Wapenzi wa aina hii ni HATARI kwa afya yako...

Wapenzi wa aina hii ni HATARI kwa afya yako...

AshaDii

Platinum Member
Joined
Apr 16, 2011
Posts
16,189
Reaction score
18,117
Habari Wapendwa wa Jf na wana MMU woote...

Kwa mara nyingine nashare yale niliyo nayo katika mahusiano yetu haya ya kila siku ambayo tunafurahia na wakati mwingine kutuendesha.

Ukiwa na mtu (mpenzi au rafiki, mchumba ama mwenza) mara nyingi matarajio huwa ni kufurahi na kufarijika juu ya mwenzi wako ama yale ambayo yahusiana na nyie. Mara nyingi, wengi hutaka kuwa moja ya sifa iwe mtu wake huyo awe sehemu ya maisha yake kuwa na amani na furaha kwa namna moja ama nyingine…

Kama wanadamu kukwazana hakuepukiki na wnegi wanasema ni moja ya kuimarisha mahusiano yenu. La msingi ni kuwa, hata mkikwazana vipi mna uwezo wa kurudi kwenye mstari na kuendelea na mahusiano yenu kama kawaida. Hata hivo wanadamu tumetofautiana na kuna wale ambao waweza kuwa wapenzi ila mmoja wao akawa ni mwenye tabia ya kudhoofisha afya (psychologically, physically hata emotionally) ya mwenzi wake aidha kwa makusudi ama kwa kutojitambua. Mtu wa namna hii akikuta mpenzi wake ni ‘hewalaah!' kwa kila jambo ndipo ambapo huyo muathirika hugeuka trailer.

Kawaida hawa wapenzi ambao ni hewala maarufu hapa (MMU) kama ‘Msukule wa Mapenzi' (in courtesy of ‘Mbu') wengi sana huwa hawajitambui. Kwa maana nyingine hata wewe msomaji unaweza kuwa mmoja ya hao watu na bado ukawa hujui. Unaweza jitazama upya kwa kuangalia baadhi ya viashiria hapa chini kupima kama mwenzi wako anaimarisha ama kudhoofisha afya yako. (Take note kuwa mara nyingi ni kama huyo mtu ana zaidi ya traits 3/4 ama zaidi ya hizi zilizootedheshwa.)

Mbinafsi

Kila mwanadamu ana kiwango Fulani cha ubinafsi… Ila hunatofautiana tokana na mahala pa kuutumia huo ubinafsi. Katika watu ambao ni muhimu, mpenzi ni mmoja wa mtu ambaye kikawaida tunapaswa kila mmoja wetu kupunguza ubinafsi kwa mpenzi wako hasa kama kuna mapenzi ya kweli. Hata hivyo kuna watu ni wabinafsi mno, kila kitu katika maisha ya kila siku hadi mahusiano yake ni lazima aangalie ‘yeye' anafaidi vipi, anapenda ama kunufaika namna gani ndipo aone kuwa kitu husika kinafaa. Huyu mtu mbinafsi ‘yeye' ndiye kipaumbele na wa kuangalia kwanza kabla ya mpenzi wake; awe ni girlfriend, rafiki, mchumba ama mwenza.

Anathamini sana wengine kuliko wewe

Naamini wengi wetu tunapenda mpenzi ambaye ana imani, ni mwepesi wa kusimamia na kutatua matatizo ya watu wamzungukao; haijalishi hao watu ni ndugu zake, ndugu zako ama tu watu baki. Mara nyingi mtu wa namna hii huwa ni mtu wa watu na mtu wa kuhakikisha kuwa kila amzungukae ana furaha na amani. Katika hili kundi, kuna yule ambaye anathamini watu wake wote sawa sawa akiwepo mpenzi wake. Kuna yule anayemthamini zaidi mpenzi wake, haijialishi ni kitu gani atasikilizwa kwaza mpenzi na wengine watafuata, na kuna yule ambaye anathamini zaidi watu wengine waliowazunguka (ndugu zake na wako pamoja na ndugu na jamaa) kuliko mpenzi kwa kasumba na imani kuwa sababu wako wote basi tatizo lake litatatuliwa tu pale atakaporejea. Hii mara nyingi ni hatarishi kwa penzi/mahusiano sababu inaweza fika wakati mpenzi husika akajisikia kutothaminiwa ama kupendwa.

