Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 10,883
- 2,765
Nasoma gazeti la Mwananchi hapa kuhusiana na mvutano aidha watoto waende likizo au wabaki shuleni kujisomea. Mjadala huu ulikuwa Bungeni. Kuna hoja kuwa baadhi ya mikoa kupitia wakuu wa mikoa imepanga utaratibu wa kuongeza "ufaulu". UFAULU kwenye maeneo yao.
Sehemu nyingine Mbunge na mmiliki wa shule, ndugu Rweikiza anasema, "wanajitolea (wazazi) wakati wa likizo, kwenye madarasa wanaweka magodoro na wasio na uwezo wanaweka nyasi nyingi, wanaweka taa watoto wabaki pale wasome usiku na mchana waweze "kufaulu". KUFAULU. Hoja hapa ni kufaulu. Hawa wadau hawaoni aibu katika kujadili hili. Wafaulu then what?
Kwa mwenendo huu, huu mtaala mpya wa elimu upite tu haraka ili kuwajenga hawa watoto kuelewa na sio kufaulu. Wakuu wa shule wanatafuta status za shule zao zionekane zimefaulisha kumbe wamewakaririsha watoto. Wanatoka na spirit hiyo toka sekondari kwenda vyuoni na wanaendeleza kukariri na kutoka huko na GPA za kutisha. Baadae unakutana na wasomi, madokta, na maprofesa wenye elimu ila hawana akili.
Ukweli uko wazi. Hawa wasomi wanajua zaidi mambo waliyojifunza kuliko wanayokutana nato katika maisha halisi. Ndio hawa unawakuta kila siku wanapinduana kwenye familia. Mume mbabe, mke mbabe. Wote wasomi. Majirani wanaonekana vijakazi, n.k.
Wakati mwingine unamsikiliza kijana anazungumza kwenye TV akitoa hoja unamuona kabisa akivuta kumbukumbu ya kile alichosoma darasani na mbaya zaidi anatumia na kingereza kwenye baadhi ya maneno kuashiria kuwa hawezi free style.
Watoto waachwe waende likizo, tena isiwe hiyari. Na huu mtaala mpya uje mapema ili kuwapa hawa watoto machaguo ya kufanya kuloko kuanza kukariri sepal, petal, kikonyo, n.k.