Steven Kanumba's Death and Elizabeth Michael a.k.a Lulu's Involvement; The Guide at JF | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Steven Kanumba's Death and Elizabeth Michael a.k.a Lulu's Involvement; The Guide at JF

Discussion in 'Celebrities Forum' started by AshaDii, Apr 15, 2012.

 1. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #1
  Apr 15, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180

  Habari wana JF...


  Kifo cha Star maarufu katika Upande wa movies kwa Jina la Steven Kanumba umetikisha taifa kuliko ilivowahi dhaniwa; Nakubali Kanumba was good na wengine wengi wanadiriki kusema he was The Great. Kwa upande wangu nilikua namkubali kweli, sababu nilimuona alivoanza na alipofika. He was no one but was able to change that.... Na nilikua namkubali more because of the way amechangia ku evolve movie Industry nchini kuliko hata movie zake - nitakua ni Muongo nikisema I have watched more than three of his movies ila nilikua namkubali kama ninavokubali na wasanii wengine hapa nchini kwa michango yao katika entertainment Industry. I have been fortunate to meet him once, and I thot him to be so cool nikifananisha na baadhi ya Ma stars nilo wahi habatika kuwaona (Kwa mfano Hemedi; unaweza chafuka nyongo kwa kumsikiliza na kumtazama swagger zake).

  Kifo chake kilikua cha kushtua mno! Wapo ambao kweli kazikwa na tumeanza kusahau, Ila believe me you bado thousands of people wana majonzi hadi dakika hii ya hii thread na post hapa. Kuna watu hawawezi angalia movie wakamaliza; Kilio kinaanza upyaaa... Discussion of his death upya... Hadi leo hii huwezi pita mahala mbali mbali ukakosa sikia randomly akiongelewa. Katika Imani zetu za Kiswahili twaweza justify kwa kusema jamaa alikua na nyota kali sana ya kukubalika na kupendwa. Siamini kama sababu tu inasemekana alikua mcheshi na mkarimu ndio sababu pekee... I don't! Nimebahatika kuongea kwa karibu na moja wa mhudumu ambae alikua zamu siku Marehemu Kanumba alipelekwa hapo hospitali akiwa katika gari yake mwenyewe kapelekwa na huyo mdogo wake na kijana mwingine Pamoja na Mama mwenye nyumba wake. Unaambiwa ilipo tambulika kua Kanumba was indeed dead ni ndani ya mda mfupi watu walikuja kwa wingi toka kona mbali mbali ya jiji kutaka kuja hakikisha kama kweli huku wengi wakiwa hawaamini.

  Kama Marehemu kutajwa jina yaweza sababisha yeye kushindwa pumzika kwa AMANI - Basi Kanumba bado ana mda mrefu wa yeye kupumzika kwa AMANI hapa karibuni. Ingekua Marehem kafariki kwa njia hio hio kwa kupitia mkono wa Mwanamke mwingine; Kifo chake, jina lake na mijadala kuhusu tukio hilo la kusikitisha lingeanza kupoa sasa. Bahati mbaya saana kwa jinsi mambo yanavoenda ndio kwanza kama ni hadithi badi tupo stage ya Climax.... Na mwisho wake hautabiriki hata kwa wale ambao husoma hadithi zaidi ya 50 kwa mwaka. It is so complicated! For the simple reason kua Mhusika Mkuu katika hilo tukio ni the Late Kanumba na Elizabeth Michael alternatevly known as Lulu.

  Utata wa muelekeo wa hii habari nzima ya kusikitisha wa Uhusika wa Lulu unakuja tokana na sababu nyiingi....
  Hii yoote inatokana na mhusika kua mtoto/binti mdogo sana ki umri.... binti ambae yeye Marehemu kamuona na twaweza sema mlea toka utoto hadi kupevuka na kua binti. Lakini zaidi sababu ambazo zina nguvu sana ni yeye Lulu alizo zijenga mwenyewe katika macho ya Jamii. Kwamba yeye ni yeye, akiongea katika vyombo vya habari mara nyingi huwa kwa kejeli na kujidai... ni binti ambae katika macho ya tulio wengi twaona ni kama kashindikana. Na yeye alikua akiona ni sifa (I presume) kuandikwa na vyombo vya habari kila siku.... Ana maneno mengi ambayo yanam paint vibaya kama binti. Ingekua huyo huyo Lulu ni binti ambae katika jamii aonekana ni mpole, mstaarabu, adabu na heshima na kutokua na Kashfa; Kitendo cha Marehemu kufariki kusinge mkandamiza saana katika jamii. Jamii ingeuliza maswali kama Jamani Kanumba alikua akifanya nini na yule binti? Yule si mdogo wake? na maneno yafananayo na hayo.

  Yule mtoto ana mtihani mkubwa.... Roho yaniuma. Nime observe asilimia zaidi ya 75 yanamlaumu kua ndio chanzo cha kifo cha Steven Kanumba kana kwamba kamuua... Hao watu wakisahau kua huyo binti hajawahi pewa chance ya kukua katika normal child environment based... toka mtoto kazungukwa na mastar, starehe, pesa, wanaume wenye tamaa na wale ambao wapo tayari kumpa lolote ili kuwez mpata.... Wakisahau kua ni mdogo akili haijakomaa. Kama mkubwa tu akipata anakua limbukeni sembuse yeye?

  Sijui ataishi maisha gani? sijui kama ana mfadhili wa kumpleka nje akitoka tu... (amini nakwambia yule binti hawezi pita mtaani popote pale Tanzania); Na vile bado ni mdogo... hata akiachiwa huru anatakiwa uangalizi wa 24/7... Kwa maisha alozoea kuishi ya Kujiachia.... na hali atakua mfungwa hata akiachiwa huru; itakua mtihani mkubwa sana kwake kiasi kwamba aweza hata taka poteza maisha yake mwenyewe.... Hata hivo tuone upepo utavoenda.


  Nawapa pole Wazazi, Ndugu/Jamaa, Wasanii wote, Wafanyakazi wake na Watanzania wote waloguswa na Kifo cha Marehem Steven Kanumba. May he Rest In Peace.

  Nampa pole sana binti Elizabeth Michael kwa doa la maisha lililomkuta; ni kitu ambacho kingeweza mkuta yeyote yule. But in this it is her. Pole zake saana na I pray for her.... Nawapa pole wazazi wake na watu wake wa karibu wote ambao wameguswa na kuumizwa kwa kuhusika kwake katika tukio.


  Lengo la hii thread ni kutengeneza kumbu kumbu ya Thread zote ambazo zimeguza hilo tukio La kusikitisha. Kwa wale ambao ni members hawapo, kwa wale ambao watakuja kua members, kwa wale ambao watataka kujikumbushia ama kusoama yote kuhusiana na shughuli nzima waweze pata kwa urahisi badala ya kutafuta randomly. Threads zipo nyingi sana hivo nimejaribu chukua baadhi ya Msingi. Kuna nyingine sijaziona Nitaomba fellow members wajaribu kuweka Links katika posts na nita update.


  Tanzanian actor Steven Kanumba reported Dead - Courtesy of Jeryson

  Steven Kanumba; Has a very touching story - Courtesy ya Pasco

  Madaktari; Hiki ndicho Kilicho muua Kanumba - Courtesy ya Matola

  Wabunge Halima Mdee na Easter Bulaya wamefurahi Kanumba Kufa? - Courtesy ya Kamura

  TBC1 Wakata matangazo bungeni, wanarusha mazishi ya Kanumba Live - Cortesy ya Wakusoma

  Kanumba frustrates JK's Travel Plans - Courtesy of Sijali

  Ya Kanumba: Konzo ya Maji Haifumbatiki na mvumbika changa hula mbovu - Cortesy ya Babykailama