Asiyejua wajibu wake juu ya mpenzi wake

Kuna mtu mwingine ambaye ni kweli anakupenda sana, ila haelewi wajibu wake kama mpenzi ni upi. Yeye mradi wewe ni mpenzi wake basi! Hapo, yeye kishamaliza, hajui welfare ya mtu wake ipo vipi? Hajui kuwa mpenzi wangu anahitaji kitu fulani ambacho kipo ndani ya uwezo wangu wacha nimfanyie… TAHADHARI: Kitu ndani ya uwezo sio kinachoegemea pesa tu, wakati mwingine hata utu; kuwa maybe unakuta mpenzi wako ana shughuli kibao na amechoka, angalia kitu ambacho kipo ndani ya uwezo wako na uoneshe support. Hii ukiiangalia inakuwa kama inaingiliana na ‘ubinafsi' ila sio… Mara nyingi mtu wa namna hii hata sio kuwa anafanya makusudi, ila tu anakuwa hajui na akielekezwa hana hiana na huelekea na kubadilika ingawa taratibu.

Mwenye tamaa

Huyu ni yule anayependa na kutamani vitu hata ambavyo si vya msingi na hahitaji… Na mara nyingi huwa tatizo kwa afya ya mwenzi wake hasa kama ni tegemezi kwa mwenzi wake na huyo mwenzi wake uwezo wake nyakati nyingine ni mdogo kuliko mahitaji (tokana na tamaa) ya mhusika. Inawezekana akawa sio tegemezi ila tokana na vile ambavyo mnaishi; let's say mna joint account, mna mipango ya msingi na mda mrefu, mmeweka malengo ya kitu fulani – inaweza pelekea kuumizwa mara kwa mara. Unaweza jikuta mmojawapo yupo makini sana na matumizi na zikitumika ni vitu vya msingi, lakini mwenzio akawa anatumia pesa kama anachota tu kisimani. Mwisho wa siku ukiangalia vitu ambavyo anatumia, you feel like crying! Havina maana hata kwake mwenyewe!

Asiye jiamini (Insecure)

Kwa sababu zozote zile alizonazo yeye mwenyewe kichwani na mayoni kwake haamini kuwa mpo pamoja, anakumiliki ama kuwa mpenzi wake anampenda na kuwa hapo kafika. Hii humfanya kusikiliza saana maneno ya watu hasa kama yanamuharibia mpenzi wake, humfanya kuwa na wivu usio kupita kiwango tarajiwa, humfanya saa ingine kusababisha kugombana na mpenzi wake mara kwa mara kwa vitu vidogo vidogo na mara nyingine humfanya hata kukuchunga sana katika kila ufanyalo sio kwa kufuatilia usalama au uwepo wako BALI kwa ku monitor kila ufanyalo kwa hofu ya kuwa utasaliti. Mara nyingi mpenzi wa namna hii siku za mwanzo unaweza ona sawa lakini kadiri muda unavyokwenda anaweza kukukondesha kiuhalisia na hata kisaikolojia.

Anayekupenda kupitiliza

Kupendwa kuna raha yake… Sana! Ila raha ya kupendwa upendwe na mtu mwenye akili yake timamu na ina uwezo wa kupima na kuyasimamia vema hata masuala yake ya mapenzi. Inapotokea kuwa mtu kakupenda sana kama vile wewe ni Mungu wake na wala haoni mabaya yoyote (hata kama yapo yanafanyika –iwe na mpenzi wake ama yeye mwenyewe) inaweza kuwa tatizo. Mtu wa kupenda akakithiri na akikupenda hawezi ishi bila wewe ni hatari, hata aweza kuua. Aweza kuuondoa uhai wake mwenyewe (hakuna ambaye anapenda aone mwanadamu anajiua kwa ajili yake), aweza pia kuondoa uhai wa yeyote ambaye anadhani kuwa ni hatari kwa penzi lake (hata kama ni watoto, mpenzi wa mtu wake) na pia anaweza ondoa uhai wa huyo ampendaye!

Hakupendi

Watu wa kundi hili ni wa aina mbili:

Aina ya Kwanza; Kuna asiyekupenda ila ana utu na imani juu ya wanadamu wenzie. Anaweza asikupende ila atakufanya ujisikie na mtu ambaye anakufaa katika maisha yako. Ubaya wa huyu mtu, siku yoyote tu akipata mtu anayempenda ni tatizo; hata ajitahidi namna gani aendelee na tabia ileile ya kukujali inakuwa wakati anachemka… Hii ni tokana na ukweli kuwa kila mwanadamu wakati fulani huchoka kufanya kitu tokana na wajibu na sio kwa kupenda.

Aina ya Pili; hakupendi na wala hajali na hukufanyia vituko kibao ila kwakuwa mpenzi wake anakuwa kampenda sana anakuwa haoni kabisa uchimvi wa mpenzi wake huyo. Mara nyingi huyu mtu wa namna hii huwa na mtu sababu kuna kitu anahitaji toka kwake. Inaweza kuwa mwili wake kwa tendo la ndoa ama ‘showoff', inaweza kuwa sababu ya vitu (material things) ama kuna faida (benefits) anapata akiwa na huyo mpenzi anayetumiwa.

Mwathirika

Hii ni maarufu katika wapenzi ambao wameathirika na magonjwa ambukizi, yasiyo tibika na ya kingono kama vile HIV/AIDS… Pia kuna ambaye ni mwathirika wa magonjwa ya zinaa ama magonjwa yoyote ambukizi anaweza asielewe lakini kuna wale ambao unakuta anaelewa fika afya yake ila hata hajali kuwa anaathiri vipi afya ya mwenzie (bila kujali kama huyo mwenzie hajui afya yake ipo vipi). Ni tatizo ambalo linaongozwa zaidi na wanaume watu wazima na kuipelekea hasa kwa mabinti wadogo ambao ni rahisi kutongozwa na kulaghaika tokana na dau dogo la pesa (ama vishawishi vya mwelekeo wa kifedha) ukilinganisha na anapomchukua mwanamke ambae ni mtu mzima.


Mropokaji hadi kumplekea kuwa Muongo

Katika mapenzi uongo ni muhimu nyakati nyingine… Kuna mahala wamlinda mpenzi wako kwa kuongopa huku mwisho wa siku ukitambua kuwa lazima uje urekebishe kwa kuweka sawa. Ila kuna wanadamu wamezaliwa haoni kabisa raha kutoongopa, huongopa hata vitu vidogo dogo na visivyo na msingi… Huyu mtu anakuwa na aina ya uwongo ambao baada ya mda mfupi tu mtu wake na watu walio wazunguka wanang'amua kuwa ni muongo! Mtu wa namna hii hukosesha raha katika kila aongealo… Na mwingine ana maneno meeengi, matendo sifuri! Hii tabia huchangia sana kuonekana mtu wa ovyo na asiyeaminika. Ni aina ya mtu ambaye ukiwa na wenzio unaogopa akifungua kinywa kutaka kuongea… Lazima aharibu tu kwa kupitiliza maongezi. Unaweza ukawa unampenda ila kasoro yake hio ikakosesha raha kabisa...

