Suphian Juma: Nimeng'atuka ACT Wazalendo

NIMENG'ATUKA ACT WAZALENDO-SUPHIAN.

Najua wengi mmeumia sana. Mmestaajabishwa mno na maamuzi ya Chama changu cha ACT wazalendo kukubali kuungana na Serikali ya Magufuli na Mwinyi tuliyoitangazia dunia imeunajisi Uchaguzi Mkuu wa Tanzania wa mwaka 2020.

Kitendo cha Chama kukubali kupeleka jina la Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar, na kuridhia kuapishwa wabunge wake; naelewa na naona wengi wananchi wenzangu si tu kimewakasirisha kupitiliza ila bali pia kimewatolea imani katika kuwaamini wanasiasa na vyama vya upinzani nchini.

Wengi tangu Jana Desemba 06, 2020 Chama kilipotangaza uamuzi wake huo kupitia Katibu Mkuu, rafiki yangu Ado Shaibu mmeendelea kuniuliza msimamo wangu mtandaoni, kwa simu hadi ana kwa ana kwa kuzingatia mimi kama mwanachama na Mtanzania ninayependa na kuheshimu Haki za Binadamu na Demokrasia, hivyo hakika nasema hampo peke yenu, Masikitiko yenu Watanzania wenzangu ni masikitiko yangu pia.

Uchaguzi ulikuwa batili, uongozi uliopatikana na unaoendelea kupatikana na uchaguzi huu ni batili pia. Haramu haijawahi kuwa halali. SIMPLE MATHEMATICS.

Kwangu mimi Suphian, ndoto yangu kuu ya kuona Taifa langu huru na lenye kufuata misingi ya Haki ni Lulu zaidi ya maslahi ya Chama cha siasa nilipo au yeyote ninayemwamini katika Siasa au nje ya siasa.

Kama nilivyoahidi wakati wa Sakata la Wabunge 19 wa CHADEMA, kwamba siwezi kumumunya maneno pale haki ikipindishwa hata kama na Chama changu, hivyo NATANGAZA: SIUNGI MKONO MAAMUZI YA CHAMA CHANGU.

Hivyo naomba dunia ijue kuanzia Leo Desemba 07, 2020 mimi Suphian Juma Nkuwi rasmi NANG'ATUKA UANACHAMA wa ACT wazalendo ili kusimama na HAKI, kusimama na familia za ndugu waliouawa, kutekwa, kufungwa na kuumizwa wakipigania Uchaguzi Huru, Haki na unaoaminika.

Asante Kiongozi wa ACT wazalendo na Kaka yangu, Zitto Kabwe na Chama kwa ujumla kwa malezi yenu ya KUSIMAMA NA HAKI mliyonipatia tangu mwaka 2015 nilipojiunga nanyi, nawatakia kila kheri.

Suphian Juma,
Aliyekuwa Mgombea Ubunge, ACT wazalendo 2020-2025 Singida Magharibi.

Desemba 07, 2020.

Hongera kwa kusimamia unachokiamini.
 
Dunia ijue??wanyaturu wenzio singida tuu hawana habari naujinga wenu ACT
 
Upo sahihi
Ila hata uchaguzi wa 2015 walikuja na ngonjera kama hizo na hatimaye walikwenda bungeni kuapishwa.
Tofauti kubwa aliojiktokeza kwa mwaka huu ni kukosekana kwa kundi kubwa la wabunge tu.
Unafikiri ni sababu zipi zimefanya hilo kundi kubwa la wabunge likosekane?
 
Upo sahihi
Ila hata uchaguzi wa 2015 walikuja na ngonjera kama hizo na hatimaye walikwenda bungeni kuapishwa.
Tofauti kubwa aliojiktokeza kwa mwaka huu ni kukosekana kwa kundi kubwa la wabunge tu.
Wabunge 117+ wa upinzani.... Yes waliibiwa kura lakini walau kuna sizeable chunk ya kuendeleza harakati.

Kura za Urais huwezi pinga mahakamani but still 6 million votes hta kma umeibiwa ni statement victory ya upinzani kupata basis ya kuimaliza CCM.

Hata Lissu angepewa 40% then wabunge walau 100 CHADEMA wasingesusa coz walau ingekuwa karibu na ukweli kuliko huu upuuzi uliotokea.

Embu tuwe realistic.... Kikwete alishinda urais kwa 80% ila wapinzani walikua na wabunge zaidi ya 50!
 
Upeo wako katika siasa ni mdogo saaaana! Suala la Serikali ya Umoja wa Kitaifa ni suala la Katiba ya Zanzibar! Wewe kafanye kazi ya urembo huna mwonekano wa kisiasa ndani ya kichwa chako na hata mwonekano wa mwili wako.
Mwaka 2016 halikua la kikatiba? Mbona ni optional wapi wamesema ni mandatory? Kwani uchaguzi huru na haki haipo kikatiba? Viti maalum haipo kikatiba? Mbona CHADEMA walivigomea?

