Sumaye ndani ya Uingereza!

Status
Not open for further replies.

kanda2

JF-Expert Member
Apr 22, 2007
1,318
72
Waziri mkuu mstaafu bwana sumaye alikwenda uingereza kwa ajili ya matibabu (medical check up).

Lakini badala ya kuwa hospitalini amekuwa akizurura kwenye miji ya uingereza kuhubiri dini,kama mgonjwa aliyetakiwa kupata matibabu nje ya nchi asingekuwa na nguvu ya kuzurura kwenye miji mbalimbali badala ya kuwa hospitali au kama ugonjwa wake haukuwa mkubwa kwanini atumie pesa za kodi kwenda nje? Wakati mwakyembe anapata huduma muhimbili?

,habari yake iko kwenye tanzania daima kwenye habari kuu maoni au kwenye picha za mtandao wa tzuk,com kwenye picha utamuona mheshimiwa sumaye akiwa kwenye ibada.

Hakatazwi kufanya ibada ila iwe kwa pesa zake sio kodi za wananchi.
 
Mkuu Kanda2, "medical check up" haimaanishi kwamba mtu anaefanyiwa ni mgonjwa. Haswa kwa viongozi wetu, wapo entitled kwa medical check up nje ya nchi. Kwa kifupi ni kucheki hali ya afya yako sio kusubiri hadi ukiwa mgonjwa.

What a man does in his spare time after the medical check up is none of our business, kwani hayupo answerable kwetu. Habari ndio hiyoo!
 
Ina maana alijigharamia yeye mwenyewe kwenda kwenye mahubiri?lazima ubalozi ulimuandalia gari n.k
 
Jibu la swali lako sitaweza lijua, ila common sense tells me huyu ni waziri mkuu mstaafu, na wakati wa trip yake hii atakua anaalikwa sehemu nyingi, utakuta kama ni sehemu ambayo inahusisha ubalozi basi ataandaliwa usafiri na mtu watoka ubalozini kufuatana nae, na kama sehemu inayomualika ni sehemu nje ya userekali... basi wao wanaweza muandalia usafiri, chakula, n.k.

Lets not jump to conculsions without putting a little thought and research katika habari tunazo ambiwa, soma au hata ambia watu wengine...
 
Kah! Wewe mwenyewe umesema amekwenda kwa medical check up, na siyo kwamba amekwenda kulazwa hosp kutibiwa, kuna sababu gani ya yeye kutokwenda kwenye nyumba ya ibada kumshukuru Mungu wake kwa yote aliyomjalia? Na je, kama angeonekana kwenye Nght Clubs ingekuwa vipi? Jamani huyu ni Waziri mkuu mstaafu ambaye pension pamoja ma mafao yake mengine yamewekwa kisheria. Dr. Mwakyembe Kutibiwa Muhimbili hakumaanishi kwamba anabaniwa. Tumeshuhudia watu wengi tu wakiwemo wabunge wakipelekwa nje pale umuhimu wa kufanya hivyo unakuwepo, kwanini kwa Sumaye iwe issue! Au ni kwa kuonekania Kanisani?
 
Ah eeehe!
Kama yupo huko na ana nguvu ya kutembea sidhani kama ni dhambi kupuyanga mitaani kidogo. Ulitaka aishi wodini kama asiyejiweza???
Nadhani hapa tujadili ubora wa huduma zetu za afya kiasi kwamba viongozi (watunga sera) wanaogopa na kwenda kutibiwa nje. Ila kuhusu routes zao wakishafika huko si suala kuntu sana kwani tukishatatua tatizo la wao kukimbilia nje kila asubuhi basi hilo suala la kupuyanga litajitatua automatikali.
 
Bush, Clinton, Mama C. Rice wakiamua kuja Tanzania on a private visit, nani atalipa expenses zao ikizingatiwa wao bado wanalindwa na kusafiri na msafara wa watu wengi?
Ninachotaka kusema kuwa stahili zao huwa zipo kisheria. Hivyo hivyo kwa wastaafu DGI, Generals, Maj Generals, CS, CJ IGP. nao pia wana stahili zao hapa Tanzania kwa mujibu wa sheria zetu.
 
Waziri mkuu mstaafu bwana sumaye alikwenda uingereza kwa ajili ya matibabu(medical check up).

Lakini badala ya kuwa hospitalini amekuwa akizurura kwenye miji ya uingereza kuhubiri dini,kama mgonjwa aliyetakiwa kupata matibabu nje ya nchi asingekuwa na nguvu ya kuzurura kwenye miji mbalimbali badala ya kuwa hospitali au kama ugonjwa wake haukuwa mkubwa kwanini atumie pesa za kodi kwenda nje? Wakati mwakyembe anapata huduma muhimbili?

