Suluhisho la maisha ya kuungaunga kwa watumishi wa umma haliko mikononi mwao bali liko mikononi mwa Serikali

Kiboko ya Jiwe

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
12,705
36,154
Salamu tawapa mchana!

Watu wengi wannamini watumishi wanapaswa kujiongeza kwa kufanya shughuli zingine nje ya career yao au nje ya ofisi ndipo wataweza kuishi kwa ustawi. Mtumishi hakupaswa kabisa kujishughulisha na shughuli yoyote nje ya shughuli za serikali anazopangiwa na mwajiri wake.

Mtumishi anapokuwa na shughuli zake binafsi lazima ataiba muda wa serikali ambao ungeleta tija kwa umma.
Watumishi wa umma wasiruhusiwe kujihusisha kwenye shughuli za kibiashara. Hii ingeleta tija kubwa kwa serikali na wananchi wangepata maendeleo kwa haraka.

Leo hii afisa manunuzi anafungua kampuni yake ambayo ina deal na bidhaa za ofisini kwao. Mganga mkuu wa wilaya anafungua duka la dawa nyumbani kwake. Hapa hata kama wewe msomaji ndiye ungekuwa wewe usingeiba dawa na kupeleka dukani kwako? Engineer wa mkoa anafungua kampuni yake ya Kihandisi, unategemea nini? ,kampuni zingine zitapata tenda za Kihandisi na kuiweka yake kando?

Hata mimi najishughulisha na shughuli za uzalishaji nje ya kazi ya kuajiriwa ili nisikwame kiuchumi au nisije nikaishi kwa madeni then niufedheheshe utumishi wa umma na familia yangu. Serikali ilipaswa kugharamia mahitaji muhimu yote kwa watumishi. Kila Mtumishi angekopeshwa nyumba kwa lazima na kwa masharti nafuu pindi anapoanza tu kazi kwenye utumishi wa umma.

Mtumishi angewezeshwa kupata angalau usafiri wa bei nafuu, hili aliweza Hitler licha ya kuwa nchi yake ilikuwa kwenye kipindi kigumu kipindi hicho. Aliweza kukopesha watumishi wote vi tax kobe. Serikali ilipe mshahara unaotosha kwa chakula cha Mtumishi na familia yake kwa mwezi wote. Ni aibu mtumishi wa umma kudaiwa hovyo.

Mtumishi wa umma anadaiwa buku 3, hii ni zaidi ya dhihaka. Mtumishi wa umma anakosa vocha!!!!
Ni heri serikali iwe na watumishi wachache huku ikiwalipa vizuri kuliko kuajiri kwa wingi lakini hali za watumishi hao zikiwa hoi.

MWISHO

Rais Samia ndiye Rais bora kuliko wote waliomtangulia.
 
Kimasilahi kwa watumishi wa umma, Rais bora alikuwa Kikwete. Rais Samia anaweza kuja kuwa bora kama atajua kuwa watumishi wa kima cha chini nao wanatakiwa kupewa allowance ya nyumba na usafiri,akilifanya hilo atakuwa Rais bora kuliko Kikwete.
 
Siku ya kwanza kuajiriwa, jua wewe ni kibarua tu, leo upo kesho haupo, wenye uchungu na wewe ni familia yako. Tumia mshahara wako vizuri kujijenga na kama una fursa za mikopo tumia vizuri, ili siku utakapoambiwa achia ngazi usianze kulaumu.
 
Sio kweli ndugu; kila kitu kinaanzia kwenye fikra.

Ni mtu mmoja mmoja na wala sio kikundi au Serikali itajayobadili maisha, vipato au maendeleo ya mhusika
 
Back
Top Bottom