Kwanini wagonjwa wamepungua hospitalini baada ya sheria mpya ya bima ya afya NHIF?

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
876
4,101
Kuna upungufu wa wagonjwa hospitalini hasa wazee na watoto. Wanafunzi wanarejea nyumbani badala ya kupelekwa hospital wanapoumwa. Muda wanaotumia wanafunzi kufuatilia bima ya afya ni mwingi kuliko muda wa masomo.

Kadi za bima kwa wanafunzi hazitoki na mara nyingi utoka wanapomaliza mwaka kwa lengo la kuthibitisha malipo ya awali . Unapewa bima inayomalizima muda mwezi mmoja then ukianza next year ya masomo unaanza upya kulipia 54k na kujaza maombi upya.

Wizara ikitoa takwimu za wanafunzi wenye bima nchini its almost 20% ya wanafunzi wote below and above 18 years

Hizi taarifa vyombo vya habari vimekatazwa kuziripoti. Mfano SAUT mwanza wanafunzi wanalalamika ila wakiita vyombo vya habari vinaingia mitini.

Hali hii ya walipa kodi kukosa huduma ya afya itaisha lini nchi? Hao wanaoshindwa kufika hospitali huko majumbani wanajitibu vipi? Wanafunzi kutopewa vitambulisho pamoja nakulipia 54k ni maelekezo ya wizara kama NHIF inavyojibu walimu? Panahitaji muda gani kumsajili mwanafunzi na kumpa namba ya utambulisho? Kwanini waombaji wasingepigwa picha unapokwenda hospital ukitaja jina lako mtoa huduma anasearch na kulinganisha sura na taarifa then unaproceed na matibabu bila ulazima wa kadi. Sometimes mtu anaweza akafoji kadi akaweka na picha yake huku namba na majina si yake kwa kutambua tu kwamba hospitali wanaangalia sura ya kwenye kadi na siyo sura kwenye database.

Afya siyo anasa na hakuna mtu anatamani kuumwa......tuache urasimu hizi ni kodi za qananchi
 
Back
Top Bottom