Earth on heaven
Member
- Jun 7, 2013
- 82
- 34
Heshima mbele wana JF wote,
Ni muda mrefu sana nimekua sipatikani hapa JF. Baadhi yetu wamekuwa mkini PM na kuniuliza Vipi TUMBIRI? Umeng'olewa meno na kucha au?
Kimsingi nimebanwa na shule Wakuu. Lakini leo wakati napita pita huku na huku kutafuta literature za kusapoti Dissertation yangu nimegundua kitu kimoja.
Waziri Mkuu Mstaafu Mh. Frederick T. Sumaye anamiliki idadi ya hisa 6,206,980[SUP]1 [/SUP]za Benki ya CRDB ambazo kwa mujibu wa Ripoti ya Mwaka ya Benki hiyo, bei ya hisa moja kwa Soko la hisa hadi kufikia tarehe 31 Disemba 2012 ilikuwa ni Sh.150 kwa hisa. Kwa maana hiyo Mh. Sumaye anamiliki hisa zenye thamani ya Shilingi 931,047,000/=.
Hata hivyo kwa mujibu wa tovuti ya soko la hisa leo tarehe 07/06/2013 saa 20:50 hisa moja ya CRDB ina thamani ya Sh.205. Kwa maana hiyo Mh. Sumaye kwa sasa anamiliki hisa zenye thamani ya Sh.1,272,430,900/=.
Haijaelezwa na ripoti ya Benki ni lini Mh. Sumaye alinunua hisa hizo na kwa bei gani.
Uwekezaji wa kiasi hiki cha fedha ni kikubwa hasa ikizingatiwa Mmiliki ni aliyewai kuwa Mtendaji Mkuu wa Serikali ndani ya Serikali iliyopita.
Hii ni taarifa tu.
TUMBIRI (PhD Candidate, CPA(T), MBA(UDSM), Bcom(Accounting), PCM(Mzumbe High School).
tumbiri@jamiiforums.com,
Upanga, Dar es Salaam, Tanzania.
[SUP]1 [/SUP]CRDB Bank Annual Report 2012 (Page 66).
Nakala: Kimbunga, Mingoi, Ndallo, Matola, Crashwise, Mzee Mwanakijiji, Malaria Sugu, chama, mandingo6262, Rejao, Mungi, Putin, Salary Slip, etc
Sasa tufanyeje TUMBIRI?