Sukari imepanda Bei. Hapo ulipo bei ipoje?

Baada ya serikali kupiga marufuku wafanya biashara kupandisha bei ya sukari (4000tsh had 4500tsh), na badala yake bei elekezi ya 2800-3000 ifuatwe;

Mtaani kwetu Ubungo Kisiwani (External)bado bei hazijashuka hadi sasa, naomba kujua ni hatua gan serikali inachukua ili kuhakikisha pale bei elekezi inapotolewa, wafanya biashara waweze kuiadapt kwa wakati??
 
Ninachofahamu mimi ni kuwa wafanya biashara ni rahisi kupandisha bei za bidhaa lakini sio rahisi kushusha. Kibaya zaidi wafanyabiashara ndio hao hao wafanyakazi wa serekalini.
 
Baada ya serikali kupiga marufuku wafanya biashara kupandisha bei ya sukari (4000tsh had 4500tsh), na badala yake bei elekezi ya 2800-3000 ifuatwe;

Mtaani kwetu Ubungo Kisiwani (External)bado bei hazijashuka hadi sasa, naomba kujua ni hatua gan serikali inachukua ili kuhakikisha pale bei elekezi inapotolewa, wafanya biashara waweze kuiadapt kwa wakati??
Jana mimi nimeenda maduka kibao sukari wakawa hawana na nilipoipa kilo 4000
 
Serikali haina Sukari wameachiwa wafanyabiashara wapange bei hata watoe bei elekezi vip haitashuka ...
Wakitaka ishuke siku moja waruhusiwe watu wa mipakani waingize Sukari hata kwa wiki mbili tu hizi sarakasi za Sukari hautaziskia tena na mambo ya vibali vyao vya magumashi kwa kupewa watu wachache...Zambia na Malawi sukari inaoza tu huko na ni hao hao Ilovo ambao wapo Tanzania...
 
Baada ya serikali kupiga marufuku wafanya biashara kupandisha bei ya sukari (4000tsh had 4500tsh), na badala yake bei elekezi ya 2800-3000 ifuatwe;

Mtaani kwetu Ubungo Kisiwani (External)bado bei hazijashuka hadi sasa, naomba kujua ni hatua gan serikali inachukua ili kuhakikisha pale bei elekezi inapotolewa, wafanya biashara waweze kuiadapt kwa wakati??
Nani anajali?, kama kina kipara na yule mchumi wa singida ndo wapiga dili wakubwa usitegemee sukari ishuke
 
Baada ya bod ya sukari kutoa bei elekezi kuwa sukari isizidi shilling 3000 lakini bado mtaani tunanunua sukari shilling 4500 hadi 5000.

Kwa wenzetu waislamu mwezi Ramadhan unaingia hivi karibu sasa kwa huu mfumko wa bei maisha yatakuwaje kwa wenzetu wa imani hiyo

Bodi ya sukari acheni kukaa ofsi ingia mtaani muone bei ya sukari ilivo juu, inaumiza Wananchi

Sasa najiuliza sisi mkoa wa Kagera tupo karibu na mzalishaji wa Sukari ambaye ni Kagera sugar tunanunua sukari bei kubwa sijui kwa Tandahimba huko wana bei gani

Mfumko wa bei uko juu mno sukari, mafuta ya kupikia juu, petrol juu, nauli juu, umeme ni kata washa, maisha yetu ni magumu mno sisi wa kijijini

Serikali hebu amueni kututumika wananchi mzigo ni mkubwa mno
 
sukari siyo kitu cha lazima kiviiiiiile
huku tarime tunagonga uji na togwa bila hiyo kitu. muhimu maziwa na unga
sukari wacha tu ipande
 
Wangepredict kwamba sukari ingepanda then wazuie mfumuko kabla hata haujatokea. Hata kilombero sugar washushe sukari 2000 Kwa kilo haitokaa ishuke Hadi 2500 itaishia kwenye 4000 labda.

Sent from my Infinix X669 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom