Steven Wassira kaumbuka Igunga

hahaha Tyson kiboko na hisi huyo mwananchi angekuwa karibu angeweza hata kuzabwa kofi.CCM hawana sera zaidi ya kuibia watu kura kwa rushwa ya kutoa Tshirt na kofia .Maendeleo hawana sera za kuelezea .Siasa za uchwara zipo ccm
 
Wakati unasubiri majibu ya maswali yako ni vizuri kukumbuka kwamba watekelezaji wa sheria ndio hao hao wanaoivunja, sasa usitegemee wassira kuwajibika ama kuwajibishwa kwakuwa amekwenda igunga kujaribu kukinusuru chama kilichompa ulaji serikalini kisivuliwe nguo.

Labda tukishakuwa na katiba mpya tutalazimika kuzingatia maswali yako na kuyawekea sheria kali na wasimamizi makini wa hizo sheria.

haya....lakini walau basi wapinzani (aka chadema maana cuf ni "wachumba wa watu") wakomae kum-nullify contenstant was ccm!!
tuwe na pa kuanzia jamani...why??
 
Mimi nilianza kushangaa pale Ndugu Wasira (TYSON) alipopewa wizara mpya ya mahusiano. Mtu ambaye hana diplomasia hata tone na hajui kujenga hoja anakuwa waziri ambaye kimsingi anatakiwa kusuluhisha mambo.
 
Mbona sijaona kitu chochote kinachoonesha kuwa Wassira ameumbuka?
<br />
<br />
...uwezi ona kwani sio wote wenye macho wanaoona,na kwakuwa akili yako imefunikwa magamba ndo kabisa ata kuelewa inakuwia vigumu...JARIBU KUANGALIA KWA KUTUMIA AKILI KAMA UNAZO JAPO KIDOGO!...
 
Huyu sokwe yeye kazoea kulala mjengoni tuu... amejikanyaga kanyga tuu.... hamna lolote....
 
siku hizi kwenye mikutano ya kampeni maswali yanaruhusiwa?so far so good ccm wako hoii na hii ya watumishi wa umma kama wassira (waziri) kwenda kufanya kazi za siasa badala ya kutumikia wananchi ni uchuro nao
 
Asante sana umenipa raha..
You are on the extreme side of blindly indoctrinated followers of CCM and remain assured you will be the last person to meet and interact with truth. The day when CDM reality will count in your brain it will be the end of your world of reality and false doctrines of people like u.
 
Jamani hii nchi yetu ni ya ajabu sana, kwani watu kama akina Steven Wasira hawana kabisa uwezo wa kuwa viongozi. Hapa kwa kweli ndipo tatizo kama taifa linatukumba. Hivi kwani hawa akina wasira type wamefikaje huku? Lakini nimepata jibu wakuu, hawa jamaa huwa wanafika hapo walipo kiujanja ujanja.

Sasa hapa unapata picha ya kuwa katika hii serikali ya CCM, kweli kuna shida kubwa sana ya kiuongozi. Hapa kweli ni lazima nchi iyumbe kwa kuwa haina viongozi sahihi wa kutufikisha tunapotaka sisi watanzania. Hivi kiongozi kama Wasira unategeme upate nini kwake. Huyu mzee huwa kwanza hapendi changamoto katika maisha yake. Halafu huwa ni kilaza sana kwa muono wa nini serikali inataka aitendee. Huwa anataka sana serikali imtendee makubwa. Wasira na wenzako jamani imetosha kwa nini msikae pembeni muwaachie na wengine ?

Kama mtanzania na mzalendo kwa nchi yangu napaza sauti kuu kwamba sasa imetosha achieni madaraka kwa vijana wachape kazi na ninyi wazee hasa wasio na busara kama Wasira mkae kando mtuangalie,tukikosea waturekebishe wazee wenye busara na si akina wasira(mlalaji wa akili na mwili).

Wazee wa type kama ya wasira hawana jipya bali huwa wanapenda tu ukubwa na kujiachia kwenye makandoro(land crueser VX au GX) ambayo yananunuliwa na walipa kodi wa tanzania.

Mungu ibariki tanzania na pia mungu uwalaani aina ya viongozi kama akina wasira.
 
watz wameshaamka wanakumbuka shuka kumekucha ccm hawana chao
Nimeamini kiswahili kigumu, heri elimu iendelee kwa kidhungu!!!
1. Watz wameshaamka,
2. wanakumbuka shuka kumekucha,
3. ccm hawana chao!

dah!
 
CCM wana wakati mgumu sana kujibu hotuba ya Rostam. Wassira anafikiri Watz wa 1990 ndo wa 2011. Anakosea sana. Huko nyuma walitumia uelewa mdogo wa wananchi kama mtaji wa kushinda na hata kutumia mabavu bila kujali demokrasia. Inasikitisha sana maana Wassira anasema ameenda Igunga kujibu hoja za chama siyo za Rostam. Huku ni kuchanganyikiwa. Ila pia siyo tatizo lake maana nao uzee tatizo na sijui kama Rais aliliona hilo au anagawa tu uwaziri. Vijana wako wengi na wenye mawazo mapya na ya kujenga. Shida ya CCM ukishakuwa na nafasi mpaka ufie hapo sasa sijui kama hiyo nayo ni sera ya chama au la.

Mungu huwa hamfichi mnafiki atawaumbua mmoja mmoja. Tunawaomba sana wananchi wa Igunga waamue kwa utashi wao na si vinginevyo kwani maendeleo si kwa ajili ya chama,mbunge au kada yeyote bali kwa ajili yao wenyewe.

Kuna wengine wanasema Mwl ataweza nini kuongoza hana elimu. Sijui kama watu wa CCM walimsikia "Rais wao" alipokuwa anateua mawaziri mwaka 2005. Kikwete alisema hivi "Uwaziri hausomewi ". Lakini Katiba yetu Ibara ya inasema hivi
67.-(1) Bila ya kuathiri masharti yaliyomo katika ibara hii, mtu yeyote atakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwa kuwa Mbunge endapo-
(a) ni raia wa Jamhuri ya Muungano aliyetimiza umri wa miaka ishirini na moja, na ambaye anajua kusoma na kuandika katika Kiswahili au Kiingereza;
(b) ni mwanachama na ni mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa. Kwa hiyo kwa wagombea wote waliopendekezwa na vyama vyao wanazo sifa hizi (a) na (b). Kinachohitaji hapa ni UTASHI, UTHUBUTU na UADILIFU katika utendaji.

Wana-Igunga Mungu awatie nguvu, awape ufahamu, busara na hekima katika kufanya maamuzi sahihi

Naomba kuwasilisha
 
Nawasifu ccm kwa uwezo wao wa kujibu maswali magumu kirahisi....
 
CCM ni mambumbu wa kusoma alama za nyakati siku zote,Wasira alikuwa anafikiri anaongea na mahawara wake pale.Huyu mzee anatakiwa kujiuzulu hana analofanya zaidi ya kuropoka na kutumia nguvu mahali panapohitaji kujibu hoja kwa akili
 
khaa hawa CCm wanachezea muda na pesa za walipa kodi huyu wassira muda wa kukaa ofisini kama waziri anaenda kwenye kampeni???

Mkuu umeuliza swali la msingi sana, hivi huyu jamaa amechukua Likizo Ofisini au kajiondokea tu, na kama amechukua likizo kaaga anaenda wapi? Je ni likizo bila malipo? kwa sababu wote tunamwona Igunga. Hawa watu wanafanya shughuli binafsi mtaani then mwisho wa mwezi wanalamba kodi zetu, natumai katiba mpya itaangalia hili.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom