Lucas Muhomba, mwendesha bodaboda aliyepata ulemavu wa kudumu baada ya kuvamiwa na "abiria" wake

A43

JF-Expert Member
Nov 18, 2023
385
757
This in not Fair, kijana kaonewa sana, nikitafakari sana nakosa chakusema

==========

Kijana Lucas Muhomba mwenye umri miaka 24 akiwa kwenye majukumu yake ya kawaida ya usafirishaji (bodaboda) alipata abiria kutoka Dumila kuelekea Mkundi kwa malipo ya 3000 ambapo alipofika mbele akaita wenzie wakamvamia wakamfunga kamba mikono na miguuni, wakamuweka mchanga mdomoni na kumtupa kwenye pangale (nyumba ambayo haijakamilika).

Baada ya kukaa kwa siku tatu Hospitali miguu mikono ilioza na alipopelekwa Muhimbili Madaktari wakamwambia inabidi akatwe miguu na mikono na hivyo Lucas amepata ulemavu wa kudumu.
 
Aisee! Bora hata hiyo picha imeondolewa. Maana inahuzunisha sana. Kuna watanzania hawana tofauti na wanyama kama mbweha. 🙁
 
Hivi huyu baada ya kuumizwa hivyo,hao watu walichukua pikipiki
Yake????
Majibu tafadhali

Ova
 
This in not Fair, kijana kaonewa sana, nikitafakari sana nakosa chakusema

==========

Kijana Lucas Muhomba mwenye umri miaka 24 akiwa kwenye majukumu yake ya kawaida ya usafirishaji (bodaboda) alipata abiria kutoka Dumila kuelekea Mkundi kwa malipo ya 3000 ambapo alipofika mbele akaita wenzie wakamvamia wakamfunga kamba mikono na miguuni, wakamuweka mchanga mdomoni na kumtupa kwenye pangale (nyumba ambayo haijakamilika).

Baada ya kukaa kwa siku tatu Hospitali miguu mikono ilioza na alipopelekwa Muhimbili Madaktari wakamwambia inabidi akatwe miguu na mikono na hivyo Lucas amepata ulemavu wa kudumu.
Binadamu kiumbe hatari sana,
Kwenye mihangaiko ya kutafuta pesa hakikisha unapata pesa itayokufanya ule vizuri na ulale vizuri pia. Hiyo mil 1 ya dhuruma inaweza wapatia chakula kizuri ila haitawapa usingizi mzuri.
 
Hivi huyu baada ya kuumizwa hivyo,hao watu walichukua pikipiki
Yake????
Majibu tafadhali

Ova
Ndiyo lilikuwa lengo lao na walifanikiwa.

Ila walichokifanya wakisikia balaa walilomuachia huyu bwana mdogo pamoja na roho zao za wizi nafsi zitawauma sana,wataambiana kwanini wasingetumia option nyengine zaidi ya hiyo ya kumfunga mikono na miguu?
 
Binadamu kiumbe hatari sana,
Kwenye mihangaiko ya kutafuta pesa hakikisha unapata pesa itayokufanya ule vizuri na ulale vizuri pia. Hiyo mil 1 ya dhuruma inaweza wapatia chakula kizuri ila haitawapa usingizi mzuri.
Huko walipo kwa habari walizoziacha usiku wa siku ya tukio hakuna atakaeacha kujilaumu.

Mtu aliyekuwa mzima mikono na miguu yake wiki mbili nyuma leo anabaki hana hata kimoja then wewe ndiye sababu huwezi ukawa na furaha ya maisha never,wazungu hufikia kujiua kwa kushindwa kuhimili ndoto mbaya wanazoziwaza kuhusu matukio mabaya kama haya
 
Kabisa aisee, we are universe maisha tunayoishi ni cycle inayojirudia hivyo basi hawawezi baki salama kwa kitendo kama hicho, huwa tunapenda sana pesa lakini ni mind game tu pesa si kitu tunahitaji ndo maana tukizipata tunazibadilisha na vitu tunavyohitaji lakini si vyote pesa inaweza kununua.
 
Back
Top Bottom