Farolito
JF-Expert Member
- Sep 10, 2018
- 11,634
- 26,373
Mheshimiwa Waziri,
Kumekuwa na mtindo wa wamiliki wa shule kuamua tu kwa utashi wao kubakiza watoto shuleni(madarasa ya mitihani) kwa kigezo kwamba wapate muda wa kumalizia mitaala tena bila kushirikisha wazazi huku wakiwa tayari wamepanga na gharama zao.
Hivi walimu wanashindwa vipi kumaliza mtaala kwenye muda uliopangwa?Kibaya zaidi wamekuwa wakiongeza gharama za ziada za Tuition fee na transport hasa kwa shule binafsi.
Sasa kama lengo la walimu ni kumaliza mtaala hili si jukumu lao,kwanini gharama zirudi kwa mzazi?
Je ni sahihi mtoto kusoma bila kupumzika?Kuna watoto wanasoma mbali na wazazi wanahitaji kuonana na wazazi wao ambao hawajawaona kwa muda mrefu,sasa kumshikilia mtoto shuleni muda mrefu kisaikolojia imekaaje?
Mimi binafsi naona shule zimeamua kubuni tu mradi wa kujipatia kipato kwa kigezo cha kumaliza mitaala.
Tayari kuna shule zimeshatoa taarifa kwamba darasa la nne hawatafunga shule ili waendelee kufundishwa,Je mmeruhusu?
Tunaomba hili suala lizuiliwe kisheria na sio kwa matamko ya kila mara maana nakumbuka mwaka Jana ulitoa tamko la kuzuia watoto kubakizwa shuleni ila naona linajirudia tena.
Pia soma: Waziri wa Elimu Prof. Mkenda, sisitiza umuhimu wa kutowabakiza watoto shule kipindi cha likizo
UPDATE:
Wizara imeitikia wito wa wadau, soma Serikali: Wanafunzi wasizuiwe kwenda likizo