Sumaye awekeza Shilingi Milioni 931 Benki ya CRDB

Sumaye awekeza Shilingi Milioni 931 Benki ya CRDB

TUMBIRI

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2011
Posts
1,933
Reaction score
1,203
Heshima mbele wana JF wote,
Ni muda mrefu sana nimekua sipatikani hapa JF. Baadhi yetu wamekuwa mkini PM na kuniuliza Vipi TUMBIRI? Umeng'olewa meno na kucha au?

Kimsingi nimebanwa na shule Wakuu. Lakini leo wakati napita pita huku na huku kutafuta literature za kusapoti Dissertation yangu nimegundua kitu kimoja.

Waziri Mkuu Mstaafu Mh. Frederick T. Sumaye anamiliki idadi ya hisa 6,206,980[SUP]1 [/SUP]za Benki ya CRDB ambazo kwa mujibu wa Ripoti ya Mwaka ya Benki hiyo, bei ya hisa moja kwa Soko la hisa hadi kufikia tarehe 31 Disemba 2012 ilikuwa ni Sh.150 kwa hisa. Kwa maana hiyo Mh. Sumaye anamiliki hisa zenye thamani ya Shilingi 931,047,000/=.

Hata hivyo kwa mujibu wa tovuti ya soko la hisa leo tarehe 07/06/2013 saa 20:50 hisa moja ya CRDB ina thamani ya Sh.205. Kwa maana hiyo Mh. Sumaye kwa sasa anamiliki hisa zenye thamani ya Sh.1,272,430,900/=.

Haijaelezwa na ripoti ya Benki ni lini Mh. Sumaye alinunua hisa hizo na kwa bei gani.

Uwekezaji wa kiasi hiki cha fedha ni kikubwa hasa ikizingatiwa Mmiliki ni aliyewai kuwa Mtendaji Mkuu wa Serikali ndani ya Serikali iliyopita.

Hii ni taarifa tu.

TUMBIRI (PhD Candidate, CPA(T), MBA(UDSM), Bcom(Accounting), PCM(Mzumbe High School).
tumbiri@jamiiforums.com,
Upanga, Dar es Salaam, Tanzania.

[SUP]1 [/SUP]CRDB Bank Annual Report 2012 (Page 66).

Nakala: Kimbunga, Mingoi, Ndallo, Matola, Crashwise, Mzee Mwanakijiji, Malaria Sugu, chama, mandingo6262, Rejao, Mungi, Putin, Salary Slip, etc
 
Hicho ni kiasi kidogo sana cha hela. mshahara plus marup rup ya waziri mkuu bila masurufu kwa miaka miwili ni zaidi ya hicho kiasi. Mkuu umekurupukaa!
Kama hivyo ndivyo hakika haqa viongozi wastaafu wanatufanya vibaya. Hata waliojiuzulu bado is wanalipwa jamani?

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Wakati wameteuliwa kuwa PM alitangaza mali zake, ambapo ali declare kuwa ana hisa sh mil. 50.
Hivyo si vibaya kwa sasa kama anahicho kiwango

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Muwe mnaona hata Aibu ....mmezidi kufuata Sumaye...wakati ukweli hakuna mtu muwazi Kama yeye ....kuna ajabu gani mtu ambayo amekuwa Waziri mkuu kwa miaka kumi ...kumiliki Hisa ???za Bilioni ???? Inawezekana kanunia kwenye IPO kwa milioni 400 ..hakuna ajabu hapo ...mbona wengine wana Bilioni 50 za Libya?
 
Kwa cheo chake alichokuwa nacho nadhanisi shida, kabilioni ka moja!
 
Baba lao ni Mungai mkuu,kaulizie DSE ukiondoa wahindi,pension funds, Mungai hufuata kwa hisa.Karibu makampuni makubwa kama TBL,TPCC,TCC,DCB yalisajiliwa
 
kawaida mkuu kwa mtu kama sumaye jamaa ana hela nyingi sana hicho cha mtoto sumaye anamiliki ardhi kubwa sana huko pwani karibu na kiluvya madukani ana ardhi kubwa sana na ngombe wengi sana wa maziwa pia anamiliki hoteli ya ngurdoto pale arusha.
 
Umekurupuka sana mbona kawaida sana wala siyo issue.

Kuna siku akili inakurudia kidogo cha kawaida.....naona umekubali hivyo vijisenti,wengine(obviously magamba) wana nyingi zaidi.
 
Hicho ni kiasi kidogo sana cha hela. mshahara plus marup rup ya waziri mkuu bila masurufu kwa miaka miwili ni zaidi ya hicho kiasi. Mkuu umekurupukaa!
Duh! Kweli una maisha marefu! Yaani jana usiku nilikuota kua ............ halafu leo nimekuona!!!! Mungu ni Mnene!
 
Hivi mnaotetea ina maana yeye hana matumizi?

Mbona huwa wanatangaza mali zao wanapoingia madarakani ila inakuwaje wanashindwa kufanya hivyo wanapoondoka madarakani?!

Mnachotakiwa kujiuliza ni kuwa hata kama ni biashara huo mtaji mkubwa viongozi huwa wanaupata kwa njia halali?

