Suphian Juma: Nimeng'atuka ACT Wazalendo

Suphian Juma: Nimeng'atuka ACT Wazalendo

Kwa sasa upinzani halisi ni CHADEMA tu. Wanaishi katika kile wanachokisema na kukiamini.

CHADEMA wanasema kilichofanyika October, 2020 ni uchafuzi uliovuka mipaka yote ya kidemokrasia toka kuwepo kwa taifa la Tanzania. Na wamesimamia hicho hicho mpaka sasa.
Kwani CHADEMA bado ipo ? Naona unaota ndoto za mchana
 
Kwa staili hiyo utahama sana.

Kwenye kila taasisi kuna maamuzi yanafanyika Kama kipimo cha uvumilivu wa viongozi wake. Kama wameteleza kwa maoni yako basi penyeza dukuduku lako sio kukimbia kimbia Kama Mbwa Koko.

Ukubwa ni uvumilivu sio umri kwenda mwana kwenda ukifika piga simu utupe mrejesho
 
CHADEMA ilikufa 2015 siku mwenyekiti wenu alipotangaza kubadili gia angani. Kilichobaki ni mzimu tu. Pole sana.
Cdm haitakufa kwa kukataliwa na wananchi, labda kifutwe na msajili wa vyama vya siasa. Cdm ni brand kubwa na ni chama cha kizazi hiki boss. Mlifanikiwa kuiua NCCR, CUF nk lakini sio kwa cdm, labda cdm ikosee ianze kujipendekeza kwa ccm. Vinginevyo itabidi ccm indelee kutumia taasisi za kimamlaka kama tume ya uchaguzi, tiss, polisi na kura za kwenye mabeg ili kutangazwa washindi na sio kushinda. Iwapo wananchi watazidi kupoteza imani na box la kura, hawatajitokeza kupiga kura, lakini sio kupigia kura ccm kwa ridhaa yao.
 
Siasa za Tanzania pasua kichwa, ndio maana watu wakiambiwa ingieni bsrabarani wanagoma,Leo ndio nimepata jibu. Kiongozi wengi wa upinzani maamuzi yao yanaangalia maslahi binafsi, sasa watu Znz wamekufa, kwa kupigania uchaguzi urudiwe, sasa watu ambao wamefiwa na wahanga wao, mwaka ujao ukiwaambia waingie barabarani watakubali, si watawaona wajinga tu
 
CHADEMA ilikufa 2015 siku mwenyekiti wenu alipotangaza kubadili gia angani. Kilichobaki ni mzimu tu. Pole sana.

Hayo ndio matamanio yako cdm ife. Ila pole maana matamanio yako hayatakaa yatimie, tena kwa hizo kura za kwenye mabeg, mbona utangoja sana.
 
Yote kwa yote ungekula ubunge na chama kuingia SUK usingejiuzuru, ila kwa sababu umebwagwa ndiyo umetoa hayo maamuzi.


But enjoy your decision.
 
NIMENG'ATUKA ACT WAZALENDO-SUPHIAN.

Najua wengi mmeumia sana. Mmestaajabishwa mno na maamuzi ya Chama changu cha ACT wazalendo kukubali kuungana na Serikali ya Magufuli na Mwinyi tuliyoitangazia dunia imeunajisi Uchaguzi Mkuu wa Tanzania wa mwaka 2020.

Kitendo cha Chama kukubali kupeleka jina la Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar, na kuridhia kuapishwa wabunge wake; naelewa na naona wengi wananchi wenzangu si tu kimewakasirisha kupitiliza ila bali pia kimewatolea imani katika kuwaamini wanasiasa na vyama vya upinzani nchini.

Wengi tangu Jana Desemba 06, 2020 Chama kilipotangaza uamuzi wake huo kupitia Katibu Mkuu, rafiki yangu Ado Shaibu mmeendelea kuniuliza msimamo wangu mtandaoni, kwa simu hadi ana kwa ana kwa kuzingatia mimi kama mwanachama na Mtanzania ninayependa na kuheshimu Haki za Binadamu na Demokrasia, hivyo hakika nasema hampo peke yenu, Masikitiko yenu Watanzania wenzangu ni masikitiko yangu pia.

Uchaguzi ulikuwa batili, uongozi uliopatikana na unaoendelea kupatikana na uchaguzi huu ni batili pia. Haramu haijawahi kuwa halali. SIMPLE MATHEMATICS.

Kwangu mimi Suphian, ndoto yangu kuu ya kuona Taifa langu huru na lenye kufuata misingi ya Haki ni Lulu zaidi ya maslahi ya Chama cha siasa nilipo au yeyote ninayemwamini katika Siasa au nje ya siasa.

