Stori ya David Masha: Ajali iliyompa ulemavu wa kudumu, kukubali matokeo na kutokata tamaa

Nimesoma hii story imenigusa sana, imenipa funzo kubwa sana.

Kwanza, pole yake kwa magumu aliyopitia.

Pili, huyu ni mpambanaji anayepaswa kuigwa kwa kuwa pamoja na changamoto ya ulemavu bado aliamini katika kujitafutia kipato chake na si kutegemea kuomba.

Namuombea kwa Mungu afike mbali, afanikiwe zaidi na ndoa yake iwe ya furaha.
 
Wewe ni simba wa vita. Pia binti aliyekubali muoane ni malkia shujaa .nina imani Mungu atawajalia watoto wema waje kuwatunza uzeeni. HONGERA. kama usingekuwa mwanakabumbu mzuri ,si ajabu historia yako ingesomeka tofauti, ndiyo maana hakuna mzazi anayepenfa mwanae awe mchezaji maishani. Lakini nani ajuaye kesho yake? HONGERA fighter.
 
Nakupa hongera sana David lkn hongera zaidi nampa dada yako Idda na mume wake, hao watu washike tena sana, moyo waliokuonesha ni binadam wachache sana wanaweza. Ingekua familia nyingine dada ako angeshaingia kwenye mgogoro mkubwa na mumewe, lkn Mungu ni mwema dada na shemeji walikupokea kiroho safi. WABARIKIWE SANA!

Sent from my SM-A217F using JamiiForums mobile app
 
Dave the fighter. Nakukubali sana jirani, kwa sie tunaofanya kazi na wewe huku Tanga tunautambua uwezo wako 'upstairs'

BTW ametoa namba zake kwa watakaoguswa kumchangia anataka kununua kiti cha umeme (kama sijakosea) kitakachomsaidia kwa urahisi kuliko alicho nacho sasa. Tumuunge mkono mpambanaji
 
Dave the fighter. Nakukubali sana jirani, kwa sie tunaofanya kazi na wewe huku Tanga tunautambua uwezo wako 'upstairs'

BTW ametoa namba zake kwa watakaoguswa kumchangia anataka kununua kiti cha umeme (kama sijakosea) kitakachomsaidia kwa urahisi kuliko alicho nacho sasa. Tumuunge mkono mpambanaji.
Nipeni namba!
 
Pole sana kaka mkubwa,,, nilipenda kuuliza kuwa ulitumia njia gani adi mikono ikapata fahamu na kufanya kazi
 
Dave the fighter. Nakukubali sana jirani, kwa sie tunaofanya kazi na wewe huku Tanga tunautambua uwezo wako 'upstairs'

BTW ametoa namba zake kwa watakaoguswa kumchangia anataka kununua kiti cha umeme (kama sijakosea) kitakachomsaidia kwa urahisi kuliko alicho nacho sasa. Tumuunge mkono mpambanaji
Wekeni Namba na jina litakalotokea tafadhali
Msalimie sana
Dahh🙌🏽
 
Back
Top Bottom