Sumaye awekeza Shilingi Milioni 931 Benki ya CRDB

Sumaye awekeza Shilingi Milioni 931 Benki ya CRDB

Tembea kaka hiyo Pesa ndogo sana,kwa waziri mkuu,igeuze kwa dola uone,Hata Mboe anae miliki Danguro ni pato lake la miezi 5 tu.
 
Tumbiri kwa Tanzania ya sasa huyo anaonekana ana hela za kawaida no wonder watu wanakushangaa maana siku izi ni mwendo wa Trillions of money.
 
TUMBIRI, mkuu nimefurahi kuona kwamba we ni alma mater mwenzangu pale Mzumbe. Ila tunatofautina kidogo mimi nilisoma PCBaba, naona wewe ulichukua PCMama. Nakutakia mema kwenye PhD yako umalize vyema ukaitumikie nchi yako kwa uadilifu na Wazumbe wote wajulikane kwa hilo.
 
Last edited by a moderator:
Heshima mbele wana JF wote,
Ni muda mrefu sana nimekua sipatikani hapa JF. Baadhi yetu wamekuwa mkini PM na kuniuliza Vipi TUMBIRI? Umeng'olewa meno na kucha au?

Kimsingi nimebanwa na shule Wakuu. Lakini leo wakati napita pita huku na huku kutafuta literature za kusapoti Dissertation yangu nimegundua kitu kimoja.

Waziri Mkuu Mstaafu Mh. Frederick T. Sumaye anamiliki idadi ya hisa 6,206,980[SUP]1 [/SUP]za Benki ya CRDB ambazo kwa mujibu wa Ripoti ya Mwaka ya Benki hiyo, bei ya hisa moja kwa Soko la hisa hadi kufikia tarehe 31 Disemba 2012 ilikuwa ni Sh.150 kwa hisa. Kwa maana hiyo Mh. Sumaye anamiliki hisa zenye thamani ya Shilingi 931,047,000/=.

Hata hivyo kwa mujibu wa tovuti ya soko la hisa leo tarehe 07/06/2013 saa 20:50 hisa moja ya CRDB ina thamani ya Sh.205. Kwa maana hiyo Mh. Sumaye kwa sasa anamiliki hisa zenye thamani ya Sh.1,272,430,900/=.

Haijaelezwa na ripoti ya Benki ni lini Mh. Sumaye alinunua hisa hizo na kwa bei gani.

Uwekezaji wa kiasi hiki cha fedha ni kikubwa hasa ikizingatiwa Mmiliki ni aliyewai kuwa Mtendaji Mkuu wa Serikali ndani ya Serikali iliyopita.

Hii ni taarifa tu.

TUMBIRI (PhD Candidate, CPA(T), MBA(UDSM), Bcom(Accounting), PCM(Mzumbe High School).
tumbiri@jamiiforums.com,
Upanga, Dar es Salaam, Tanzania.

[SUP]1 [/SUP]CRDB Bank Annual Report 2012 (Page 66).


Nakala: Kimbunga, Mingoi, Ndallo, Matola, Crashwise, Mzee Mwanakijiji, Malaria Sugu, chama, mandingo6262, Rejao, Mungi, Putin, Salary Slip, etc

Je kiongozi lazima awe masikini? Sifa za elimu ulizozitoa hapo ni kubwa kuja na hoja ya kitoto kama hii. Just a ---- thread with an envy eyes! Did you ask kama hamekiuka maadili katika kuzipata kwake? Je wakati ananunua hisa moja ilikuwa shiling ngapi? huyo mzee amefanya kazi miaka mingapi na amepata mapato kiasi gani? je tume ya maadili wameleta nongwa? Let us work hard guys otherwise we will not be able to take this country to prosperity!
 
Muwe mnaona hata Aibu ....mmezidi kufuata Sumaye...wakati ukweli hakuna mtu muwazi Kama yeye ....kuna ajabu gani mtu ambayo amekuwa Waziri mkuu kwa miaka kumi ...kumiliki Hisa ???za Bilioni ???? Inawezekana kanunia kwenye IPO kwa milioni 400 ..hakuna ajabu hapo ...mbona wengine wana Bilioni 50 za Libya?

Brother ni wewe?
 
Mkuu kwa ninavyofahamu mimi data za research zinapaswa kutumika kwa ajili ya research, when you disclose other people information unakuwa unakosea. That is not academics mkuu. Hayo ungeweka kwenye research paper yako baada ya kufanya utafiti kwa undani. Japokuwa na-appreciate pia kwamba inaweza ukawa umefanya kwa nia njema jaribu pia kuliangalia hilo. By the way kwa mtu mwenye akili akipata pesa alizokua anapata sumaye kwenye career yake yote ku-raise pesa hizo sio jambo la ajabu.
 
