Kifo cha upasuaji wa kuinua makalio chasababisha Uturuki na Uingereza kufanya mkutano

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,331
33,141
w

CHANZO CHA PICHA,NATASHA KERR
Maelezo ya picha,
NATASHA KERR

Serikali ya Uingereza imesema itakutana na maafisa nchini Uturuki kujadili kanuni kuhusu utalii wa kimatibabu na urembo, kufuatia vifo kadhaa.
Melissa Kerr, 31, alikufa katika Hospitali ya kibinafsi ya Medicana Haznedar mjini Istanbul mnamo 2019 wakati wa upasuaji wa kuongeza makalio (Brazilian butt-lift).
Mchunguzi wa maiti aliibua wasiwasi yeye na wengine kwasababu hawakupewa taarifa za kutosha kabla ya kusafiri nje ya nchi.
Waziri wa afya Maria Caulfield alisema serikali ilichukulia suala hilo "kwa uzito".
Katika majibu yake kuhusu ripoti ya kuzuia vifo vya siku zijazo iliyoandikwa na mchunguzi mkuu wa miili Norfolk Jacqueline Lake, Bi Caufield alisema maafisa kutoka Idara ya Afya na Huduma ya Jamii "watatembelea Uturuki hivi karibuni kukutana na wenzao".
g

CHANZO CHA PICHA,NATASHA KERR
Maelezo ya picha,
Baada ya kifo chake, familia ya Melissa Kerr ilisema inatumai wengine wataepuka "utalii wa vipodozi"

Mnamo Septemba, uchunguzi uligundua kuwa Bi Kerr, kutoka Gorleston, Norfolk , aliteseka na donge la damu ambalo lilisafiri hadi kwenye mapafu yake wakati wa upasuaji wa kuinua makalio nchini Brazil (BBL).
Wachunguzi waliambiwa shughuli za BBL zilikuwa za hatari kubwa zaidi ya taratibu zote za upasuaji wa urembo.
Uingereza imekubali kusitishwa kwa operesheni kama hizo kutokana na hatari zinazohusika .
Bi Lake aliamua kuwa Bi Kerr hakupewa taarifa za kutosha kufanya uamuzi salama na akasema "hatari kwa raia wanaoendelea kusafiri nje ya nchi kwa taratibu hizo inaendelea... na nina Imani kwamba vifo vijavyo vinaweza kuzuilika kwa njia ya utoaji taarifa bora".
Mama huyo wa watoto watatu alifarki mnamo Agosti 2020 baada ya kuchomwa liposuction nchini Uturuki na BBC hapo awali iliripoti jinsi wagonjwa saba wa Uingereza walivyofariki baada ya upasuaji wa kupunguza uzito nchini humo.
f

CHANZO CHA PICHA,NATASHA KERR
Maelezo ya picha,
Melissa Kerr alikufa wakati wa upasuaji wa urembo katika hospitali ya Uturuki mnamo 2019

Mnamo Septemba, uchunguzi ulisikika kuwa Bi Kerr, kutoka Gorleston, Norfolk , aliteseka na donge la damu ambalo lilisafiri hadi kwenye mapafu yake wakati wa upasuaji wa kuinua makalio nchini Brazil (BBL).
Wachunguzi waliambiwa shughuli za BBL zilikuwa za hatari kubwa zaidi ya taratibu zote za upasuaji wa urembo.
Uingereza imekubali kusitishwa kwa operesheni kama hizo kutokana na hatari zinazohusika .
Bi Lake aliamua kuwa Bi Kerr hakupewa taarifa za kutosha kufanya uamuzi salama na akasema "hatari kwa raia wanaoendelea kusafiri nje ya nchi kwa taratibu hizo inaendelea... na nina Imani kwamba vifo vijavyo vinaweza kuzuilika kwa njia ya utoaji taarifabora".
Mama huyo wa watoto watatu alifarki mnamo Agosti 2020 baada ya kuchomwa liposuction nchini Uturuki na BBC hapo awali iliripoti jinsi wagonjwa saba wa Uingereza walivyofariki baada ya upasuaji wa kupunguza uzito nchini humo.
h

CHANZO CHA PICHA,GOOGLE
Maelezo ya picha,
Bi Kerr aliugua ugonjwa wa kuganda kwa damu katika Hospitali ya Medicana Haznedar wakati wa upasuaji mjini Istanbul

Mhafidhina Bi Caulfield, waziri wa afya ya akili na mkakati wa afya ya wanawake, alitoa "rambirambi zake za dhati" kwa familia ya Kerr na kusema: "Ni muhimu tujifunze kutokana na kile kilichompata ili kuzuia vifo vya siku zijazo."
Alisema serikali inafahamu ukaguzi uliofanywa na baadhi ya nchi zinazotoa "utalii wa afya... huenda usilingane na viwango vya udhibiti wa Uingereza" lakini kwamba "uwazi na viwango hivyo ni muhimu ili kupunguza hatari zinazoweza kutokea kwa wagonjwa".
f

CHANZO CHA PICHA,NATASHA KERR
Maelezo ya picha,
Ripoti ya kuzuia vifo vya siku zijazo ilitumwa kwa waziri wa afya ili kujaribu kuwaonya watu wengine kuhusu kusafiri kwenda Uturuki kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji wa urembo

"Ni muhimu sana kwamba wale wanaofikiria kufanya utaratibu wa kuinua makalio (BBL) wa Brazil wafahamishwe kikamilifu kuhusu hatari na wawe na wakati wa kutafakari kikamilifu uamuzi wao kabla ya upasuaji," alisema Bi Caulfield.
"Hatari ya kifo kwa upasuaji wa BBL ni angalau mara 10 kuliko taratibu nyingine nyingi za urembo."
Serikali ilikuwa inafikiria jinsi ya "kuwasilisha kwa ufanisi" habari kuhusu hatari za kwenda nje ya nchi, alisema.
Waziri huyo alisema wakati serikali ya Uingereza inaangalia duniani kote "matokeo ya utalii wa kimataifa wa afya... tuna nia kubwa nchini Uturuki kutokana na idadi ya raia wa Uingereza wanaosafiri kwenda nchini humo kwa matibabu". chanzo. Kifo cha upasuaji wa kuinua makalio chasababisha Uturuki na Uingereza kufanya mkutano - BBC News Swahili
TAHADHARI::
Jamani dada zangu munaotaka kuongeza Makalio yenu acheni kabisa mawazo ya kwenda nchini Uturuki kuongeza makalio wata kumalizeni Waturuki hawana ujuzi wa kuongeza makalio. Madaktari wengi wa Uturuki ni Ma-Daktari feki kuweni makini sana na suala la kuongeza Makalio. Nitafuteni mimi niwape dawa zangu za Asili za kuongeza Makalio zisizo na madhara yoyote yale. Kwa mwenye kutaka kuongeza makalio anitafute kwa wakati wake.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom