Sumaye awekeza Shilingi Milioni 931 Benki ya CRDB

Sumaye awekeza Shilingi Milioni 931 Benki ya CRDB

Heshima mbele wana JF wote,
Ni muda mrefu sana nimekua sipatikani hapa JF. Baadhi yetu wamekuwa mkini PM na kuniuliza Vipi TUMBIRI? Umeng'olewa meno na kucha au?

Kimsingi nimebanwa na shule Wakuu. Lakini leo wakati napita pita huku na huku kutafuta literature za kusapoti Dissertation yangu nimegundua kitu kimoja.

Waziri Mkuu Mstaafu Mh. Frederick T. Sumaye anamiliki idadi ya hisa 6,206,980[SUP]1 [/SUP]za Benki ya CRDB ambazo kwa mujibu wa Ripoti ya Mwaka ya Benki hiyo, bei ya hisa moja kwa Soko la hisa hadi kufikia tarehe 31 Disemba 2012 ilikuwa ni Sh.150 kwa hisa. Kwa maana hiyo Mh. Sumaye anamiliki hisa zenye thamani ya Shilingi 931,047,000/=.

Hata hivyo kwa mujibu wa tovuti ya soko la hisa leo tarehe 07/06/2013 saa 20:50 hisa moja ya CRDB ina thamani ya Sh.205. Kwa maana hiyo Mh. Sumaye kwa sasa anamiliki hisa zenye thamani ya Sh.1,272,430,900/=.

Haijaelezwa na ripoti ya Benki ni lini Mh. Sumaye alinunua hisa hizo na kwa bei gani.

Uwekezaji wa kiasi hiki cha fedha ni kikubwa hasa ikizingatiwa Mmiliki ni aliyewai kuwa Mtendaji Mkuu wa Serikali ndani ya Serikali iliyopita.

Hii ni taarifa tu.

TUMBIRI (PhD Candidate, CPA(T), MBA(UDSM), Bcom(Accounting), PCM(Mzumbe High School).
tumbiri@jamiiforums.com,
Upanga, Dar es Salaam, Tanzania.

[SUP]1 [/SUP]CRDB Bank Annual Report 2012 (Page 66).

Nakala: Kimbunga, Mingoi, Ndallo, Matola, Crashwise, Mzee Mwanakijiji, Malaria Sugu, chama, mandingo6262, Rejao, Mungi, Putin, Salary Slip, etc

acha utani wewe milin 900 sio pesa ya kukustua kwa mtu aliyewahi kuwa waziri mkuu,unajua kiinua mgongo cha pm ni kiasi gani,tatizo uzembe kufanya kazi unakuaminisha kuwa hizo ni pess mingi,hata machinga kariakoo kibao wanazo
 
Cha kufurahisha hapa Hadi wale CDM wanamtetea Sumaye....wala haitwi GAMBA
Ok...nimeelewa ....mwana Kaskazani Mwenzetu
 
Naona Tumbiri kashambuliwa sana na wa wadau, lakini sidhani kama kama kuna ubaya kutaja mwanahisa wa CRDB aliaayeamua kuwekeza kiasi kikubwa hivyo hata kama kazitoa kwenye mifuko ya jamii kwa kukopa kama PM na kisha miufuko hiyo ikaamua kulalamikia mamlka za serikali na kisha mamlaka husika kama serikali zikazuia fao la kujitoa kwa wananchi wasiojua kwa nini pesa yao haipo tena katika mifuko walikoziweka...Tafakarini kabla ya kukubali kuwa kiongozi akimaliza muda wake wa uongozi basi anayohaki ya kuwa na mabilioni, shule za akina Bayi, n.k!
 
Je hii ni spying? Hii ndo mana waajiri wengi hawaruhusu watafiti katika taasisi zao sababu ya kutoa taarifa ambazo siyo zilizokupeleka pale.

Nacho jua katika dissertation lazima diclare kutunza siri za sehemu unayofanyia utafiti (diclare confidentiality to materials or organization information) kwa kuwa wewe si msemaji wa taasisi hiyo.

Je huoni kuwa umevunja taratibu hivyo kuwapa wakati mgumu watu wengine katika tafiti zao katika kupata information kwa waajiri?
 
Hz hela zinatusaidia sana tunakopa tunazungushia tunalewea na tunalipwa mishahara acheni fitna jama!
 
Aww wabongo tumezidi sasa akiweka uswisi wameficha hela kaweka crdb Hapa unasema ni nyingi sana hivi kuwa go sahihi ni kipi we ni msomi fanya research mungai ana share kiasi gani kwenye makampuni hiyo ni hela ndogo kwa waziri mkuu mstaafu ukumbuke inawezekana alinunua kabla hazijaenda sokoni
 
Kwa upande mwingine niseme wewe kama candidate we PHD ume-act in a very unethical manner ku-disclose information that was meant to inform your research but you are using it without enough evidence, to try to misinform public and act against someone for the purpose obvious to potray negative image, using the information trusted by the source which is likely to be private. Please present much hard evidence to argue your case otherwise this is much vague and your intentions are very personal and lack clear purpose.

Mkuu Profesa,
Nakuheshimu sana Profesa wangu. Kwanza kwa jina lako na maono yako humu jamvini lakini kwa hili naona umepotoka kidogo Mkuu wangu. Annual Report za Public Listed Company ni Public Reports. Sheria ya Makambuni pamoja na Kanuni za uendeshaji wa Stock Exchange zinaagiza Annual Reports of every listed company must be published contained Chairman Statement, Directors Report, Auditor Report, Financial Statement, etc.

Sasa mimi nimedisclose kitu ambacho tayari kipo mitaani na kinapaswa kijulikane kisheria. After all Mh. Sumaye namuheshimu sana sina personal ugomvi nae kama unavyotaka kuaminisha jukwaa kwamba nina introduce personal attack. Hata wewe ukitaka hiyo ripoti just google ipo na free of charge.

Regard,
TUMBIRI.
 
Last edited by a moderator:
Muwe mnaona hata Aibu. Mmezidi kufuata Sumaye wakati ukweli hakuna mtu muwazi Kama yeye kuna ajabu gani mtu ambayo amekuwa Waziri mkuu kwa miaka kumi kumiliki Hisa??? Za Bilioni???? Inawezekana kanunia kwenye IPO kwa milioni 400 hakuna ajabu hapo mbona wengine wana Bilioni 50 za Libya?

Mkuu hatumfuati fuati Sumaye. Yeye ni Public figure. Amewai kushika Ofisi yetu kubwa Serikalini kwa hiyo lolote linalomuhusu linatuhusu pia. Kama hutaki tusimwandikie humu ungemshauri asingegombea Ubunge na kuwa Waziri Mkuu. As long as amewai kuwa Mbunge na Waziri Mkuu wetu basi utarajie tu akiumwa ataandikwa, akiiba ataandikwa, akifa ataandikwa, akitelekeza familia ataandikwa vilevile. Si kwa sababu tunamchukia bali ni kwa sababu ni mtu amewai kutuongoza.
 
Nacho jua katika dissertation lazima diclare kutunza siri za sehemu unayofanyia utafiti (diclare confidentiality to materials or organization information) kwa kuwa wewe si msemaji wa taasisi hiyo.

Je huoni kuwa umevunja taratibu hivyo kuwapa wakati mgumu watu wengine katika tafiti zao katika kupata information kwa waajiri?

Mkuu Magu,
Jua tu kwamba Sifanyi Dissertation yangu CRDB. Data nilizotua ni Public data. Nimezitoa kwenye Annual Report ambazo hata Mtanzania anaeishi kule KAMACHUMU BUKOBA au kule NAMANYERE NKASI ana-access kulingana na Sheria ya Makampuni concerning Public Listed Companies. Just google CRDB Annual Report 2012 utaiona hiyo ripoti.

Hapa sijavunja taratibu za utafiti.

Nakala: Profesa, etc.
 
Last edited by a moderator:
Inategemea alianzaje na kama shares zimekua... Unaa bila analysis ni sawa na ushirikina
 
Mkuu Profesa,
Nakuheshimu sana Profesa wangu. Kwanza kwa jina lako na maono yako humu jamvini lakini kwa hili naona umepotoka kidogo Mkuu wangu. Annual Report za Public Listed Company ni Public Reports. Sheria ya Makambuni pamoja na Kanuni za uendeshaji wa Stock Exchange zinaagiza Annual Reports of every listed company must be published contained Chairman Statement, Directors Report, Auditor Report, Financial Statement, etc.

Sasa mimi nimedisclose kitu ambacho tayari kipo mitaani na kinapaswa kijulikane kisheria. After all Mh. Sumaye namuheshimu sana sina personal ugomvi nae kama unavyotaka kuaminisha jukwaa kwamba nina introduce personal attack.

