Suala la Tume Huru au Katiba hatma yake ni Madaraka na si maslahi ya wananchi. Tuweni macho

Tafakari yetu

JF-Expert Member
Apr 19, 2021
1,502
4,408
Habarini wakuu,

Tangu mjadala wa wapinzani wengine kudai tume huru ya uchaguzi na wengine katiba mpya kuingia katika taswira mpya baadhi yetu tumeingiwa na mashaka. Je, kwa nini wasimamie kitu kimoja? Je, wanaofanya hivyo ni kwa maslahi ya nchi au wananchi?

Nimejipa muda wa kusikiliza pande zote mbili, upande wa wanaotaka tume mpya na upande wa wale wanaohitaji katiba mpya na kubaini yafuatayo:

i) upande wa wanaotaka tume huru, hawa wamejielekeza moja kwa moja kusimamia agenda yao ya kutaka madaraka. Madaraka ni sehemu ya wachache hivyo hitaji la tume huru ni hitaji la wachache.

Wananchi wanawaza mbali zaidi ya tume, wanawaza barabara, elimu, huduma za afya na maji na mgawanyo sawa wa rasilimali za umma. Na zaidi ya yote wanachoangalia ni amani. Baadhi ya watu wamekuwa wakijiuliza nami pia natamani kufahamu kutoka kwa wadai tume huru: Kama tume ni kwa ajili ya nchi kwa nini idaiwe mpaka kuhatarisha amani?

ii) kundi la pili ni la wanaodai katiba mpya. Kundi hili halijaenda mojamoja kujipambanua maslahi yake na hamu ya madaraka lakini waswahili husema fumbo mfumbie mjinga mwerevu ataling'amua.

Licha ya ajenda kuu ya kudai katiba mpya lakini kundi kundi limekuwa likipigania uwepo wa tume huru kwenye katiba mpya zaidi ya choxhote na hili linatupeleka palepale kwenye agenda kuu ya kundi la kwanza.

Kudai tume huru tafsiri yake ni kupigania maslahi na madaraka. Pia katika suala hili la tume huru ni suala linalohitaji uelewa na si ushabiki. Tumeshuhudia Mara kadhaa wapinzani wakishangilia na kusema tume ilikuwa huru wanaposhinda lakini hapo hapo sehemu wanaposhindwa hulalamika na kudai tume haikuwa huru. Je, tume huru ni nini? Elimu inahitajika katika hili

Yote kwa yote, wanaotaka katiba mpya wana maslahi yao na wanaotaka tume huru wana maslahi yao. Sisi wananchi tuwe nao macho na tuwapime kwa dhamira zao.
 
... wanaopinga Tume Huru na wasioitaka Katiba Mpya ni akina nani na kwanini? Mbona hilo husemi?

Tume zenye heshima kubwa nchi hii zimeundwa kuanzia ile ya Jaji Mkuu Nyalali, Jaji Samatta, Jaji Kisanga, n.k. wote hao wameona udhaifu mkubwa kwenye Katiba na sheria na kupendekeza ziboreshwe; Tume ya Jaji Warioba ikaundwa halafu unaleta upumbavu hapa! Who are you? Au ndio kuvimbiwa kwenyewe huko?
 
... wanaopinga Tume Huru na wasioitaka Katiba Mpya ni akina nani na kwanini? Mbona hilo husemi?

Tume zenye heshima kubwa nchi hii zimeundwa kuanzia ile ya Jaji Mkuu Nyalali, Jaji Samatta, Jaji Kisanga, n.k. wote hao wameona udhaifu mkubwa kwenye Katiba na sheria na kupendekeza ziboreshwe; Tume ya Jaji Warioba ikaundwa halafu unaleta upumbavu hapa! Who are you? Au ndio kuvimbiwa kwenyewe huko?
Umemjibu vyema. Hawa maCCM wanafikiri ni wao tu wenye Hati miliki ya kuongoza nchi.

Kama CCM hawawezi kushinda kwa kutumia Tume Huru au katiba mpya ina maana wanatuthibitisjia kuwa ni wao ndiyo wanazuia ili wabaki madarakani.
 
Back
Top Bottom