Mwenye Dharau (In courtesy of @BADILI TABIA )

Kuna wapenzi wenye dharau sana, inaweza kuwa dharau kwako mwenyewe, aidha kwa kila utendalo ama kukuona kama huna uwezo wa kufanikisha lolote.. Ama yaweza kuwa kukuona kana kwamba huwezi jitegemea nakadhalika. Mara nyingi hizi dharau huwa zinakuwa tokana na wewe mwenyewe (yawezekana kuna baadhi ya mambo ambayo unafanya yanaleta dharau dhidi yako toka kwake) AMA yaweza kuwa ni dharau zake tu tokana na tabia yake ya kudharau watu.
Mwingine anaweza asikudharau wewe lakini akawadharau watu wako wa karibu ambao pia ni msingi katika maisha yako... Kama vile wazazi, siblings, marafiki nakadhalika. Hili suala hata kama wampenda mpenzi wako kuna wakati inaweza changia kukuleta kukosa raha hasa katika mazingira ya mpenzi wako kuwepo karibu na watu wako wa karibu ambao anawadharau.


Haya ni baadhi ya maeneo ambayo nimeona kuwa yanaweza muathiri mhusika kwa wenye wapenzi wa namna hizo kwa namna moja ama nyingine. Inawezekana kuna ambaye hakubaliani, inawezekana kuna ambaye anayo ya zaidi; nawakaribisha tuweze jadiliana tupate kitu na tuone namna gani tunaweza tambua wapenzi wetu kama wana tabia hizo. Sisemi kuwa hawafai, ila ukitambua mapema ni rahisi hata kurekebishana kama mtu wako ana muelekeo wa kuelewa madhaifu yake.

Naomba ushirikiano wenu wa mawazo/mchango/mitazamo...

Pamoja Saana.

AshaDii.

 
Here we go again, the phenomenon of love and the proverbial 'it's always somebody else's fault'.

But such is life.

There is always someone/something who/which is at fault when things do not go accordingly, where to place that fault; depends on one's mtazamo.. Ofcourse backing it up with reasons which should be sound enough.
 
Nianze na asiyejua wajibu kwa mpenzi wake, kuna wengine hawajui kiukweli, lakini kuna wengine hawataki kujishughulisha na uhusiano huo sababu wanajua fika kuwa wanapita tu. So hii ya kutotimiza wajibu wakati mwingine ni dalili ya mtu kutotaka 'commitment'. Kama wote mkiamua mnapitisha tym its okay, ila kama mmoja anatarajia ndoa au mahusiano ya kudumu ni tatizo sana.

kutojiamini, inaweza kuwa ni ishu ya mtu binafsi au wakati mwingine ni kipindi cha 'denial ya mahusiano kuvunjika'
kweli kuna watu hawajiamini kwenye mahusiano kwa sababu kadha wa kadhaa, sitaingia kwenye sababu hizo.

Ila kuna wengine kutojiamini kunawapata pale wanapoona mahusiano hayo hayaendi kama walivyotarajia, na wakati huo huo hawajawa tayari kuondoka kwenye mahusiano hayo. Inakuwa kama mtu analazimishia mahusiano, akiona dalili ndogo tu inayoweza kutia mahusiano mashakani basi ni 'mtifu wa nguvu'
ni vizuri ukiwa na mpenzi ukajaribu kutafuta sababu ya kutojiamini kwake.

mwathirika, hili ni janga la kitaifa, kuna watu wanajijua na bado wanawatenda, may their souls rest in hell!
 
labda naweza ongezea mitazamo ya maisha, kuna mtu una-date naye lakini unajikuta mna mitazamo tofauti kabisa ya maisha, akiona njano, wewe unaona nyekundu.
Hii hudhoofisha mahusiano kabisa, na kama hamwezi kuwa na point mnayoshare mitazamo bora kuondoka mapema.
 