Regard,
TUMBIRI.

Mkuu Tumbiri nadhani ungejishughulisha kidogo ungepata ukweli wa namna mh. Sumaye alivyopata hizopesa. Mwaka 2005 CRDB walitangaza kuuza hisa, na hisa mojailikuwa Tsh. 70. watu wengi wenye pesa zao wakati huo walinunua hisa CRDB mmoja wapoalikuwa Sumaye.

Sasa kama alinunua wakati ule kwa Tsh. 70, ingekuwa vema kuhoji kiasi kile alichonunulia hizo hisa wakati ule na si hiki kiasi ulichoandika hapa.
 
Mkuu kwenye andiko langu nime-declare ripoti niliyoinukuu haijasema hizo hisa alinunua lini na kwa Shilingi ngapi? Mbona hamtaki kunielewa? Sina chuki na Mh. Sumaye. Tofauti yangu na yeye ni itikadi tu. Namtakia kila heri kwenye mbio zake za Urais iwe Urais wa Tanganyika au Muungano lakini ninachomwambia ni kwamba atashindwa!
 
Ndiyo maana nimekushauri uchimbe tena kidogo ili upate taarifa kamili namna hiyo pesa ilivyoongezeka hadi kufikia hicho kiasi maana ni miaka nane sasa tangu huyu mh. anunue hizo hisa. kumbuka pia kwamba kila mwaka kuna faida na ongezeko la idadi la hisa pia iwapo mh. hafanyi withdraw ya faida.
 
Kwa baadhi ya watanzania kuwa tajiri ni dhambi kwa maana wameaminishwa na wanasiasa na wakaamini utajiri ni WIZI.

Bandiko lako umelileta likiwa limebeba mantiki iliyojificha kana kwamba alichokifanya Mh. Frederick T. Sumaye ni dhambi.

Kwa mtu uliyewahi kutoa matongo tongo nje ya nchi, ni kama unashangaza vile kwa kuwa na mshangao kuhusiana na hisa za Mh. Frederick T. Sumaye kulingana na thamani ya "madafu" ya Tanzania.

Ukiwa kama msomi, ulipaswa uweke uchambuzi hapa ili watu wafahamu ni muda gani alizinunua na kwa kiasi gani katika mazingira yapi. Kipato chake kikoje kwa sasa na kilikuwaje wakati ananunua hizo hisa.

Kuleta thamani ya hisa kwa miaka miwili ya nyuma ni kitolitendea haki janvi (JF) na Mh. Frederick T. Sumaye.

Kwani walioko serikalini ni maskini na lazima uwe maskini ukiwa serikalini?.
 
Napita tu, kwan chuon mwalimu aliyekuwa anafundisia financial management nilikua namchukia, so nikiona majadiliano ya hisa dse chuki inarud
 
Waziri Mkuu Mstaafu Mh. Frederick T. Sumaye anamiliki idadi ya hisa 6,206,980[SUP]1 [/SUP]za Benki ya CRDB ambazo kwa mujibu wa Ripoti ya Mwaka ya Benki hiyo, bei ya hisa moja kwa Soko la hisa hadi kufikia tarehe 31 Disemba 2012 ilikuwa ni Sh.150 kwa hisa. Kwa maana hiyo Mh. Sumaye anamiliki hisa zenye thamani ya Shilingi 931,047,000/=.

Hata hivyo kwa mujibu wa tovuti ya soko la hisa leo tarehe 07/06/2013 saa 20:50 hisa moja ya CRDB ina thamani ya Sh.205. Kwa maana hiyo Mh. Sumaye kwa sasa anamiliki hisa zenye thamani ya Sh.1,272,430,900/=.

Haijaelezwa na ripoti ya Benki ni lini Mh. Sumaye alinunua hisa hizo na kwa bei gani.

Uwekezaji wa kiasi hiki cha fedha ni kikubwa hasa ikizingatiwa Mmiliki ni aliyewai kuwa Mtendaji Mkuu wa Serikali ndani ya Serikali iliyopita.

Yeye anapinga mapendekezo ya rasimu ya katiba kuwepo kwa serikali tatu na hoja yake ni gharama, gharama zinakuwa kubwa kwa serikali kwa wenye madaraka kujichotea kama hivi kwa maslahi yao, amekuwa akimnyoshea kidole Loawasa kwa utajiri, ama kweli nyani .........
 
Back
Top Bottom