Kama nilivyoahidi wakati wa Sakata la Wabunge 19 wa CHADEMA, kwamba siwezi kumumunya maneno pale haki ikipindishwa hata kama na Chama changu, hivyo NATANGAZA: SIUNGI MKONO MAAMUZI YA CHAMA CHANGU.

Hivyo naomba dunia ijue kuanzia Leo Desemba 07, 2020 mimi Suphian Juma Nkuwi rasmi NANG'ATUKA UANACHAMA wa ACT wazalendo ili kusimama na HAKI, kusimama na familia za ndugu waliouawa, kutekwa, kufungwa na kuumizwa wakipigania Uchaguzi Huru, Haki na unaoaminika.

Asante Kiongozi wa ACT wazalendo na Kaka yangu, Zitto Kabwe na Chama kwa ujumla kwa malezi yenu ya KUSIMAMA NA HAKI mliyonipatia tangu mwaka 2015 nilipojiunga nanyi, nawatakia kila kheri.

Suphian Juma,
Aliyekuwa Mgombea Ubunge, ACT wazalendo 2020-2025 Singida Magharibi.

Desemba 07, 2020.View attachment 1644080
KuPata KITUKO KAMA HIKI ANDIKA
SUPHIANRUKWA KWENDA NO 15577
 
Kuanzia jana nimekuelewa sana mkuu kwako Tanzania kwanza tamaa nyuma, sema ulikuwa humjui Zitto vizuri sasa ndiyo umejua rangi yake haswa
 
Imekuuma jamaa amegoma kuwa sehemu ya watu malaghai na dhuluma
Inaniumaje ccm mie nimecheka karukwa anapiga kelele Kanaani awawezi ingia wotee

Hata Safina ya Nuhu walichagua nani wa kuingia naoo arelax hahaa ahamie chadema
 
Narudia tena kwamba CHADEMA ilikufa mwaka 2015 kwa mwenyekiti kubadili gia angani na kumfanya Dr Slaa kuondoka kwenye Chama hicho. Huo ndio ukweli mchungu.
Hayo ndio matamanio yako cdm ife. Ila pole maana matamanio yako hayatakaa yatimie, tena kwa hizo kura za kwenye mabeg, mbona utangoja sana.
 
Narudia tena kwamba CHADEMA ilikufa mwaka 2015 kwa mwenyekiti kubadili gia angani na kumfanya Dr Slaa kuondoka kwenye Chama hicho. Huo ndio ukweli mchungu.

Kama ingekuwa imekufa mngekuja na kura za kwenye mabeg?
 
Mkuu unaleta UANAHARAKATI katika mbio za SIASA ?!!

Ninyi ndio mnaowachanganya wafuasi wenu kwa KUWADHANISHA ya kwamba MAMBO YENU siasani ni sawa na zile harakati za akina Ralph Abernathy,Fannie Lou Hamer,Desmond Tutu na wengineo...

Hivi mnashindwaje kuwa kama wanasiasa wa Kenya akina Raila Odinga,Kenyatta,Musalia Mudavadi Rutto na wengineo...?!!!

Ama hao ni "wanafiki"?!!
Ama hao si WANASIASA wa kweli bali "vibaraka na wachumia tumbo"?!!!

Leo hii mnataka mfanye LOBBYING ZA KIHARAKATI na si za KISIASA ndani ya VYAMA VYA SIASA.....

Boutrous Boutrous Ghali(former UN SG) alipata kusema "ONLY STUPID PEOPLE DO NOT CHANGE THEIR MINDS"

Endeleeni kusubiri UJIO wa VYAMA MALAIKA kutoka MBINGUNI.....


Kijana Muuza Al Kasus
Tandale
Umetaja watu mbali mbali wakiwemo wana harakati bila kuwataja na sifa zao ili aweze kujua nini maana ya kuwataja, je raila ana nini katika swala la msimamo? Naomba eleza
 
Siasa zenu hizi sio sahihi ni maonyesho, 2015 maalim na wenzake walisusa peke yao haikusaidia bali hawakuumizwa sana km mara hii. Mara hii wameumizwa sana bali CHADEMA wamesusa bara.

Ukiwa kiongozi ktk mazingira ya sasa tz au mpinzani ni mateso na hali kadharika ukiwa ccm ni maumivu maana wao ndio hakuna kushikisha kabisa.

Muhimu subra tukitaraji itafika muda mabadiliko ya lazima yatatokea na tunaweza kuwa nchi ya watu wenye furaha na kufuata katiba mzuri
 
Hamia CHADEMA, ukimaliza hamia NCCR MAGEUZI au CUF.

Shortcuts ni kuhamia CCM kabisa.

Mpaka ufikie umri wa Mzee Warioba utakuwa ushahama vyama 100.

Hahahaha 🤣🤣🤣🤣
Elimu elimu elimu !!!!!!
Baba wa taifa alihimiza sana, ipende sana ccm huenda unanufaika nayo
 
Back
Top Bottom