Suphian Juma: Nimeng'atuka ACT Wazalendo

Suphian Juma: Nimeng'atuka ACT Wazalendo

Rule and divide naona inaleta matokeo japo naamini hawatafanikiwa.

Hongera brother, Ukweli utakuweka huru.!
 
NIMENG'ATUKA ACT WAZALENDO-SUPHIAN.

Najua wengi mmeumia sana. Mmestaajabishwa mno na maamuzi ya Chama changu cha ACT wazalendo kukubali kuungana na Serikali ya Magufuli na Mwinyi tuliyoitangazia dunia imeunajisi Uchaguzi Mkuu wa Tanzania wa mwaka 2020.

Kitendo cha Chama kukubali kupeleka jina la Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar, na kuridhia kuapishwa wabunge wake; naelewa na naona wengi wananchi wenzangu si tu kimewakasirisha kupitiliza ila bali pia kimewatolea imani katika kuwaamini wanasiasa na vyama vya upinzani nchini.

Wengi tangu Jana Desemba 06, 2020 Chama kilipotangaza uamuzi wake huo kupitia Katibu Mkuu, rafiki yangu Ado Shaibu mmeendelea kuniuliza msimamo wangu mtandaoni, kwa simu hadi ana kwa ana kwa kuzingatia mimi kama mwanachama na Mtanzania ninayependa na kuheshimu Haki za Binadamu na Demokrasia, hivyo hakika nasema hampo peke yenu, Masikitiko yenu Watanzania wenzangu ni masikitiko yangu pia.

Uchaguzi ulikuwa batili, uongozi uliopatikana na unaoendelea kupatikana na uchaguzi huu ni batili pia. Haramu haijawahi kuwa halali. SIMPLE MATHEMATICS.

Kwangu mimi Suphian, ndoto yangu kuu ya kuona Taifa langu huru na lenye kufuata misingi ya Haki ni Lulu zaidi ya maslahi ya Chama cha siasa nilipo au yeyote ninayemwamini katika Siasa au nje ya siasa.

Kama nilivyoahidi wakati wa Sakata la Wabunge 19 wa CHADEMA, kwamba siwezi kumumunya maneno pale haki ikipindishwa hata kama na Chama changu, hivyo NATANGAZA: SIUNGI MKONO MAAMUZI YA CHAMA CHANGU.

Hivyo naomba dunia ijue kuanzia Leo Desemba 07, 2020 mimi Suphian Juma Nkuwi rasmi NANG'ATUKA UANACHAMA wa ACT wazalendo ili kusimama na HAKI, kusimama na familia za ndugu waliouawa, kutekwa, kufungwa na kuumizwa wakipigania Uchaguzi Huru, Haki na unaoaminika.

Asante Kiongozi wa ACT wazalendo na Kaka yangu, Zitto Kabwe na Chama kwa ujumla kwa malezi yenu ya KUSIMAMA NA HAKI mliyonipatia tangu mwaka 2015 nilipojiunga nanyi, nawatakia kila kheri.

Suphian Juma,
Aliyekuwa Mgombea Ubunge, ACT wazalendo 2020-2025 Singida Magharibi.

Desemba 07, 2020.View attachment 1644080
Ndio nani????
 
Endeleeni tu kuisaidia ccm kuuwa vyama vyenu, hakuna mapimbi wa kuja kuvisimamisha tena ndio vinakufa hivyoo,

CHADEMA haitakufa kwa kukataliwa na wananchi, labda kifutwe na msajili wa vyama vya siasa. Chadema ni brand kubwa na ni chama cha kizazi hiki boss. Mlifanikiwa kuiua NCCR, CUF nk lakini sio kwa chadema, labda chadema ikosee ianze kujipendekeza kwa ccm

Vinginevyo itabidi ccm indelee kutumia taasisi za kimamlaka kama tume ya uchaguzi, TISS, polisi na kura za kwenye mabeg ili kutangazwa washindi na sio kushinda

Iwapo wananchi watazidi kupoteza imani na box la kura, hawatajitokeza kupiga kura, lakini sio kupigia kura ccm kwa ridhaa yao.
 
Mkuu unaleta UANAHARAKATI katika mbio za SIASA ?!!

