Kwanini Watumishi wa Umma wana roho mbaya na wanajikatili wenyewe kwa wenyewe?

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
876
4,101
Kikokotoo kimeandaliwa na watumishi wa umma na kinalalamimiwa na watumishi wa umma

Bima ya watoto imeondolewa na watumishi wa umma kisa watoto wao wanatibiwa bure ila wanashindwa kufahamu kuna kufukuzwa kazi.

Mishahara inaandaliwa na watumishi wa umma na siku zote waliopo hazina ukiwasikia wanasisitiza kutopanda kwa mishahara lakini wabunge kila wakijisikia mishahara na posho inapanda tena kwa kuandaliwa na Watumishi wa Umma.

Watumishi wa Umma wanapenda wenzao watimuliwe lakini wanalinda kwa hali na mali wanasiasa wasiondoke madarakani, angalia kazi wanayofanya polisi na TAKUKURU kwa wenzao

Watumishi wa Umma wanatengeneza sheria kandamizi zakuwaadhibu wao lakini wanashiriki kutunga sheria za kuwawekea kinga

Mtumishi wa Umma anatamani rushwa kwa mfanyabiashara wakati huo huo anamtungia mfanyabiashara sheria na kumwekea mazingira magumu ya biashara

Mtumishi wa Umma ni kiumbe pekee ambaye ameenda shule kujifunza namna ya kujiadhibu; lini mtajikwamua?
 
Back
Top Bottom