusu hili swala la serikali ya Zanzibar kudai kuwa ina eneo lake la ardhi huko wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.

Kama ilivyo kawaida ya baadhi yetu, huwa hatukurupuki kulalamika bila kufuatilia kwa makini kina cha kile kilichoongelewa na serikali au mtu husika.

Ukweli ni kwamba hili swala limetumiwa kisiasa makusudi na namba 1 wa huko, ili aweze ku win kiurahisi katika mbio za kumchagua mgombea uraisi wa nchi hiyo kupitia chama anachotokea, na vile vile kupita katika uchaguzi mkuu ambao utafanyika miaka miwili tu ijayo.

Ikumbukwe kwamba namba 1 huyo babu zake ni wandengereko wa Mkuranga mkoani Pwani, ambapo baba yake mwenyewe alieleza kwamba alipelekwa katika kisiwa hicho na wazazi wake ili akajifunze elimu akhera na baadae kurudi mkuranga kuendelea na mambo mengine.

Ila kwa bahati mbaya au nzuri baba huyo alipofika huko, akaongeza na elimu dunia na mwisho wake kulowea huko hadi kuwa namba 1 wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.

Sasa namba 1 wa sasa historia anaijua na kamwe hawezi kufanya mzaha wa kumega palipo asili yake, huku akijua kwamba huenda na yeye ikatokea siku 1 akawa namba 1 tena wa JMT kama ilivyotokea kwa baba yake.

Kuna msemo wa waingereza unasema "Home sweet Home" na ndio maana namba 1 huyo miaka yake yote ya siasani hakuwa kugombea huko alipo sasa, bali alikuwa anagombea kule ilipo asili yake (mkuranga)

Sasa kwa vile amezungukwa na wazalendo uchwara wa Zanzibar ambao wengi wao wanaonesha chuki ya dhahiri kwake kama mzanzibar-mtanganyika na Tanganyika yetu kwa ujumla. Basi ndo akaja na style ya kuwafubaza kwa kile wapendacho kukisikia ili iwe rahisi kuchagulika kwa kuamini kwamba namba 1 huyo yuko pamoja na wao katika kupigania masilahi ya kisiwa chao.

Mnaofikiri kuwa Bagamoyo itamegwa chini ya namba 1 huyu wa sasa basi mtasubiri sana na ukizingatia hata huyu wa Muungano nae asili yake ni huko udigoni Tanga. Maana angekuwa original wa kule kisiwani, kamwe asingepewa nchi kama ilivyokuwa kwa kina dr SAS alienyang'anywa tonge mdomoni na mzee rukhsa kwa sababu ya kile nilichoeleza hapo juu.

Karibuni kwa kuchangia kistaarab.

Tanganyika nitakupenda mpaka kufa.
 
Wameweka kinga ili tusiongelee visiwa vya Fungu Mbaraka ambavyo teyari wamechukua kimya kimya, (jina limeshabadilishwa kutoka Latham Island na kuitwa Fungu Kizimkazi).
viko mbele na kusini mwa Dar. Muungano ukivunjika bara haina bahari, labda Mtwara
 
Katika siasa kila mtu anaweza kuongea lolote, lkn inapokuja swala la utekelezaji mambo huwa zero.

Hakuna nchi au mtu anaeweza kumega ardhi halali ya Tanganyiko.

Hili hata Malawi au Idi Amin huko alipo analijua, sembuse Kazanzibar
 
Jambo limesainiwa teyari hivi karibuni, ndo ukisikia changamoto za Muungano kutatuliwa. Kila kilichakuwa kinabaniwa pua hapa zenji kimekubaliwa na viongozi wa huko.
 
Nawe naona umetumwa kwa nia ya kupooza tu hali ya hewa kwa historia mbili tatu.

Kama si ardhi yao, MARUFUKU ile ni ya nini? Kama haiwezi kumiliki, ardhi ile ni mali ya nani?

Kwa nini serikali ya JMT haijatoka kuuelezea umma, ukweli wa taarifa ile?
 
Ile Ardhi ni ya SMZ.
Wameinunuwa au wametunukiwa wakati wa Nyerere 1977.
Fatlia utajuwa.

Watu wamevamia na kujenga ndio taarifa ilotoka.

Mtanzania yeyote anahaki kumiliki Ardhi. na ikiwa imevamiwa unahaki ya kudai

Sasa tujiulize hili eneo litumika kwa manufaa ya wazanzibari au laa
Nasikia kuna mfadhili anataka kupewa hii sehemu na Raisi wa Zanzibar ( mfalme).
Sasa ndio pirika zote hizo.
 
Ngoja tuone itakavyokuwa kama raisi Mwinyi mwenyewe ana uwezo wa kuwazuia hao jamaa kulichukua hilo eneo.
 
Wanakwepa kujibu HOJA za Karume, wakati huo huo wanatuliza tuhuma za No1 wa huko kukodisha visiwa 2 Kwa wageni kimya kimya.

Zenz itabaki kuwa Mkoa wa bara na Si vyinginevyo.
 
Hii ardhi ilimilikishwa kwa SMZ sawa na muwekezaji yoyote, haina maana sasa ni sehemu ya Zanzibar
Kwani ile ya mmiliki wa AS Roma kadai ni sehemu ya kwao?
 
Jambo limesainiwa teyari hivi karibuni, ndo ukisikia changamoto za Muungano kutatuliwa. Kila kilichakuwa kinabaniwa pua hapa zenji kimekubaliwa na viongozi wa huko.
Kusainiwa sio tatizo, maana ndio hiyo strategy ninayokwambia. Swala litaendelea kupigwa danadana hadi pale namba 1 wa huko atapopewa kipindi cha pili na cha mwisho katika utawala wake.
 