Ninyi ndio mnaowachanganya wafuasi wenu kwa KUWADHANISHA ya kwamba MAMBO YENU siasani ni sawa na zile harakati za akina Ralph Abernathy,Fannie Lou Hamer,Desmond Tutu na wengineo...

Hivi mnashindwaje kuwa kama wanasiasa wa Kenya akina Raila Odinga,Kenyatta,Musalia Mudavadi Rutto na wengineo...?!!!

Ama hao ni "wanafiki"?!!
Ama hao si WANASIASA wa kweli bali "vibaraka na wachumia tumbo"?!!!

Leo hii mnataka mfanye LOBBYING ZA KIHARAKATI na si za KISIASA ndani ya VYAMA VYA SIASA.....

Boutrous Boutrous Ghali(former UN SG) alipata kusema "ONLY STUPID PEOPLE DO NOT CHANGE THEIR MINDS"

Endeleeni kusubiri UJIO wa VYAMA MALAIKA kutoka MBINGUNI.....


Kijana Muuza Al Kasus
Tandale

Hoja yako ni nini hapa?
 
Hongera sana Suphian, uamuzi wako ni uamuzi wa kusimamia misingi
Nakuunga mkono mia kwa mia. ACT siyo chama cha kusimamia ajenda za msingi za Taifa tena, bali ni chama rahisirahisi tu cha watu wasio na msimamo usioyumba, ni chama cha wasaka fursa
 
Eti wengi wameumia ,mpuuzi sana ulikuwa na lipya lipi sema umefukuzwa unalialia tu mitandaoni
Angefukuzwa chama chake kingetoa taarifa. Hapa yuko kwa verified user kasema ule haukuwa uchaguzi, bali maonyesho ya ujinga na ukatili wa mtu mweusi kwenye box la kura.

Hivyo hayuko tayari kukubaliana na maamuzi ya chama chake kubariki ule ushenzi, ili watu kadhaa wapate vyeo full stop.
 
Cdm haitakufa kwa kukataliwa na wananchi, labda kifutwe na msajili wa vyama vya siasa. Cdm ni brand kubwa na ni chama cha kizazi hiki boss. Mlifanikiwa kuiua NCCR, CUF nk lakini sio kwa cdm, labda cdm ikosee ianze kujipendekeza kwa ccm. Vinginevyo itabidi ccm indelee kutumia taasisi za kimamlaka kama tume ya uchaguzi, tiss, polisi na kura za kwenye mabeg ili kutangazwa washindi na sio kushinda. Iwapo wananchi watazidi kupoteza imani na box la kura, hawatajitokeza kupiga kura, lakini sio kupigia kura ccm kwa ridhaa yao.
Kitendo cha kutotolea ufanunuzi kuapishwa yule mbunge wa Nkasi, kwa waelevu chadema ni waganga njaa tu
 
Kitendo cha kutotolea ufanunuzi kuapishwa yule mbunge wa nkasi,kwa waelevu cdm ni waganga njaa tu

Msimamo wa chama uko wazi kuwa uchaguzi ule haukuwa halali. Hata huyo mbunge hayuko kwa baraka za chama bali alikimbilia. Maadamu alilazimisha kuwa kuchaguliwa na wananchi, busara ilitumika kumpotezea. Na ndio maana huoni chama kikijihusisha na yeye wala kumjadili ili asitumike kwenye propaganda mfu za kuchafua haiba ya chama. Kirahisi hivyo.
 
Kinachowaumiza vyama vya upinzani ni tamaa na uroho wa vyeo. Hivi kwa mfano Maalim Seif angeukataa umakamu wa kwanza wa rais feki kule zanzibar angekosa nn? VIP halima mdee asingeenda kujiapisha bungeni Maisha yasingeenda? Msimamo ni muhimu Sana kwa taasisi.
 
Msimamo wa chama uko wazi kuwa uchaguzi ule haukuwa halali. Hata huyo mbunge hayuko kwa baraka za chama bali alikimbilia. Maadamu alilazimisha kuwa kuchaguliwa na wananchi, busara ilitumika kumpotezea. Na ndio maana huoni chama kikijihusisha na yeye wala kumjadili ili asitumike kwenye propaganda mfu za kuchafua haiba ya chama. Kirahisi hivyo.
So chama kitapokea ruzuku kupitia yule mbunge?
 
Back
Top Bottom