Oook yeah. Problem ni kuwa hizi sifa hatuzionagi when it matters most. We are supposed to see these wakati wa uchumba. Bahati mbaya kipindi hiki Mambo mengi yanakua masked unapogundua mara nyingi unakuwa ushajicommit! An eye opener kwa wale ambao bawajala viapo!:
 
Nianze na asiyejua wajibu kwa mpenzi wake, kuna wengine hawajui kiukweli, lakini kuna wengine hawataki kujishughulisha na uhusiano huo sababu wanajua fika kuwa wanapita tu. So hii ya kutotimiza wajibu wakati mwingine ni dalili ya mtu kutotaka 'commitment'. Kama wote mkiamua mnapitisha tym its okay, ila kama mmoja anatarajia ndoa au mahusiano ya kudumu ni tatizo sana.

kutojiamini, inaweza kuwa ni ishu ya mtu binafsi au wakati mwingine ni kipindi cha 'denial ya mahusiano kuvunjika'
kweli kuna watu hawajiamini kwenye mahusiano kwa sababu kadha wa kadhaa, sitaingia kwenye sababu hizo.

Ila kuna wengine kutojiamini kunawapata pale wanapoona mahusiano hayo hayaendi kama walivyotarajia, na wakati huo huo hawajawa tayari kuondoka kwenye mahusiano hayo. Inakuwa kama mtu analazimishia mahusiano, akiona dalili ndogo tu inayoweza kutia mahusiano mashakani basi ni 'mtifu wa nguvu'
ni vizuri ukiwa na mpenzi ukajaribu kutafuta sababu ya kutojiamini kwake.

mwathirika, hili ni janga la kitaifa, kuna watu wanajijua na bado wanawatenda, may their souls rest in hell!


Kongosho umeongea mambo ya msingi na ni kweli kabisaa, kuna kitu nimetoka nacho hapo; hasa hapo kwenye kutojiamini. Nimejifunza kitu... I guess woga wa kujua mahusiano mhusika unayataka sana kuliko mwenzio nayo ni mbaya na yaweza pelekea huko. Sad.

Asante saana kwa mchango wako, ukipata zaidi tafadhali share.
 
Ahsante.Wakati mwingine huwa tunadhani tupo kwenye love kumbe ni ignorance

Zion D, Naamini inakuwa ni love kweli... Nadhani unapopenda, unapenda mno hadi huoni kwa yale ambayo unatendwa. Once mapenzi yakipungua walau kidogo na ukaanza kuona reason basi ndipo inakuwa rahisi kuona hayo madhaifu na kama yakugusa.
 
Oook yeah. Problem ni kuwa hizi sifa hatuzionagi when it matters most. We are supposed to see these wakati wa uchumba. Bahati mbaya kipindi hiki Mambo mengi yanakua masked unapogundua mara nyingi unakuwa ushajicommit! An eye opener kwa wale ambao bawajala viapo!:

Kwa wengi ndio hivo... Ni vigumu sana kumsoma tabia mpenzi wako kama mlikutana moja kwa moja kwa kutongozana. Unaweweza mjua vema ni yule ambae ulifahamiana nae kabla ya kuwa na mpango huo. Ndio maana wazazi walikuwa wakisisitiza zamani kuoa toka familia ambazo zinajulikana, ili kujua tabia ya mke ama mme. Sasa hivi tunatongozeana kwenye mabaa, basi kaazi kweli kweli.
 
Pokea like yangu toka moyoni mwangu dada AshaDii. Sijawahi kusoma andiko lako nkakosa kujifunza kitu. Am blessed sana.. Usiwe una adimika sana dada

Nicas, tajitahidi saana nisiadimike tena :becky:. Kama unavyo ona... Sana hebu nipe mchango wako katika hili suala. What do you think?

hivi ukifanya dating more than a year utashindwa kugundua hata mojawapo ya hizi tabia?

Change, Inategemea na ukaribu wenu, mnashinda pamoja kwa mda gani, huyo mpenzi wako ni fake/genuine kiasi gani na vitu kama hivo.

But betters still, kama nilivyogusia, anaweza kuwa na hizo tabia, lakini sababu wampenda sana, husikii wala huambiwi..
 
Back
Top Bottom