Wameweka kinga ili tusiongelee visiwa vya Fungu Mbaraka ambavyo teyari wamechukua kimya kimya, (jina limeshabadilishwa kutoka Latham Island na kuitwa Fungu Kizimkazi).
viko mbele na kusini mwa Dar. Muungano ukivunjika bara haina bahari, labda Mtwara
Hizi ni tuhuma kubwa. Bunge halikuhusika na hili?
 
Sasa namba 1 wa sasa historia anaijua na kamwe hawezi kufanya mzaha wa kumega palipo asili yake, huku akijua kwamba huenda na yeye ikatokea siku 1 akawa namba 1 tena wa JMT kama ilivyotokea kwa baba yake.
Tanganyika nitakupenda mpaka kufa.
Duh... Mkuu Mr Dudumizi , kauli huumba, lisemwalo lipo!, tembelea hapa uone mimi nilisema nini Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, 2025 Mama Akabidhi Kwanza Mwanamume, Kisha 2030 Ndipo Aje Mwanamke
Kwa faida ya wavivu wa kufollow links
.Lakini kama ataisikia hii sauti, sio vibaya kama atajiandaa na kumuandaa mtu wa kumpokea, kwa maoni yangu, Dr. Hussein Mwinyi atatufaa sana, hivyo namuomba Rais Samia akiisikia sauti, amuombe Dr. Hussein Mwinyi, kwa uchaguzi wa urais wa 2025 aje kugombea urais wa JMT, kuimalizia awamu ya pili ya Mama Samia kwa yeye kukubali kuwa rais wa JMT kwa awamu moja tuu.

Natumaini nimeeleweka.
P.
P
 
Kwa hiyo unamaanisha tusiogope kauli isiyo na ushahidi, muhimu kwanza wangetuambia hizo ekari zinaanzia wapi na kuishia wapi ndio tuanze kulalamika tukishahakikisha?

Mimi niliamini ile kauli kwasababu ya huyu mzanzibari tuliyenaye huku Bara, anayeonekana "kupakumbuka" sana kwao wakati huu, hasa nikikumbuka ule msamaha wa deni la Tanesco kwa Zanzibar juzi tu
 
Nawe naona umetumwa kwa nia ya kupooza tu hali ya hewa kwa historia mbili tatu.

Kama si ardhi yao, MARUFUKU ile ni ya nini? Kama haiwezi kumiliki, ardhi ile ni mali ya nani?

Kwa nini serikali ya JMT haijatoka kuuelezea umma, ukweli wa taarifa ile?
Serikali haiwezi kukurupuka kulielezea swala hilo ambalo ni mfano wa ndugu wawili mmoja mkbwa wa ndoa (Tanganyika) na mungine mdogo wa nje ya ndoa (Zanzibar) wanazozania mirathi na ukizingatia wakubwa wanaelewa kinachoendelea.

Laiti tamko hilo lingetolewa na Kenya, Uganda, Rwanda au Malawi hapo ndo serikali ingelichukulia hili swala serious maana hizo nchi zipo nje ya ule udugu wa damu (Muungano)
 
Ile Ardhi ni ya SMZ.
Wameinunuwa au wametunukiwa wakati wa Nyerere 1977.
Fatlia utajuwa.

Watu wamevamia na kujenga ndio taarifa ilotoka.

Mtanzania yeyote anahaki kumiliki Ardhi. na ikiwa imevamiwa unahaki ya kudai

Sasa tujiulize hili eneo litumika kwa manufaa ya wazanzibari au laa
Nasikia kuna mfadhili anataka kupewa hii sehemu na Raisi wa Zanzibar ( mfalme).
Sasa ndio pirika zote hizo.
Angalau wewe umeeleweka. Ila pamoja na kwamba jamaa wanahaki kama ulivyoandika, lkn kinachofanyika sasa hivi ni hiyo strategy ya kisiasa ili kutafuta uungwaji mkono kutoka kwa wafia Zanzibar yao.

So hili swala litakuwa la moto kipindi hiki, afu baada ya malengo litayayuka kama lilivyoyayuka miaka mingi iliyopita mpaka watu wakawa hawalifahamu.
 
Ngoja tuone itakavyokuwa kama raisi Mwinyi mwenyewe ana uwezo wa kuwazuia hao jamaa kulichukua hilo eneo.
Kuwa na uwezo au vinginevyo, wewe amini tu huu ni upepo uliofunguliwa kwa sababu maalum. Ukishapita watu wataendelea na maisha yao bila kusikia tena habari ya ardhi hiyo ya Bagamoyo.
 
Wanakwepa kujibu HOJA za Karume, wakati huo huo wanatuliza tuhuma za No1 wa huko kukodisha visiwa 2 Kwa wageni kimya kimya.

Zenz itabaki kuwa Mkoa wa bara na Si vyinginevyo.
Wewe unaona mbali na ulichoandika kina uhalisia fulani.
 
Hii ardhi ilimilikishwa kwa SMZ sawa na muwekezaji yoyote, haina maana sasa ni sehemu ya Zanzibar
Kwani ile ya mmiliki wa AS Roma kadai ni sehemu ya kwao?
Ndio maana nikasema hili swala linatumiwa tu kisiasa lkn hakuna anaeota kwamba ardhi ya Tanganyika itachukuliwa kirahisi rahisi hivi.
Ni swala linalotumiwa kisiasa kwa muda tu kwa malengo fulani.

Baada ya hapo kila mtu atalisahau kama lilivyosahaulika miaka mingi iliyopita.
 
Back
Top Bottom