  Maisha Kitendawili.... Wengi hufa bila kutegua - Courtesy ya The Boss

  Kifo Cha Kanumba: Ni uzembe tu! Sio Lulu - Courtesy ya Pasco

  Kifo cha Steven Kanumba na hatma ya Elizabeth Michael - Courtesy ya Maseto


  Africa Magharibi bado utata, wadhani Kanumba kagongwa na gari - Courtesy ya Misnomer

  Speculations behind Kanumba's Death - Courtesy ya Jack Beur

  Nyimbo ya Kanumba kabla hajafa ni kama amejitabiria - Cortesy of Hassbaby

  Neno la mwisho la Kanumba kwa Mama - Courtesy of Independent Voter

  Bungeni Leo; Martha Mlata: Kanumba alitakiwa awe na body guard - Courtesy of Dadio

  Filamu ya Kifo cha Kanumba yanaswa kwa siri - Courtesy ya Gumzo

  Mod tunaomba utengeneze Jukwaa la Kanumba kuepusha Duplicant - Cortesy of Matope (Lmao hapa)

  Kifo cha Kanumba chazua Ushirikina - Courtesy ya Maseto

  Kifo cha Kanumba: Wengi kupandishwa Kizimbani - Courtesy ya Allien

  Kufa Kufaana; Wasanii Bongo Movies Waanza kuchangisha Pesa - Courtesy ya Ma2mbo

  Michango ya Rambi Rambi ya Msiba wa Kanumba watafunwa - Courtesy ya Kimbunga

  Kanumba; Holly wood nao walonga - Courtesy ya Alien

  Steve Kanumba: Historia; Kazi zake na Mengineyo - Courtesy of Allien

  "Nimezaa na Kanumba' - Courtesy of Ngoshwe

  Ramli kali.. Nyuma ya pazia kifo cha Kanumba - Courtesy of Bujibuji

  Umaarufu wa Kanumba unanitia mashaka - Courtesy of PETER JOHN MLEY


  [Lulu Related Thread to the Death of Kanumba]
  ...........................


  "Ujinai" wa Lulu katika "Mauaji" ya Kanumba (R.I.P)- Courtesy of Woman of Substance

  Tetesi-UTETEZI WA LULU: Kanumba alitaka kunibaka - Courtesy ya Rutashubanyuma

  Je Lulu ana haki juu ya Kifo cha Kanumba? - Courtesy ya MPAMBANAJI.COM

  Sakata la Lulu na Kifo cha Kanumba, What does the Law say? - Courtesy ya Majamba Jr.

  Police wamuachie Lulu mara moja! - Courtesy of Rutashubanyuma

  Ushauri alopewa Lulu na Lady Jaydee 2009 akiwa 14yrs - Courtesy of Independent Voter

  Mh. Halima Mdee: Nitamsaidia Lulu kadri niwezavo - Courtesy of Mwitaz

  Neno la Leo: Jamii ya walo wema Imsamehe Elizabeth Michael - Courtesy of Majid

  Ushauri huu kwa Kanumba na Kifo chake - Courtesy of Kitalolo  The above ndio threads ambazo nimejitahidi ku compile. DISCLAIMER; Nimeweka threads tokana na uhusiano wake na the whole event. Kuweka kwangu hapa sio kwamba all details katika all threads ni valid and verified.


  Pamoja Saana.

  AshaDii...
   
 2. A

  Ave Ave Maria JF-Expert Member

  #2
  Apr 15, 2012
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 10,757
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 0
  Dah.....umenirahisishia maana kuna threads ambazo nilikuwa sijaziona!
   
 3. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #3
  Apr 15, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Duu hii siredi imekua sticky??? Mods ni nomaaaaaaa,mbona yale yaleeeeeeee?
   