Hicho ni kiasi kidogo sana cha hela. mshahara plus marup rup ya waziri mkuu bila masurufu kwa miaka miwili ni zaidi ya hicho kiasi. Mkuu umekurupukaa!
Karibu tena mkuu.

Nilidhani uko Mbeya unawafundisha vijana wenu kwa maagizo ya Mwigulu.

Hizo pesa ni kiodogo kulinganisha na nini na za nani?
 
Kama hivyo ndivyo hakika haqa viongozi wastaafu wanatufanya vibaya. Hata waliojiuzulu bado is wanalipwa jamani?


Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
Na hapo ni CRDB tu bado kwingine,pia hizo ni hisa tu baada biashara nyingi,na wanaosma marupurupu wasiwe wavivu wa kufikiri marupurupu hayo ni kiasi gani?Sophia Simba alisema hakuna msafi CCM,sasa kama huyo ni Sumaye ,je Mzee aliyehamia Kifungilo ana kiasi gani?je akina Mramba,yona,Mamvi wana kiasi gani?ndio maana Chenge alisema ana vijisenti tu.Tutaendelea kurumbana na kutoa mapovu kwenye JF wakati ''wakali wenyewe'' wanakula bata.
 
Mkuu Profesa,
Nakuheshimu sana Profesa wangu. Kwanza kwa jina lako na maono yako humu jamvini lakini kwa hili naona umepotoka kidogo Mkuu wangu. Annual Report za Public Listed Company ni Public Reports. Sheria ya Makambuni pamoja na Kanuni za uendeshaji wa Stock Exchange zinaagiza Annual Reports of every listed company must be published contained Chairman Statement, Directors Report, Auditor Report, Financial Statement, etc.

Sasa mimi nimedisclose kitu ambacho tayari kipo mitaani na kinapaswa kijulikane kisheria. After all Mh. Sumaye namuheshimu sana sina personal ugomvi nae kama unavyotaka kuaminisha jukwaa kwamba nina introduce personal attack. Hata wewe ukitaka hiyo ripoti just google ipo na free of charge.

Regard,
TUMBIRI.
TUMBIRI sina tatizo na taarifa zenyewe, na unalosema ni kweli ila hapa palinitatiza kidogo "...Uwekezaji wa kiasi hiki cha fedha ni kikubwa hasa ikizingatiwa Mmiliki ni aliyewai kuwa Mtendaji Mkuu wa Serikali ndani ya Serikali iliyopita..." Maana kama hutupi more evidence juthibitisha hili mfano mshahara wake kwa mwezi, marupurupu ya safari na ya uongozi n.k. na ukizingatia kwa miaka yote tangu akiwa Waziri mheshimiwa huyu alikuwa na interest sana na ardhi na kilimo na uwekezaji wowote halali/usio halali alioufanya na ni wa thamani gani basi hapo tunaweza kujadili kiasi hii kina maana gani? Bahati mbaya au nzuri viongozi hawa wanachofanya ni kutumia mwanya wa taarifa walizonazo kuhusu opportunity za nchi hii, upatikanaji wa mikopo, ardhi, mitaji ambayo wengi wetu huwa taarifa hizi tunazipata kwa shida kidogo haziko tu avaiable mpaka uwe na skills na uwe umekuwa exposed jinsi ya kuzipata. Ukiachilia mbali zinazotolewa na mabenki ya kibiashara ambazo nyingi ni viini macho kwa mtu wa kawaida. So ninaafikiana na wewe ni idadi ya pesa ya kushtua kidogo, ila tunahitaji evidence zaidi kabla ya kumrukia shingoni
 
Mkuu Profesa,
Nakuheshimu sana Profesa wangu. Kwanza kwa jina lako na maono yako humu jamvini lakini kwa hili naona umepotoka kidogo Mkuu wangu. Annual Report za Public Listed Company ni Public Reports. Sheria ya Makambuni pamoja na Kanuni za uendeshaji wa Stock Exchange zinaagiza Annual Reports of every listed company must be published contained Chairman Statement, Directors Report, Auditor Report, Financial Statement, etc.

Sasa mimi nimedisclose kitu ambacho tayari kipo mitaani na kinapaswa kijulikane kisheria. After all Mh. Sumaye namuheshimu sana sina personal ugomvi nae kama unavyotaka kuaminisha jukwaa kwamba nina introduce personal attack. Hata wewe ukitaka hiyo ripoti just google ipo na free of charge.