Weird
 
Halima aliuliza "Hatukuukubali uchaguzi wa 2010, wa 2015 lakini tuliingia bungeni. Nini cha tofauti 2020?
Tofauti ni magnitude ya wizi haijawahi tokea upinzani upate madiwani 8 nchi nzima na ipate mitaa 10 tu nchi nzima na kuambulia majimbo mawili bara.

Hili halijawahi kutokea na ndio tofauti na chaguzi zingine.
 
Ngoja tuone ila dogo kaanza kurusha madongo upinzani mapema hana stamala kabisa na baada ya jiwe kuondoka mamluki wengi watafukuzwa CCM sio mbali ni 2025-26 hapo.
Si unajua JIWE mtu wa kuingizwa CHAKA ,watu washakaa mezani na Dogo atapewa SHAVU tu.
 
Ngoja tuone ila dogo kaanza kurusha madongo upinzani mapema hana stamala kabisa na baada ya jiwe kuondoka mamluki wengi watafukuzwa CCM sio mbali ni 2025-26 hapo.
Ameondoka ACT, that's the point. Hawana Mbunge, hawana Diwani, hata mmoja, hawana vitimaalum, hawana ruzuku. Zanzibar wanao watatu tu kwa hiyo watakula nini bila kutegemea Waarabu? Hiyo ya kujiunga au kutojiunga CCM ni janjanjanja tu sitegemei hata kama CCM watamchukua.
 
Mtu yeyote anayehama hama vyama huwa namuona hana uwezo mzuri wa kufanya maamuzi.
 
Ndo huyu anayesema na msigwa?
NIMENG'ATUKA ACT WAZALENDO-SUPHIAN.

Najua wengi mmeumia sana. Mmestaajabishwa mno na maamuzi ya Chama changu cha ACT wazalendo kukubali kuungana na Serikali ya Magufuli na Mwinyi tuliyoitangazia dunia imeunajisi Uchaguzi Mkuu wa Tanzania wa mwaka 2020.

Kitendo cha Chama kukubali kupeleka jina la Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar, na kuridhia kuapishwa wabunge wake; naelewa na naona wengi wananchi wenzangu si tu kimewakasirisha kupitiliza ila bali pia kimewatolea imani katika kuwaamini wanasiasa na vyama vya upinzani nchini.

Wengi tangu Jana Desemba 06, 2020 Chama kilipotangaza uamuzi wake huo kupitia Katibu Mkuu, rafiki yangu Ado Shaibu mmeendelea kuniuliza msimamo wangu mtandaoni, kwa simu hadi ana kwa ana kwa kuzingatia mimi kama mwanachama na Mtanzania ninayependa na kuheshimu Haki za Binadamu na Demokrasia, hivyo hakika nasema hampo peke yenu, Masikitiko yenu Watanzania wenzangu ni masikitiko yangu pia.

Uchaguzi ulikuwa batili, uongozi uliopatikana na unaoendelea kupatikana na uchaguzi huu ni batili pia. Haramu haijawahi kuwa halali. SIMPLE MATHEMATICS.

Kwangu mimi Suphian, ndoto yangu kuu ya kuona Taifa langu huru na lenye kufuata misingi ya Haki ni Lulu zaidi ya maslahi ya Chama cha siasa nilipo au yeyote ninayemwamini katika Siasa au nje ya siasa.

Kama nilivyoahidi wakati wa Sakata la Wabunge 19 wa CHADEMA, kwamba siwezi kumumunya maneno pale haki ikipindishwa hata kama na Chama changu, hivyo NATANGAZA: SIUNGI MKONO MAAMUZI YA CHAMA CHANGU.

Hivyo naomba dunia ijue kuanzia Leo Desemba 07, 2020 mimi Suphian Juma Nkuwi rasmi NANG'ATUKA UANACHAMA wa ACT wazalendo ili kusimama na HAKI, kusimama na familia za ndugu waliouawa, kutekwa, kufungwa na kuumizwa wakipigania Uchaguzi Huru, Haki na unaoaminika.

Asante Kiongozi wa ACT wazalendo na Kaka yangu, Zitto Kabwe na Chama kwa ujumla kwa malezi yenu ya KUSIMAMA NA HAKI mliyonipatia tangu mwaka 2015 nilipojiunga nanyi, nawatakia kila kheri.

Suphian Juma,
Aliyekuwa Mgombea Ubunge, ACT wazalendo 2020-2025 Singida Magharibi.

Desemba 07, 2020.

Itabidi wadau humu mum tag mwana 😂😂

Ova
 
Suphian Juma shoga kutokana na maelezo ya msigwa
 
Back
Top Bottom