 4. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #4
  Apr 15, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180

  King Kong... Nilituma speacial Request kwa Mods... Hii issue bado itaendelea kufuatiliwa hadi pale hatma ya Lulu itapojulikana. Hivo niliomba for the benefit ya wale ambao hawana mda mwingi wa kupitia threads katika forums mbali mbali hivo taarifa nyingine kuwapita. Of coz it won't be a sticky forever.....

  BTW Ndio yale yalee yepi hayo?
   
 5. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #5
  Apr 15, 2012
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,618
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Thank you so much for the initiative, imerahisisha sana kutafuta threads zenye kuhusiana na saga hii.
  I think it should be in Habari na Hoja Mchanganyiko because it has been discussed from so many angles.
  What say you?
   
 6. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #6
  Apr 15, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180

  Alter mie sielewi.... Ilikua habari na hoja mchanganyiko na I thot nimekosea nikaomba ihamishwe.... So far ilikua Celebrities Forum na sasa ipo hapa Entertainment... Mimi I really don't mind ipo wapi as long as people can access it.
   
 7. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #7
  Apr 15, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,809
  Likes Received: 1,128
  Trophy Points: 280
  Kazi kwa wapenzi wa tufilamu imerahisishwa.
   
 8. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #8
  Apr 15, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,966
  Likes Received: 1,857
  Trophy Points: 280
  Ashadii hii thread ni nzuri na umekuwa muwazi sana kwani hujashabikia bali umetoa blacks and white. me too nakukubali kwa hilo ma dia
   
 9. Yummy

  Yummy JF-Expert Member

  #9
  Apr 15, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 1,801
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  AshaDii mi iko penda wewe sanaaaa....nashukuru kwa kazi nzuri.
   
 10. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #10
  Apr 15, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Ashadi mie jana nimekiri kwa kinywa kuwa kweli kumbe Kanumba ametutoka na machozi kuanza kunitoka bila ajizi.sikuwa mpenzi wa movie zake ingawa siku za karibuni niliangalia Uncle JJ,Big Daddy and The Young B...
  yaani hata sielewi ni nini hiki?
  RIP Steven Kanumba- hakuna aliye msafi na kwa Neema ya Mungu uturehemu
  I will always miss u
   
 11. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #11
  Apr 15, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hata mimi nilitaka kumuuliza ndiyo yale yale yepi tena?
   
 12. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #12
  Apr 15, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  I am humbled kwa acknoledgements Zoote....

  @ Yummy mimi penda wewe pia, Nimefurahi kwa kunijulisha hilo.... THANK U.
   
 13. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #13
  Apr 15, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180

  I know what you mean dear.... Mimi naomba nikiri toka habari zake za kifo, hadi mazishi hadi yoote yalotokea; Hakun a mahala niliweza ongea na mtu kuliongelea tukio... Nilikua msikilizaji tu! Hakuna hata post moja niliweza elezea kuhususiana na topics related to the event.... Niliona it was too depressing. Naona thou sio kwamba nilikua nampenda kivilee.... Imeniuma sana. Na more Imeniuma hatma ya Lulu.... I wish I had access to that kid kwa kumuona tu kuona yupo vipi na the way anategemea maisha yatakua..... Ananiuma mno. Wote yeye na Kanumba.

  I concur.... Rest In Peace Kanumba.
   
 14. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #14
  Apr 15, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180

  Losambo binadamu ni kazi saana. Tumetofautiana kufikiria.... Yeye kaona tu kua ni thread ya Kanumba bila kuangalia beyond... Kwamba imenichukua a lot of my time kutafuta hizo threads ili nisome yalonipita wakati sipo... Huku nikifanya hivo nikaona ni kazi kubwa mno ambayo sio lazima member mwingine apitie kuweza soma threads zote; hivo azikute pamoja in a single thread.... We have a long way to go....

  Ngoja tumsubiri atueleweshe yale yale yepi.....
   