Regard,
TUMBIRI.
TUMBIRI sina tatizo na taarifa zenyewe, na unalosema ni kweli ila hapa palinitatiza kidogo "...Uwekezaji wa kiasi hiki cha fedha ni kikubwa hasa ikizingatiwa Mmiliki ni aliyewai kuwa Mtendaji Mkuu wa Serikali ndani ya Serikali iliyopita..." Maana kama hutupi more evidence kuthibitisha hili mfano mshahara wake kwa mwezi, marupurupu ya safari na ya uongozi n.k. na ukizingatia kwa miaka yote tangu akiwa Waziri mheshimiwa huyu alikuwa na interest sana na ardhi na kilimo na uwekezaji wowote halali/usio halali alioufanya na ni wa thamani gani basi hapo tunaweza kujadili kiasi hii kina maana gani? Bahati mbaya au nzuri viongozi hawa wanachofanya ni kutumia mwanya wa taarifa walizonazo kuhusu opportunity za nchi hii, upatikanaji wa mikopo, ardhi, mitaji ambayo wengi wetu huwa taarifa hizi tunazipata kwa shida kidogo haziko tu avaiable mpaka uwe na skills na uwe umekuwa exposed jinsi ya kuzipata (Kutokana na kutokuwajibika na kukosa uzalendo kwa tuliowaeka madarakani bila shaka). Ukiachilia mbali zinazotolewa na mabenki ya kibiashara ambazo nyingi ni viini macho kwa mtu wa kawaida. So ninaafikiana na wewe ni idadi ya pesa ya kushtua kidogo, ila tunahitaji evidence zaidi kabla ya kumrukia shingoni
 
Kwa huyo wa mikoa ya kule juu Kaskazini lazima Philemon Michael atetee
 
Tanzania: Taifa ambalo linachukia watu wakiwa na hali nzuri. Ila wanaenzi maskini... Sasa angalia hela ndogo kama hiyo... Tunaambiwa ati tatizo.
 
Tanzania ndio maana kamanda wa polisi akiua anapandishwa cheo.

Mtumishi wa serikali akifisadi anahamishwa kituo cha kazi.

Mkuu TUMBIRI watanzania sasa hivi akili za kuhoji ufisadi zimedumazwa na mabilioni yalioko uswiss, bila kusahau tirioni za Shimbo hivyo unavyotoa taarifa kuhusu kabilioni kamoja lazima wakushangae.!!
 
Last edited by a moderator:
Hicho ni kiasi kidogo sana
cha hela. mshahara plus marup rup ya waziri mkuu bila masurufu kwa miaka
miwili ni zaidi ya hicho kiasi. Mkuu umekurupukaa!

Mbona pinda alisema ana 25mil tu, je yeye hayo marupurupu hayapati...
 
Mkuu kwa ninavyofahamu mimi data za research zinapaswa kutumika kwa ajili ya research, when you disclose other people information unakuwa unakosea. That is not academics mkuu. Hayo ungeweka kwenye research paper yako baada ya kufanya utafiti kwa undani. Japokuwa na-appreciate pia kwamba inaweza ukawa umefanya kwa nia njema jaribu pia kuliangalia hilo. By the way kwa mtu mwenye akili akipata pesa alizokua anapata sumaye kwenye career yake yote ku-raise pesa hizo sio jambo la ajabu.

Mkuu sijaona kosa la Tumbiri kwenye hili. Actually information aliyoitoa sio siri unless tuwe wavivu tu wa kusoma. Suala la hisa si siri ni ndio maana CRDB baada ya kuanza kuuza hisa kibwagizo cha PLC kiliongezwa kwenye name yao kikimaanisha Public Limited Company. So umiliki wa hisa ni kwa ajili ya public consumption, nani ana hisa ngapi kwenye PLC si confidential mkuu.
 
Sumaye aliwahi kusema anamiliki tractor mbili na moja ilikuwa bovu na kapickup kamoja. naona ameuza mahindi kwenye soko la kibaigwa mpaka akamiliki hisa za CRDB. Afadhali yeye hatuna evidensi amekwapua sehemu. shida ni kwa hawa wakina prince
 
sio kila kitu ni wizi kuna watu wanapenda kuwekeza katika hisa kwa hiyo amejipangia kila mwezi atanunua hisa kiasi fulani kwa hiyo baada ya muda ni lazima atakuwa nazo nyingi na thamani inapanda kwa hiyo naamini inawezekana hata kwa mtanzania wa kawaida tu....
 
Back
Top Bottom