Kukimbia chama sio suruhisho la tatizo.
Katika demokrasia za vyamani, kuna njia tatu.
1. Kukubaliana na maamuzi ya wenzako walio wengi/ wakubwa wako chamani.
2. Kukakataa maamuzi hayo na kujenga ushawishi kutoka ndani ili yabadilishwe
3. Kuona kwamba hukubaliani na maamuzi, na huna ushawishi wa kuyabadilisha, na hivyo, kujitenga na maamuzi hayo kwa kujiuzulu.
Huyu mwamba, kwa uandishi huu, kaona
1.Maamuzi hakubaliani nayo.
2. Hawezi kujenga ushawishi wa kuyabadili maamuzi
3. Jambo pekee la kufanya ni kujitenga na maamuzi hayo kwa kujiuzulu, ili hata siku ikitokea hukumu juu ya maamuzi hayo, aweze kusema aliyapinga na kutengana nayo.
Namuunga mkono, kwa sababu.
1. Ni haki yake ya kikatiba.
2. Maamuzi yana logical consistency. Haiyumkiniki useme uchaguzi si halali, halafu ukubali cheo unachopewa na mtu ambaye unasema hakushinda katika uchaguzi halali. Hii ni contradiction.
3.Ana expose undumilakuwili wa vyama vya upinzani Tanzania.