.....Hakatazwi kufanya ibada ila iwe kwa pesa zake sio kodi za wananchi.

Acha wivu na majungu, unamuonea gere Sumaye, hiyo ni husuda, msione mwenzenu akifaidi, acha roho ya korosho, mwache atumie. Hata yeye analipa kodi, alaaaaa.

Mod thread ya majungu hii, mmeiona au hadi kuireport?
 
Ina maana alijigharamia yeye mwenyewe kwenda kwenye mahubiri?lazima ubalozi ulimuandalia gari n.k

Tofautisha kati ya kwenda kwenye mahubiri na kuhubiri dini. Kiini cha kwenda UK ni Medical Check Up, na anastahili pia kutumia gari aliloandaliwa na balozi kwenda kusali. Ulitaka atembee kwa miguu kubana matumizi ya serikali!
 
Ah eeehe!
Kama yupo huko na ana nguvu ya kutembea sidhani kama ni dhambi kupuyanga mitaani kidogo. Ulitaka aishi wodini kama asiyejiweza???
Nadhani hapa tujadili ubora wa huduma zetu za afya kiasi kwamba viongozi (watunga sera) wanaogopa na kwenda kutibiwa nje. Ila kuhusu routes zao wakishafika huko si suala kuntu sana kwani tukishatatua tatizo la wao kukimbilia nje kila asubuhi basi hilo suala la kupuyanga litajitatua automatikali.

Miaka 48 baada ya uhuru bado tunarudi kwa watawala wetu kwa ajili ya medical check-up! Kama mlivyotufahamisha tusiojua, medical check up si lazima uwe mgonjwa basi kwanini hawa wakuu wasionyeshe uzalendo wao kwa kufanyiwa check-up hapo nyumbani na waende nje kwa tiba tuu! Kama ni check-up ya kufuatilia tiba ya awali basi ni haki yake. Lakini na yenyewe iwe na kikomo. Mtu akiwa fit kuzunguka kuhubiri basi frequency ipunguzwe. Tuwaonee huruma wenzetu ambao hata mkunga wanamsikia redioni!

Amandla.........
 
Umetuambia:
Sumaye afanya utapeli wa kodi yetu
Halafu tena unatuuliza:
Ina maana alijigharamia yeye mwenyewe kwenda kwenye mahubiri?
Baada ya kuangalia title yako nilitegemea una information zote jinsi huo utapeli ulivyofanyika, lakini inaelekea unataka majibu humu, ndo maana unarudi kuuliza. Maybe huko ulikokuita 'kuzurura' ilikuwa ni sehemu ya maelekezo ya daktari, na nimesema 'maybe' kwa kuwa sijui na wewe pia hujui. Tukae kimya kusubiri anayejua!!!
 
Kwa nini tusiboreshe huduma zetu au kukawa na hosp. moja maalumu Tz kwa kucheki afya za vingozi?

Hospitali kubwa kama KCMC unawapa uwezo wa vifaa na madaktari na ikibidi hata unaleta na madaktari toka nje!

The same applies kwa shule za serikali

Hivi lini huduma zitakaa ziboreke wakati viongozi hawatibiwi huko?

Au nje ni kujustfy ulaji wa pesa?
 
Miaka 48 baada ya uhuru bado tunarudi kwa watawala wetu kwa ajili ya medical check-up! Kama mlivyotufahamisha tusiojua, medical check up si lazima uwe mgonjwa basi kwanini hawa wakuu wasionyeshe uzalendo wao kwa kufanyiwa check-up hapo nyumbani na waende nje kwa tiba tuu! Kama ni check-up ya kufuatilia tiba ya awali basi ni haki yake. Lakini na yenyewe iwe na kikomo. Mtu akiwa fit kuzunguka kuhubiri basi frequency ipunguzwe. Tuwaonee huruma wenzetu ambao hata mkunga wanamsikia redioni!

Amandla.........

Fundi Mchundo:

Chukua nchi. Nitaukana uraia wa kimarekani na kurudi bongo.
 
Waziri mkuu mstaafu bwana sumaye alikwenda uingereza kwa ajili ya matibabu(medical check up).

Lakini badala ya kuwa hospitalini amekuwa akizurura kwenye miji ya uingereza kuhubiri dini,kama mgonjwa aliyetakiwa kupata matibabu nje ya nchi asingekuwa na nguvu ya kuzurura kwenye miji mbalimbali badala ya kuwa hospitali au kama ugonjwa wake haukuwa mkubwa kwanini atumie pesa za kodi kwenda nje? Wakati mwakyembe anapata huduma muhimbili?

