Sumaye kuwa Katibu Mkuu CHADEMA?

Hivi Chadema ni chama cha watu wa Kaskazini tu,mimi nilidhani,huo ukatibu mkuu lazima apewe mtu wa kaskazini?mgombea uraisi kaskazini,mwenyekiti,kaskazini,katibu mkuu kaskazini,wakuu wa vitengo kaskazini,hiki sio chama bali ni klabu.

Sasa kama nyie watu wa kanda zingine mko waoga hamuwezi kujitokeza waziwazi kuikabili serikali mpewe tu huo ukatibu kwa fadhila au ?????????!!

Sumaye na Lowassa walionyesha ujasiri na kujitokeza waziwazi kuwa kinyume cha DOLA dhidi ya wanayoyaamini na hayo ndo watu wengi hawana na hawawezi kuthubutu
 
Tukiachana na dhana kulipa fadhila au deni. Je Sumaye anafaa au hafai? Je ataweza kuongoza mapambano kama ilivyokuwa kwa mtangulizi wake Dr Slaa ingawa aliamua kukabidhi silaha kwa adui?

Mhe. Sumaye anafaa kabisa kuwa katibu mkuu.
 
hahahahaha!!!! CDM Ndio basi tenaaa!!! wapiga dili washakivamia .....
 
Hizi ni habari za uhakika kabisa... Na hauto fanyika uchaguzi bali atapewa hicho kiti kwakuwa ni mtu wa Mgombea Urais..
Hili ni deni lingine ambalo chadema wanamlipa Lowasa..

Wewe mkuu una akili sana,deni la mwisho ambalo chadema lazima wamlipe lowasa kwa mujibu wa makubaliano rasmi yaliyosainiwa kwa mwanasheria ni nafasi ya Mwenyekiti wa chama.

Hizi ni habari za kuaminika ingawa najua manyumbu yatakuja kwa fujo hapa,lakini mwishowe yote yataangukia mtoni na kuliwa na Mamba
 
Meela mtizamo wako umefanana na wangu.Sumaye alileta ile dhana ya fisi na mkono wa binadamu kwamba utadondoka kama unakumbuka mr z alivyokuwa anamponda lowasa kuwa anajifanya mradi wa kahama kuwa kete yake ya kisiasa wakati ilikuwa ni muendelezo wa watangulizi wake.
 
ZERO huyuhuyu ninayemfahamu? Ambaye alikuwa waziri mkuu kwa miaka 10 na serikali haikufanya chochote kama yeye mwenyewe alivyokuwa anajitusi mchana kweupe? Duh! kama ni kweli basi CCM ina raha saaaana! Maana B yake itazidi kutamalaki upande wa pili. Ama kweli ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni!!!
 
WanaJF
Waziri mkuu mstaafu Mh Frederick Sumaye amejiunga rasmi na CHADEMA mjini Arusha kwenye mkutano wa kufunga kampeni za kumnadi Godbless Lema.

Haya ni maandalizi ya awali ya kumwandaa Sumaye kushika nafasi ya ukatibu mkuu wa CHADEMA, nafasi iliyoachwa na Dr. Slaa.

Tusubiri
Anafaa
 
Wakati mwingine kununua mchezaji kwa bei mbaya kwa ajili ya kusaidia timu sio.dhambi,
Dr slaaa kahamia timu.pinzani,sio.mbaya kwa wao kutafuta mchezaji mpya wa kujaza nafasi
 
sijui kwanini sikuzaliwa kaskazini
one day ningekuwa mtu ndani ya CHADEMA.......
 
Mkuu hivi mpaka leo bado unaacha akili zako kwenye vmakabati ya Nepi pale Lumumba?

Jitahidi uwe unatoroka mara mojamoja utaendelea kuwa kituko mpaka lini? Siamini kama hujui utaratibu wa upatikanaji wa Katibu mkuu ndani ya Chadema.... Siamini.

Hivi umemwona Laki si pesa wa leo? Wewe unasubiri nini? Jiongeze.

BACK TANGANYIKA

Au muulize jamaa kama amemuona MUSSA ALLAN wa leo
 
Last edited by a moderator:
Inatia huruma sana, hawa jamaa ndo angalau walikua na probability ya mbali sana kubadikusha mfumo wa Tanzania, ila wamemuweka kwanza Lowassa, sasa hivi wakimuongeza na huyu yaani chama kimekufa kabisa, wao watabaki kua kama TLP au vyama vingine ambavyo vipo tu ka havipo.
 
Kama ni kweli nazidi kuamini kuwa chadema ni chama cha kikanda. Chama cha kaskazini

Na hii ndiyo inaifanya Chadema haifi kwasababu tu ccm wanakipigia sera za Ukanda,Udini na Ukabila. Chama chochote cha upinzani ambacho hakipigiwi sera hizo lazima hakitakuwa.CUF na Chadema vimekuwa na kuimarika kwasababu ya ccm kuvipigia sera za udini ,ukanda na ukabila. Unapotaja tu Ukanda tayari kuna wafuasi wengi, ukitaja udini tayari kuna wafuasi wengi hata wale ambao walikuwa wamelala wanashtukakuwa kumbe chama chetu ni hiki! Ukitaja Ukabila tayari kuna wafuasi wengi. Ukiacha CUF na Chadema ambavyo vinatajwa kwa ukanda, ukabila na udini, vyama vya upinzani ambavyo havitajwi kabisa kwa ukanda, udini na Ukabila havina wafuasi wengi na vingine hata madiwani tu havina
 
Back
Top Bottom