Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,555
- 41,066
Nchi yetu bado ni miongoni mwa nchi 50 maskini sana Duniani, yenyewe ikishikila nafasi ya 27 kwa umaskini, huku Burundi ikishika nafasi ya kwanza katika Dunia, na DRC nafasi 5 Duniani. Kwa kiasi kikubwa umaskini huu unaochangiwa na uongozi mbaya, uongozi usio na maono wala uthubutu.
Kiongozi aliyevunja rekodi ya Afrika kwa kuzurura na watu wengi Duniani anapoenda kwenye mataifa mengine ni Mobuto Seseko, aliyekuwa Rais wa DRC (wakati huo Zaire). Huyu alikuwa akizurura kwenye mataifa mengine akiwa na wapambe wa kuzurura naye wapatao 200. Kama uzururaji wa kiongozi mkuu wa nchi na kundi kubwa la watu kungekuwa kunaondoa umaskini, basi DRC pengine ilistahili kuwa nchi ya 5 kwa maendeleo badala ya kuwa nchi ya 5 kwa umaskini Duniani.
Wakati wa utawala wa awamu ya 4, kiongozi mkuu wa nchi alipewa jina la Rais mtalii na wakati mwingine Vasco Dagama, kwa sababu ya wakati wote kufanya utalii kwenye mataifa mengine. Lakini angalao alikuwa na timu ndogo ya watu aliokuwa anatalii nao.
Kiongozi wetu wa sasa anatafuta kuvunja rekodi ya kuzurura na kundi kubwa la watu kwenye mataifa mengine. Safari yake ya India, aliteua watu wa kuzurura nao wapatao 100, wote wakitumia kodi za Watanzania, walio wengi wakiishi kwenye umaskini kiasi hata cha kushindwa kuhudhuria hata baadhi ya misiba ya ndugu zao kwa kukosa nauli. Lakini kodi yao, kiongozi wao hana machungu nayo, anaamua kuitumbua kwa starehe pamoja na wale aliowateua kwa wakati husika.
Sijui kiongozi kwa kuzurura huko nje na kundi kubwa la watu, anataka kutatua nini. Labda kwa sababu watu wamekuwa wakimlaumu kwa safari zake zisizo na tija, sasa ameamua kwenda na watu wengi, kuzurura nao, kutumbua pesa ya umma, kula vinono na starehe mbalimbali, ili hawa watu baada ya kuonjeshwa starehe zote huko nje, aone kama baada ya kurudi wataendelea kusema kuwa kuzurura nje ni kubaya. Au watasifia kuzurura kwenye mataifa mengine ili waendelee kukumbukwa kwenye starehe hizo za kuzurura kwa gharama ya wananchi.
Rekodi ya kwanza ya kuzurura nje na kundi kubwa la watu kwa pesa ya umma, ilivunjwa kipindi cha awamu ya pili mwaka 1992, ambapo kiongozi mkuu wa nchi alienda na ujumbe wa watu wapatao 90 huko Rio de Janeiro, nchini Brazil, ambapo kundi kubwa la hao watu hawakuingia hata kwenye ukumbi wa mikutano, badala yake waliishia kwenye maduka makubwa kufanya shopping. Wakarudi toka huko, hata wasijue mkutano wenyewe ulikuwa unahusu nini.
Walivyotua uwanja wetu wa ndege walipoulizwa ulikuwa ni mkutano wa nini, wakasema kuwa ulikuwa ni mkutano wa Mazingira, kitu kilichoashiria kuwa walikuwa ni watu wajinga kabisa ambao walishindwa hata kuelewa kuwa mkutano huo ulikuwa ni wa SUSTAINABLE DEVELOPMENT, ambao ndani yake, mazingira ilikuwa component tu. Miaka mitano baadaye, UNDP ilishangazwa na Tanzania kushindwa kutekeleza hata azimio moja la maazimio ya Rio de Janeiro.
Sababu ilikuwa ni dhahiri, kiongozi alienda kuzurura na kundi kubwa la wazururaji ambao kwao kilichokuwa muhimu ni kupata nafasi ya kutumbua kodi.
Rekodi hii ya awamu ya pili ya kuzurura na kundi kubwa nje, leo inavunjwa na bintiye.
Rais Mkapa aliwahi kusema:
"Kama kukitokea kiongozi yeyote akakuambia kuwa huko nje kuna pesa nyingi inayoweza kuiletea Tanzania maendeleo, mwambie mjinga wewe"