,habari yake iko kwenye tanzania daima kwenye habari kuu maoni au kwenye picha za mtandao wa tzuk,com kwenye picha utamuona mheshimiwa sumaye akiwa kwenye ibada.

Hakatazwi kufanya ibada ila iwe kwa pesa zake sio kodi za wananchi.

Inaweza kuonekana kuwa ni sawa kwake kutembeatembea, na kweli si vibaya, ila tungekuwa tunajua gharama wanazotayarishiwa hawa wanaoenda medical check up tungeweza kujadili zaidi. Inawezekana kuna fungu maalum limewekwa na ni kubwa kiasi kwamba linaacha nafasi ya baada ya checkup mtu kuendelea kutanua huko huko. Hapo kutakuwapo tatizo na kama fungu hilo limeachwa wazi tu yaani mtu atumie mpaka atakapotaka kurudi, basi ni tatizo pia.
Kuna wakati waziri mkuu mwingine alitumia nafasi ya ziara yake kikazi kwenda kuwatembelea wanae, nayo ilikuwa issue.
Lamsingi ni serikali kuwa transparent, kutueleza gharama kama hizo zimegharimu kiasi gani na kama kungekuwapo na uwezekano wa kuzipunguza, ikiwa ni pamoja na kuboresha hospitali zetu.
 
Mimi sijaona tatizo kwa Waziri Mkuu mstaafu kwenda kufanya medical check up UK,na sasa baada ya medical check up hali yake inaonekana ni nzuri je unategemea akae kwenye nyumba tuu alimofikia? nafikiri sio sahihi.Yeye kama Mtanzania mwingine yeyote anauhuru wa kutembea na kujionea mambo pamoja na kujifunza pia.

Kwa yeye kuchagua kwenda kanisani ni kheri na sidhani kuwa ni kosa lakini tungeambiwa kuwa anavinjari kwenye night clubs hapo kweli tungepaswa kuuliza kulikoni kiongozi mstaafu kuvinjari kwenye night clubs?
 
Last edited:
acha wivu na majungu, unamuonea gere sumaye, hiyo ni husuda, msione mwenzenu akifaidi, acha roho ya korosho, mwache atumie. hata yeye analipa kodi, alaaaaa.

mod thread ya majungu hii, mmeiona au hadi kuireport?
wewe uliyeanzisha thread ya vakesheni ya issa michuzi ulikuwa unamuonea wivu,husuda,majungu,gere au kijicho?

Hukujua kama michuzi analipa kodi na kutoa zawadi kwa watanzania?

Katizame comments kwenye michuzi blog juu ya topic yako ya kijicho kwa michuzi.

Kama sumaye alikuwa hana ugonjwa wa kiasi hicho kwanini alipelekwa ulaya na kutumia kodi zetu kwenye mahubiri ya kidini? Lazima kuna walinzi wanaolipwa kwa kodi zetu wameongozana nae.

Au baada ya kumaliza check up arudi nyumbani kwani lazima awe anaishi hotelini akiwa uingereza na chumba chake pekee yake hakipungui pounds elfu mbili kwa siku,bado wapishi na walinzi.huu ni utapeli wa kodi za wananchi.
 
Mimi sijaona tatizo kwa Waziri Mkuu mstaafu kwenda kufanya medical check up UK,na sasa baada ya medical check up hali yake inaonekana ni nzuri je unategemea akae kwenye nyumba tuu alimofikia? nafikiri sio sahihi.Yeye kama Mtanzania mwingine yeyote anauhuru wa kutembea na kujionea mambo pamoja na kujifunza pia.

Kwa yeye kuchagua kwenda kanisani ni kheri na sidhani kuwa ni kosa lakini tungeambiwa kuwa anavinjari kwenye night clubs hapo kweli tungepaswa kuuliza kulikoni kiongozi mstaafu kuvinjari kwenye night clubs?

Hata mimi nisingeona tatizo isingekuwa wakina mama zaidi ya 13,000 (9/11 zaidi ya nne) wanakufa kila mwaka kwa kukosa huduma bora wakati wa kujifungua! Hawa ndiyo waliotufikisha hapa, basi angalau wangeonyesha empathy kwa wenzao. Hatuombi makuu. Wakunga na vifaa vya kutoa huduma wakati wa kujifungua katika kila zahanati. Wakati tukisubiri hilo, basi hizo check-up wafanyie kwenye hospitali za nchini kwetu sote.

Amandla......
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom