Suala la Kizushi

klorokwini

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
8,648
5,139
Baada ya kusoma thread nyingi hapa MMU nimegundua kwamba linapotendeka kosa kwenye mahusiano watu wengi wanaelekeza lawama kwa mhusika na kusahau mazingira. Ghafla jana baada ya kukosa usingizi kutokana na kuibiwa saa yangu mpya kabila la Seiko nikajikuta najiuliza hili suali.

Je Vishawishi (temptations) vina vina/havina nafasi katika kuliandama penzi la dhati (True Love)?

Naweka hii mada halaf naikimbia.
Kwaherini.
Tuonane chit chat
 
kila kitu kizuri lazima kipate mapambano.
Penzi la dhati halina exception litakutana na mapambano.
Na mapambano hayo ni ya kivishawishi zaidi.
 
Vishawishi vipo siku zoote... Iwe kwa yule ambae ana penzi la dhati ama hata yule ambae yupo katika penzi ambalo sio la dhati. Tofauti ni jinsi gani hivo vishawishi vinaathiri....

Penzi la dhati

Hapa mtu anaweza awe na vishawishi na vikamshawishi hasa lakini visiyumbishe lile penzi la dhati hata kwa chembe... Yaani anaweza mtu akatoka hapo na akalala na mtu mwingine akamaliza hamu ila bado pendo na penzi lake lipo kwa yule warohoni kwake. Msiniulize inakuaje (yaliowakuta wanaelewa kama hayajakukuta kama mimi then tujihesabu wenye bahati :eyebrows:) Hii ni maarufu saana kwa wanaume... Kwa wanawake wengi wenye penzi la dhati ni vigumu mno kushawishika na temptations za nje else kuna issue anataka kusolve via hivo vishawishi na hicho/hivo vitu ni vya msingi.

Penzi lisilo la dhati

Hapa vishawishi vyaweza yumbisha penzi ambalo lipo na kusababisha sa ingine hio source ya vishawishi iwe ni Penzi la dhani in the long run.

Klorokwin Habari yako broda? Nilikumiss mpaka imenibidi nipost...lol... Pamoja Saana.
 
mazingira huwa haya husishwi kutokana inaweza kumkandamiza mlalamikaji ndo maana watu wanaikimbia..
 
ukianza ku-consider mazingira, una-create room kwa ajili ya watu kutafuta visingizio... at the end of the day, ndiyo unaanza kusikia visingizio vya ajabu kama 'shetani alinipitia' etc
 
Vishawishi vipo na vitaendelea kuwepo! Nguvu ya penzi hupimwa katika kuvishinda hivyo vishawishi!

Na nguvu hiyo ipo kwa mtu ndio maana huyo mtu hulaumiwa pale anapoanguka ktk vishawishi!
 
Vishawishi vipo siku zoote...Tofauti ni jinsi gani hivo vishawishi vinaathiri....

Penzi la dhati

Hapa mtu anaweza awe na vishawishi na vikamshawishi hasa lakini visiyumbishe lile penzi la dhati hata kwa chembe... Yaani anaweza mtu akatoka hapo na akalala na mtu mwingine akamaliza hamu ila bado pendo na penzi lake lipo kwa yule warohoni kwake. :eyebrows: Hii ni maarufu saana kwa wanaume...

Kwa wanawake wengi wenye penzi la dhati ni vigumu mno kushawishika na temptations za nje else kuna issue anataka kusolve via hivo vishawishi na hicho/hivo vitu ni vya msingi.Pamoja Saana.
"Yes I did, but she/he meant nothing to me" - haya maneno nimeyasikia sana kwenye soup operas na movies za kidhungu, yakitoka kwa wanawake na wanaume kuwaambia wapenzi wao na mara nyingi au zote huaminiana na yakaishia hapo. Huku uswahili "confessions" kama hizo hazifanyiki kwani salama salama kinachofuatia ni talaka kama sio kisago kwanza. Swali langu ni hili, je mpenzi wako akikuambia hivyo, utachukua uamuzi gani? Utasamehe na kuzingatia "penzi lenu la dhati" au utasapa lapa?

Hiyo ya pili nyekundu nimepitwa kidogo. Ni vishawishi gani anavyoweza kuvitumia mwanamke kwa sababu anataka kusolve via hivo vishawishi na hicho/hivo vitu ni vya msingi?
 
usingeunga ningeomba ban.
Swahiba wewe tena? Umesahau tuliapa kushirikiana kwa dhiki na faraja?

Afu klorokwini muongo sana amesema yuko chit chat nimemfuata wala hayupo, kumbe hajaacha utapeli eeh? Yan sijui wampendea nini swahiba jamani!
 
Swahiba wewe tena? Umesahau tuliapa kushirikiana kwa dhiki na faraja?

Afu klorokwini muongo sana amesema yuko chit chat nimemfuata wala hayupo, kumbe hajaacha utapeli eeh? Yan sijui wampendea nini swahiba jamani!

hukumuelewa, anachit chat na wateja wa kahawa. Mi mwenyewe cjui nampendea nini. Lol. Ila shem wako nampenda zaidi swahiba.
 
Vishawishi havikosekani, swala ni jinsi ya kupambana na vishawishi.

Klowo pole kwa kuibiwa Seiko..du! inabidi ujipange kununua saa nyingine, nunua Rolex..! Afu umepoteaaa!
 
"Yes I did, but she/he meant nothing to me" - haya maneno nimeyasikia sana kwenye soup operas na movies za kidhungu, yakitoka kwa wanawake na wanaume kuwaambia wapenzi wao na mara nyingi au zote huaminiana na yakaishia hapo. Huku uswahili "confessions" kama hizo hazifanyiki kwani salama salama kinachofuatia ni talaka kama sio kisago kwanza. Swali langu ni hili, je mpenzi wako akikuambia hivyo, utachukua uamuzi gani? Utasamehe na kuzingatia "penzi lenu la dhati" au utasapa lapa?

Hiyo ya pili nyekundu nimepitwa kidogo. Ni vishawishi gani anavyoweza kuvitumia mwanamke kwa sababu anataka kusolve via hivo vishawishi na hicho/hivo vitu ni vya msingi?


Kuna binti/Mwanamke anaweza akawa na mtu wake ambae anampenda saana kwa dhati. Ila ikatokea akapata tatizo na mara nyingi huwa related na material based. For instance inaweza ikawa the following cases...



  1. Ana mpenzi wake ambae wana hali mbaya kimaisha... ikatokea kuna nafasi ya kazi ambayo yaweza okoa na kuboresha hali mbaya walo nayo (ambayo haina hope ya kutatulika kamwe wala hakuna mwanga kua itatatulika) Then another Man (for men are really good at reading these signs) anatumia hicho kama kigezo cha kumpata huyo mwanamke na kumuahidi kazi mpenziwe (makubaliano ambayo mara nyingi hua ya siri); Na in most cases it works... thou yaweza buma. Na tatizo huja pale huyo mwanaume anapotaka aendelee kupewa hio huduma. Sad but haya mambo yapo.
  2. Ana Mpenzi wake anampenda... ila hali yake ni ya kawaida mno nae ajitahidi kihivo hivo kuendehsa maisha ila mwanamke ana mlolongo wa matatizo.... kama vile Umasikini kwao, wadogo wanaosoma, wazazi wasiojieweza na mengine kibao! Hio yaweza tumika kama weapon kwa mwanaume mwenye pesa kua aweza toa hizo huduma kama ataku mpenzi wake. Wakuta ki Mantik she has to agree ili walau aweze okoa jahazi....

Mammamia.... Ni mengi, ila hayo nimetoa kama mfano.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom