Sukari imepanda Bei. Hapo ulipo bei ipoje?

Sukari Bongo wameifanya madawa ya kulevya wanaficha sukari baadae wengine wanapewa vibali magumashi wawaletee Watanzania Sukari kila mwaka hili jambo lazima litokee mwishoni mwa Mwezi wa kumi na mbili au mwezi wa kwanza wacha movie iendelee ndio kwanza tupo episode ya kwanza...
 
Ila nchi za afrika bana,yaani kila duka unakuta kuna sukari inatoka brazil . Sasa najiuliza hivi viwanda vyetu sukari vinaweka wapi baada ya kuzalisha?

Sasa fikiria hata wewe sukari itoke brazil ni kilometer ngapi mpaka hapa? Halafu zingatia na shilingi yetu ilivolegea dhidi ya dollar
inasemekana kiwanda kinachozalisha sukari bagamoyo kiliathiriwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha na kupelekea uhaba uliopo
 
Ramadhani mwezi wa 4 sukari mashamba ya miwa yamejaa maji hawawez kuingia kuvuna si kwa trecta wala mtu so uzalishaji hakuna tena viwandan ndio imesababisha uhaba wa sukar na ndio mabingwa waliokua nayo kwa wingi wanauza wanavotaka
 
Ukiwa mwanakijani unauziwa aftatu. Hiyo bei ni kwa wapinzani wasioitakia mema nchi yetu, kijani sio sukari tu hata asali wanalamba.
Huwa nawasemaga sana wajinga wajinga wanaosemaga wataisoma namba,bila kujua wote tunanunua sukari 5,000
 
Maccm hawajui kwamba kupanda kwa Bei Kuna waathiri chawa wao. Anyway hawajali Sana kwani Kuna Bumunda wataiba kura.
 
Mwanaume hutakiwi kujua bei ya sukari,vitunguu,nyanya,pilipili,unga nk.
Bali inatakiwa ujue bei ya petroli,bia,thamani ya dola na bei ya tiketi za ndege.
 
Aisee sukari inazidi kupaa kwa kasi kwelikweli sijajua shida ni nini maana binafsi sijasikia taarifa kutoka kwa mamlaka, huku kwetu sukari 4000 Tz shilingi kilo moja
 
Back
Top Bottom