Sumaye kuwa Katibu Mkuu CHADEMA?

Sumaye kuwa Katibu Mkuu CHADEMA?

Hizi ni habari za uhakika kabisa... Na hauto fanyika uchaguzi bali atapewa hicho kiti kwakuwa ni mtu wa Mgombea Urais..
Hili ni deni lingine ambalo chadema wanamlipa Lowasa..

Acha uzuzu wewe, nafasi ya ukatibu tangu lini Ni ya kuchaguliwa??????

Hii mizuzu mingine bana
 
Anafaa Sana Sana sanaaaaa


Tuache utani. Sumaye hafai kufanya chochote. Kwanza amechoka kisiasa. Baada ya kuwa Waziri Mkuu miaka 10 yeye ni senior kwa wote - Lowassa, Mbowe, Duni Duni, Mbatiya. Hatokubali na wala miiko ya siasa haitokubali. Hayo ni 9 la 10 ni kwamba hana akili. Ni Ziro. Mpeni Mnyika au Msigwa, they have been tried and tested. Lakini, kwani Lowassa ana cheo gani sasa hivi? Na Mbowe atapata adhabu gani kwa kushindwa kura kwa tamaa ya hela za Lowassa? Yaani atabaki hivi hivi? Wanachama wa.eridhika?
 
WanaJF
Waziri mkuu mstaafu Mh Frederick Sumaye amejiunga rasmi na CHADEMA mjini Arusha kwenye mkutano wa kufunga kampeni za kumnadi Godbless Lema.

Haya ni maandalizi ya awali ya kumwandaa Sumaye kushika nafasi ya ukatibu mkuu wa CHADEMA, nafasi iliyoachwa na Dr. Slaa.

Tusubiri

Itakuwa poa sana.
 
Hivi kweli chadema kama siyo ukanda, sumaye ana kipi kipya kwa Watanzania?
 
Nilitegemea a positive overhaul, watatumia hoja gani kushawishi watu? Katiba mpya? Ufisadi? HAPANA.
Chama kinakufa, ilitakiwa vijana wapewe uongozi, kina Mnyika! Sio wazee tena wenye makamdokando! Mbowe angejitoa tu uenyekiti achukue kijana, na katibu achukue kijana mwingine! Mbowe mapambano kashindwa! Kitu kimoja chadema wanatakiwa wajue, watanzania wengi sio wajinga, kama hawajajifunza somo! Hongera zao.
 
Hizi ni habari za uhakika kabisa... Na hauto fanyika uchaguzi bali atapewa hicho kiti kwakuwa ni mtu wa Mgombea Urais..
Hili ni deni lingine ambalo chadema wanamlipa Lowasa..
Pitia katiba za vyama,anzia ccm mpaka vyote,then utajua katibu wa chama hupatikanaje.Wakati fulani usipojua kukaa kimya kwenye jamvi kama hili utaelewa kupitia wenzio,soma mada kwanza uielewe ndo uchangie,Kinana hakuchaguliwa,Mangula hakuchaguliwa,Slaa hakuchaguliwa,Prof Safari hakuchaguliwa na mkutano,huteuliwa then vikao husika humpitisha kama anafaa.
 
Hizi ni habari za uhakika kabisa... Na hauto fanyika uchaguzi bali atapewa hicho kiti kwakuwa ni mtu wa Mgombea Urais..
Hili ni deni lingine ambalo chadema wanamlipa Lowasa..

Hivi kinana alipata kura ngapi? Hivi alimshinda nani vile!?
 
Wakati mwingine uwa nashangaa unafiki wa hawa Chadema sasa hivi wanalalamika Dr.Magufuli, kuwarudisha baadhi ya mawaziri wanasema wanataka sura mpya lakini kwenye chama chao wanamuandaa Sumaye kuwa kiongozi wa chama na mgombea urais 2020, huyu Sumaye ndiyo aje kupambana na Dr.Magufuli.

Huu msiba mkubwa kwa Chadema.
 
chadema mtu akiwa upande wao hata kama ni mbovu wao wasema anafaa Leo wanasema prof mhongo hafai ila ikitokea prof mhongo kesho akahamia upande wao utawasikia wakimnadi na kumuita msafi tuliona kwa mh Edward lowassa kabla walimpa kila a in a ya jina la ubaya lakini cha ajabu alipo temwa ccm na kuhamia upande wao wale wale waliosimama kweny majukwaa wakituhakikishia kuwa Edo no fisadi na ushahidi wanao cha ajabu wakadai Edo siyo mwizi na mwenye ushahidi aende mahakamani nikajiuliza ule ushahidi waliokuwa nao ukowapi watuletee ili tweende mahakamani.
Hawa hawa chadema walimtaja sumayi ni fisadi leo ni msafi kisa tu yuko upande wao.Kiukweli na ndy maana Mh Rais amepuuza maneno yao dhidi ya prof mhongo Jana nilimuona mnyika akimnadi mwizi wa nagari na kumponda prof mhongo.MWENYE CV YA SUMAYI AIWEKE HAPA TUONE
 
Sisi Wachaga Sio Wanafiki Hatuwezi kumpa Uongozi Mbulula Sijui wawapi ichi chama kitabaki Mikononi Salama kwa wachaga ..
 
Sumaye Cdm tunakuunga mkono na 2020 chukua fomu uikomboe Tanzania..
 
WanaJF
Waziri mkuu mstaafu Mh Frederick Sumaye amejiunga rasmi na CHADEMA mjini Arusha kwenye mkutano wa kufunga kampeni za kumnadi Godbless Lema.

Haya ni maandalizi ya awali ya kumwandaa Sumaye kushika nafasi ya ukatibu mkuu wa CHADEMA, nafasi iliyoachwa na Dr. Slaa.

Tusubiri

Yakitimia hayo CHADEMA itakuwa imetekwa na itakuwa na sifa zote za kuitwa CCM(B). Na kama CCM(A) ipo kwa nini tuchague CCM(B).

Go go go JPM, peleka wapinzani uchwara Makumbusho ya Taifa kwa kauli mbiu #Hapakazitu.
 
Nani awe katibu mkuu wa Chadema si ajenda tena ya watanzania. Sumaye awe katibu mkuu, Kingunge awe mwenezi, Lowassa mwenyekiti hakuna anayejali maana Magufuli akienda kwa spidi hii 2020 Chadema itakuwa goigoi kupita kupita leo.
 
  • Thanks
Reactions: nao
Sumaye Cdm tunakuunga mkono na 2020 chukua fomu uikomboe Tanzania..

Alikuwa Waziri Mkuu kwa miaka 10 hakukamata hata kontena moja lenye bidhaa zisizolipiwa kodi, mwenzake Majaliwa Kassim Majaliwa kakamata zaidi ya makontena 2500 ndani ya siku 10 tu za uongozi wake. Aje tu 2020 tumpe hukumu yake kama tulivyomfanya Lowassa.
 
Hii habari haiwezi kuwa kweli. Labda watu wengi hawafahamu. Sumaye na Lowassa hawapatani HATA KIDOGO. Mh Sumaye alishawishiwa kujiunga UKAWA bila Lowassa kujulishwa kwa sababu ilikuwa dhahiri asingekubali; ndio maana mwanzoni ilisemekana kuwa amehamia NCCR na wala sio CHADEMA. Taarifa zilizopo ni kuwa Sumaye alishawishiwa kujiunga UKAWA baada ya wanaUKAWA kudhani kuwa afya ya Lowassa haikuwa nzuri sana hivyo ilihitajika back-up. Kwa hiyo Lowassa alijiunga UKAWA kama back-up in case Lowassa akiishiwa nguvu ya kutekeleza majukumu. Na Lowassa hakujulishwa na wala hafurahii kuwa pamoja na Sumaye hata leo japo hana jinsi. Au watu mmesahau kiapo cha Sumaye kuwa kama CCM ingemteua Lowassa kugombea urais yeye angehama CCM na kuingia upinzani? Hamshangai ni kitu gani tena kimfanye amfuate Lowassa huku alikokwenda kuteuliwa kugombea urais? In short, ili mradi Lowassa anamiliki CHADEMA kama chama alichokinunua kwa pesa nyingi kamwe Sumaye hawezi kuwa katibu mkuu wa CHADEMA

Hizi ni habari za uhakika kabisa... Na hauto fanyika uchaguzi bali atapewa hicho kiti kwakuwa ni mtu wa Mgombea Urais..
Hili ni deni lingine ambalo chadema wanamlipa Lowasa..
 
Mkuu hivi mpaka leo bado unaacha akili zako kwenye vmakabati ya Nepi pale Lumumba?

Jitahidi uwe unatoroka mara mojamoja utaendelea kuwa kituko mpaka lini? Siamini kama hujui utaratibu wa upatikanaji wa Katibu mkuu ndani ya Chadema.... Siamini.

Hivi umemwona Laki si pesa wa leo? Wewe unasubiri nini? Jiongeze.

BACK TANGANYIKA
huyu rutta kuna kitu kinamwasha sana achana naye huyu ni kama lukos
 
Back
Top Bottom