 15. Yummy

  Yummy JF-Expert Member

  #15
  Apr 15, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 1,801
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Sana aisee na kwa kuwa umeshalitambua hilo inabidi umpotezee tu. Binafsi nimependa jinsi ulivyoelezea hauko upande wowote umeelezea vizuri sana kwa pande zote mbili though watu tunajiuliza maswali mengi sana kuhusiana na huyo Lulu(ametuchanganya,hasa kwenye swala la umri.....naona ataendelea kutuchanganya zaidi tu huko mbele). Mimi sio mshabiki wa mastar wetu hapa kwanza huwa nasikia kizungu mkuti nikisia neno star.....lol ila kifo cha Kanumba kimenigusa yaani nimeona huruma inshort vifo vyote vya ghafla huwa vinanihuzunisha sana nakosa raha hata wiki nzima hata kama simfahamu muhusika. Huyo Lulu nilikua namsikia tu kwa wadada wa kazi ndio nimekuja kumuona picha zake kwenye hii habari ya Kanumba,ni kazuriii hakutakiwa kuingia kwenye hayo mambo bado mdogo sana. Nimechoka zaidi nilipoona picha kwa lady jay dee yani mbona mdogo sana kwa hayo mambo anayoyafanya?!
   
 16. 124 Ali

  124 Ali JF-Expert Member

  #16
  Apr 16, 2012
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 5,705
  Likes Received: 2,388
  Trophy Points: 280
  AshaDii nafikiri tuendelee na ishu zetu jammaa keshajistukia kuwa yuko peke yake ,unafikiri atarudi kuja kufafanua hiyo 'yale yale' yake? na akifanya hivyo nitatafuna buttons za keyboard zote nakuapia!
   
 17. J

  John W. Mlacha Verified User

  #17
  Apr 16, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 3,515
  Likes Received: 540
  Trophy Points: 280
  ashadii we mkali ..nakupenda sana na ubarikiwe
   
 18. BPM

  BPM JF-Expert Member

  #18
  Apr 16, 2012
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,766
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  AD kwa kweli hadi sasa huyo bint anahitaji ushauri mkubwa sana na pia watu wanatakiwa waelewe na kukubaliana na yote yaliyotokea kama sehemu ya maisha.. ni kweli yule bint ananyooshewa sana vidole na hii imechangiwa sana na umaarufu wa kununu na hata ulimbukeni

  lakin pia tumeona nini kinaendelea nyuma ya pazia kwenye tasnia ya filamu na nadhani sehemu zote
   
 19. queenkami

  queenkami JF-Expert Member

  #19
  Apr 27, 2012
  Joined: Feb 8, 2010
  Messages: 1,340
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  AshaDii napenda na kushukuru sana jinsi unavyojitolea kurahisiha mambo pale unapoona watu wanahangaika.
  Nakumbuka ulifanya pia kwenye msiba wa Regia.
  Kanumba aliniuma niliposikia amefariki,ilikua ghafla na mapema mno ila sasa nimeshakubali kuwa hayupo,nimeshaanza kumsahau Kanumba ila Lulu ndio kwa sasa ametawala mawazo yangu,japo kalikua kamapepe lakini hana tofauti na wadogo zetu wengi wa siku hizi ambao wana mambo makubwa wangali wadogo lakini kwa vile ni ndugu zetu kamwe hatuwaombei yawapate yaliyompata LULU.Picha za juzi akilia zimeniumiza sana,namuonea huruma ningekua na jinsi ninemchomoa ktk hali aliyoko sasa ila sina zaidi ya kumuombea kwa Mungu amvushe na kumpatia faraja tena.Japo upelelezi bado unaendelea lkn akili yangu inanilazimisha kuamini kuwa mtoto wa watu hana hatia.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 20. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #20
  May 21, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,105
  Likes Received: 6,577
  Trophy Points: 280
  Nimeiona hii leo,
  tena nimeanza kulia upya,
  sikumjua huyu kijana,
  lakini hata leo nina password moja natumia
  jina lake, sijui niibadili au niiache sijui.

  Asante AshaDii, kweli wewe ni msomi.
   
Loading...