gogo la shamba
JF-Expert Member
- Mar 1, 2013
- 6,669
- 2,165
kama wana ccm mpaka sasa wanabisha kwamba Mwangosi hakuuwawa na polisi wanasema aliuwawa na chadema,hayo usemayo si rahisi kuyakubali na kuyaamini
Bwana Steven Masatu Wassira waziri katika serikali ya rais Kikwete anajinasibu kama mtu ambaye hana kashfa, nataka kumkumbusha baadhi ya mambo yake kwani nimesoma maojiano yake kwenye gazeti la dira ya mtanzania.
Mwaka 2006 Wasira akiwa waziri ama wa maji au wa kilimo alimpatia kijana wake anayeitwa KAMBARAGE zaidi ya sh bilioni 1 kwa ajili ya kununua dhahabu kutoka kwa wachimbaji wadogo wa Buhemba.
Kijana akajitosa kwenye bihashara lakini akakutana na upinzani mkubwa kwa hiyo ikabidi atafute washirika ambao ni wazoefu na wazaliwa wa Buhemba akajiunga na kijana mmoja aitwae ENOCE KAREGO huyu ni mzaliwa wa Buhemba kwa waliokwishafika Buhemba huyu bwana ndie anayemiliki ukumbi mkubwa unaoitwa KAREGO upo nyuma ya kituo cha polisi Buhemba.
Biashara ilianza vizuri na wakawatikisa wenzao kwani KAMBARAGE alikuwa anapeleka dhahabu hiyo Marekani bei yao ilikuwa nzuri hivyo wakateka soko, kama una jamaa Buhemba ulizia, ilipofika mwaka 2007 mshirika wa mtoto wa Wassira akaingiwa na tamaa baada ya KAMBARAGE kutoka Marekani alikuja na kiasi kikubwa cha fedha na kumkabidhi bwana ENOCE fahamu kuwa pesa ya kununulia dhahabu maeneo ya machimbo haiwekwi benk kutokana na mazingira ya manununzi.
ENOCE akaweka mazingira ya kuwa ametekwa na majambazi maeneo ya Sabasaba alfajiri wakati akimpelekea KAMBARAGE dhahabu aliyokuwa amenunua, ikapigwa yowe eneo ilo na kuanza kufatila kama wanaweza kuwapata majambazi hao.
Katika kufatilia kuna kijana mmoja mzaliwa wa Tanga aliuawa kwani alikuwa mgeni eneo hilo alikuwa amekuja kumsalimia dada yake alieolewa hapo, kwa hiyo yowe ilipopigwa nae alitoka majira ya saa 11 alfajiri alipokutana na wanayowe katika maojiano hawakuelewana kwa hiyo alipigwa hadi kufa, alikuja kutambuliwa baadae na shemeji yake alipokuja kutazama maiti.
Alipopewa taarifa mtoto wa Wassira alikuja Buhemba ili kupata taarifa kamili, ENOCE alimueleza kuwa alfajiri ya siku ya tukio akiwa anaendesha gari lake kuelekea Bunda walitokea watu wenye bunduki na kupiga risasi kioo cha mbele hivyo gari lilikosa mwlekeo na kwenda nje ya barabara, ndipo alipovamiwa na kunyanganywa dhahabu yote aliyokuwa anampelekea, KAMBARAGE alimtaarifu baba yake ambaye aliwasiliana na polisi ili wachunguze suala ilo.Taarifa ya polisi ilipinga madai ya ENOCE kuwa alitekwa na ikaonekena ni tukio la kupangwa.
Wassira alikuja Buhemba na ndege ndogo ya serikali na kutua katika mgodi wa Buhemba akaamuru askari wamkamate ENOCE apelekwe mgodini azungumze nae kweli baada ya nusu saa ENOCE alikuwa kwenye ndege akifanya mazungumzo na Wassira baada ya masaa 2 ENOCE alishuka na kuondoka na polisi ambapo alikuwa ameamriwa ndani ya wiki 1 awe amekabidhi dhahabu yote na pesa iliyokuwa imebaki kwa KAMBARAGE, ENOCE akufanya hivyo kwa hiyo baada ya wiki alikamatwa na kuswekwa ndani.
Amekaa magereza kwa zaidi ya miaka 2 mpaka ndugu zake walipochachamaa kuwa wataweka mambo yote hadharani ilikuwa inaelekea uchaguzi wa 2010 ndipo akaachiwa na kesi kufutwa.
Cha kujiuliza mwaka 2006 Wassira alitoa wapi zaidi ya sh bilioni 1 na kumpatia mwanae tena mmoja, hatujui wengine walipewa kiasi gani, ilo ni moja mengine yaja.
Hakuna ukweli wowote katika uzi huu, made from Ukawa
Hii ni habari ya kutunga
JE,INAWEZEKANA KITU KISAFI KITOKE KATIKA KITU KICHAFU ?!
dah! pasco mambo yako yako supa sana.
unaposema ni hela ya "kawaida sana" ni asilimia ngapi ya watanzania wanaweza ipata hiyo pesa kwa "chapcap"? ungesema hiyo pesa ni ya kawaida sana kwa "baadhi ya watu" labda ndio ingekuwa sawa.
Mkuu Nchi Yangu, asante kwa taarifa hii, TZS. 1B, ni hela ya kawaida sana!, labda kama una jingine!.
Pasco.
Mara mseme ni fisadi, mara ananukiwa na shombo ya samaki kwa ajili ya kujituma kutafuta pesa. Sasa tujue lipi machizi nyie?
Wewe Pasco umepandwa na wazimu kichwani hadi kuiita Bilion moja ni hela ya kawaida?
Billion 1 ni sawa na karibia Milion 1 US $ na kwa takwimu zao wenyewe USA ni chini ya 1% ya Wamarekani wote Taifa lenye nguvu zaidi ki uchumi duniani wenye Bilion 1 ya kitz bank!!
Lkn leo hii kapuku mwenzangu huyu anadiriki kuiita tsh Bilion 1 hela ya kawaida!Pasco kapimwe akili
Mleta mada kweli ni hayawani. Tshs 1 bilion unaona ni pesa nyingi sana?. Diamond Platinum ana 4 Bilion kwenye akaunti yake. Masanja mkandamizaji ana 8 Bilion, Kigwendu ana 5 bIlion, Wema Sepetu ana 1.5 Bilion sasa unashangaa kwa mtu kama Wasira kuwa na 1 Bilion?.
Wassira ana utajiri wa kurithi toka kwa wazazi wake. Ana mifugo na machimbo ya madini. Jamani acheni kuleta mada ambazo hazina kichwa wala miguu, Wassira kwa sababu ni mwanasiasa hawezi kuwa na pesa kama hiyo?
Nadhani anarejea kauli ya wabongo km Fisadi wa Bariadi akiita vijisent na Beparila BK anaita ya UGORO,,,!!
Billion moja ambayo ni Milion elfu 1 leo unaiita hela ya kawaida?Huyu Pasco vipi lkn?
Hamna sehemu duniani kwa exchange rate yyt ile wataiita hela itakayopatikana kwenye exchange hiyo kuwa ni ya kawaida
Ilete mshikaji make hili jamaa ukisoma maelezo yake linajifanya li safi kuliko Nyerere.Leta ya pembejeo.Ndiyo maana kwenye mchakato wa katiba hakuna lilichoongea zaidi ya kupinga ile ibara ya miiko ya uongozi.Wasira akijibu hii ajiandae na kujibu ufisadi alioufanya mfuko wa pembejeo mwaka 2008/2009.ntaileta.