Hata ukiwa na biashara halali ila kama mtaji wako ulitokana na hela chafu bado huna justification.

Hivi kiongozi si anaweza kuchukua mkopo wa mamilioni kama ushahidi tu wakati hela ya kulipa teyari anayo na hakuna anaejua hiyo hela kaipata vipi?

Basi hata kumlaumu Chenge kumiliki bilioni moja na zaidi ilikuwa si sahihi kwani nae alikuwa kiongozi mwandamizi serikalini.
 
Muwe mnaona hata Aibu ....mmezidi kufuata Sumaye...wakati ukweli hakuna mtu muwazi Kama yeye ....kuna ajabu gani mtu ambayo amekuwa Waziri mkuu kwa miaka kumi ...kumiliki Hisa ???za Bilioni ???? Inawezekana kanunia kwenye IPO kwa milioni 400 ..hakuna ajabu hapo ...mbona wengine wana Bilioni 50 za Libya?
Kamanda,

Umesababisha niingie hapa. Sidhani Tumbiri anafanya hivi kwa nia mbaya. Kwa 'sisi' tunaofahamu njia 'halali' alizopitia hadi kuwekeza tunaweza kumtoa fongotongo.

Hold on, umeanza lini kuuma maneno? Unashindwa kumtaja Membe? Anang'oa meno pia?
 
Heshima mbele wana JF wote,
Ni muda mrefu sana nimekua sipatikani hapa JF. Baadhi yetu wamekuwa mkini PM na kuniuliza Vipi TUMBIRI? Umeng'olewa meno na kucha au?

Kimsingi nimebanwa na shule Wakuu. Lakini leo wakati napita pita huku na huku kutafuta literature za kusapoti Dissertation yangu nimegundua kitu kimoja.

Waziri Mkuu Mstaafu Mh. Frederick T. Sumaye anamiliki idadi ya hisa 6,206,980[SUP]1 [/SUP]za Benki ya CRDB ambazo kwa mujibu wa Ripoti ya Mwaka ya Benki hiyo, bei ya hisa moja kwa Soko la hisa hadi kufikia tarehe 31 Disemba 2012 ilikuwa ni Sh.150 kwa hisa. Kwa maana hiyo Mh. Sumaye anamiliki hisa zenye thamani ya Shilingi 931,047,000/=.

Hata hivyo kwa mujibu wa tovuti ya soko la hisa leo tarehe 07/06/2013 saa 20:50 hisa moja ya CRDB ina thamani ya Sh.205. Kwa maana hiyo Mh. Sumaye kwa sasa anamiliki hisa zenye thamani ya Sh.1,272,430,900/=.

Haijaelezwa na ripoti ya Benki ni lini Mh. Sumaye alinunua hisa hizo na kwa bei gani.

Uwekezaji wa kiasi hiki cha fedha ni kikubwa hasa ikizingatiwa Mmiliki ni aliyewai kuwa Mtendaji Mkuu wa Serikali ndani ya Serikali iliyopita.

Hii ni taarifa tu.

TUMBIRI (PhD Candidate, CPA(T), MBA(UDSM), Bcom(Accounting), PCM(Mzumbe High School).
tumbiri@jamiiforums.com,
Upanga, Dar es Salaam, Tanzania.

[SUP]1 [/SUP]CRDB Bank Annual Report 2012 (Page 66).

Nakala: Kimbunga, Mingoi, Ndallo, Matola, Crashwise, Mzee Mwanakijiji, Malaria Sugu, chama, mandingo6262, Rejao, Mungi, Putin, Salary Slip, etc
Katika mambo yooote mazuri aliyoyafanya baba, moja kubwa baya ninaloamini ametuachia ni kuamini kuwa utajiri ni dhambi! Kuingizwa kwa misamiati kama ufisadi ambayo maana yake ya moja kwamoja haipo bali huhusianishwa na mtu yeyote ambaye kipato chake tunakitilia mashaka.

Uchumi wa nchi unaweza kujengwa na pesa zinazovuja kwenye systems mbalimbali, iwapo pesa hizo zitawekewa nchini na sera zikaruhusu watu wengi kunufaika na miradi au uwekezaji unaotokana na pesa hizo. Uchumi wa nchi kama Syprus na Switzeland umejengwa kwa misingi ya kuvutia uwekezaji katika mabenki, kulinda usiri wa wawekezaji na kuhakiksiha usalama wa pesa zinazowekwa. Hili limepelekea Serikali kuwa na capital kubwa na hata mabenki kuwa na uwezo wakufanya biashara kubwa kubwa kutokana na capitle kubwa walizonazo. Tuzibe mianya ya wizi, lakini tuvutie pesa ambazo hatuna ushahidi nazo wa mojakwamoja (na kuacha majungu kama hatuna ushahidi) zibaki nchini na kusaidia kukuza uchumi wa nchi.

Kwa upande mwingine niseme wewe kama candidate we PHD ume-act in a very unethical manner ku-disclose information that was meant to inform your research but you are using it without enough evidence, to try to misinform public and act against someone for the purpose obvious to potray negative image, using the information trusted by the source which is likely to be private. Please present much hard evidence to argue your case otherwise this is much vague and your intentions are very personal and lack clear purpose.
 
Back
Top Bottom