Wale wenye ulemavu jifunzeni kujikubali

James Hadley Chase

JF-Expert Member
Mar 25, 2020
1,576
2,658
USIKIVU HAFIFU (HARD OF HEARING)

Kwa wale wenye kusumbuliwa na masikio,uziwi na hata usikivu hafifu. Baadhi hamna ujasiri wa kujiweka wazi kwa wengine kuhusu changamoto mliyonayo.

Yaani mnashindwa kusema kuwa nina changamoto ya masikio. Mimi sisikii vizuri. Mimi nina tatizo la kutosikia. Unajikuta unaishia kupata tabu kuwasiliana na wengine na kujenga mahusiano.

Unateseka kumuelewa mwenzako huku mwenzako akiteseka kukuelewa wewe.

Achilia mbali wale ambao wakipiga simu wakaambiwa tuwasiliane kwa meseji wanaendelea tu kupiga simu na hata kutoa tuhuma zisizo na staha.
Ooh hapokei simu huyu tapeli!
Ooh hapendi kuongea na simu huyu ni tapeli!

Kwenu waathirika wa masikio. Poleni kwa changamoto mliyonayo.

Pia msiogope kuanzisha mawasiliano na wengine maana bila mawasiliano hakuna mahusiano.

Mawasiliano huanzisha mahusiano.
Mawasiliano mazuri hutunza mahusiano.
Mawasiliano ndio huendeshao mahusiano.
Mahusiano mabaya huvunja mahusiano.

Hii inamaanisha kuwa mahusiano yoyote uyatakayo huanza na mawasiliano,
Iwe mahusiano ya kazi,biashara ama mapenzi.

Hauna budi kujiweka wazi hauna budi kujikubali.

Hauna budi kuwa wa kwanza kujifurahia na kuonyesha wengine furaha iliyoko ndani yako

Hauna budi kuwa wa kwanza kujieleza kuhusu tatizo lako kwa wengine,itasaidia kupunguza unyanyapaa ile kusimangwa kisogoni kuwa
Halisikii hilo!
Ni li kiziwi hilo!
Lidada lizuri ila likiziwi!
Likaka lizuri ila likiziwi!!

Na dhihaka nyingine zote mnazokutana nazo,

Ni vyema kuwa na utaratibu huu.

Mnapoanza mawasiliano na mtu ni vyema ukajieleza sio lazima ila ni muhimu itakupunguzia kebehi na mishangao!

Mfano mtu anakusalimia habari dada au habari kaka,

Ukibahatika kumsikia mjibu salama ndugu yangu, Kwema? Mimi nina tatizo la kutosikia vizuri au mimi sisikii vizuri unapozungumza nami naomba usichoke kunisemesha unapoona sikuitikii pengine nitakua sijakusikia. Muelekeze namna nzuri ya kuwasiliana nawe ili umuelewe vyema kisha achia tabasamu usoni mwako hii itamuonyesha muhusika kuwa unajikubali na una raha pia changamoto yako haujaiona kama ni kikwazo wala hujitiishi huruma maana hata yeye huenda anayo changamoto inayomsumbua ndani kwa ndani haionekaniki kwa macho.

Kwa wale mnatumia lugha ya alama pia sio vibaya kumuelekeza mtu kama hataweza mshauri mnaweza kuwasiliana kwa kutumia simu mnaandika meseji mnazungumza vizuri tu.

Kwenye simu njia nzuri ya kuwasiliana na mtu ili akuelewe kwa haraka ni meseji,
Usijifungie wala kujiwekea kikwazo kukosa mahusiano kwasababu ya tatizo la masikio,
Uziwi sio kikwazo. Usikivu hafifu sio kikwazo.

Ondoa kikwazo kwa kujieleza na kujiweka wazi bila aibu.

Mtu akikukataa usihusishe hisia zako kuwa umekataliwa kwasababu ya changamoto ya masikio.

Wanaachwa kina Wema Sepetu na Diamond na hawana ulemavu wowote itakua sembuse wewe? Kwanza kuachwa ni kitu cha kawaida sana, Hivyo isikutie unyonge. Ukiachwa fahamu sio chaguo lako na utapata aliye chaguo lako!

Pili usijifungie ndani unajinyima fursa
Usiogope kujieleza kuhusu tatizo lako unapoteza nafasi ulizokusudiwa.

Kwa jamii yetu. Mtu mwenye usikivu hafifu ama ambaye hasikii ni vyema kumuuliza njia gani nzuri ya kuwasiliana nae akakuelewa.

Sio vizuri kujipatia uzoefu na utaratibu ulionao wewe bila kutambua muhusika kiwango chake cha usikivu kipoje. Kuna watu mkishaambiwa mtu ana tatizo la masikio mnaongea kwa sauti ya juu sana kama spika za matangazo mkidhania mnamsaidia mtu kusikia wakati mnamuumiza.

Kuna wengine mnaongea kwa ishara wakati muhusika haielewi lugha ya ishara.

Kuna mnaongea kwa sauti ya chini sana na kufoka muhusika anapokua hajakusikia.

SIO KITU KIZURI,
Tujifunze kuwa tuko makundi tofautitofauti na inafaa sana kuelewana!

#USIKIVUHAFIFU
#USIKIVUHAFIFUSIOKIKWAZO
#HardOfHearing
#hearingloss
 
Jamii ingeanza kutambua namna nzuri ya kuzungumza na hawa watu, jamii ingekuwa na upendo wenye kuondoa dhihaka, unyanyapaa, vicheko na kadhia zingine, jamii ingekuwa na uelewa kuwa hujafa hujaumbika... WENGI WANGEKUWA NA UJASIRI MKUBWA SANA.

Shida kuuuuubwa inaanzia kwenye jamii ngazi ya familia mpaka juu. Mtu akinyanyapaliwa mara mbili tatu anatoa wapi ujasiri wa kujieleza? Ikiwa hali yenyewe ni stress tupu?

Wengi si kwamba hawapendi. Ila ukiongea nao ndio utagundua shida inaanzia kwa watu waliowazunguka.

Hushangai mpaka leo watu wanaogopa kusema hali zao za afya? Jamii ya ovyo tuliyonayo ni chanzo cha nafsi nyingi kuishi kwa mateso ambayo hayapaswi kuwa mateso.

Zaidi, nikupongeze kwa kugusia jambo hili.
 
Mbona wengine wanajikubali
Wako mpaka wakurugenzi wa makampuni ni walemavu na wanapiga
Kazi fresh tu

Ova
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom