Frank Wanjiru
Platinum Member
- Apr 12, 2012
- 25,598
- 46,633
Habari ya ukweli kabisa
Na Mmiliki wa cave Disco.
The sound of Serengeti
Anaanza Kwa kusema
Mimi nilikuwa nafanya kazi AICC kama Director of Conferences and Marketing, na wakati huo naendesha Disco hapo New Safari Hotel, The Cave, ambayo ilikuwa basement ya hotel na bendi yangu ya The Sounds of Serengeti (Jamani Buzi Langu) iliyokuwa inapiga Equator Hotel.
Mdau wangu mkubwa wa muziki alikuwa Hidaya, na tulimpa membership ya Club na Band, bure.
Dj wangu akiitwa MacHope Davis Junior, the Young Millionaire a.k.a. Tumaini Mzeru (marehemu) toka Matombo Msalabani, Morogoro.
Lakini nikienda Dar nakunywa kwa rafiki yangu Charles Mbandwa, kwenye joint yake ya Guys & Girls, Bagamoyo Road, karibu kwa Batengas hse.
Tukawa marafiki sana na alikuwa na hela kutokana na biashara yake ya Clearing and Forwarding.
Alikuwa akija Arusha na kufikia nyumbani kwangu na baadaye tunakwenda Nairobi kucheza miziki ya Seaman's Club, opposite na 680 Hotel.
Siku moja akaniambia anamleta Pepe na bendi yake na anaomba niwe mwenyeji wao Arusha.
Na kweli walifikia nyumba yangu ya AICC No. 52 Serengeti Rd, Corridor Area pamoja na akina Emolo na wanenguaji.
Mimi nilikuwa sina mke wala watoto pale mjengoni , wenye Bedroon 5 Master na Bedroom 3 za Servant quater.
Tulipiga muziki Hotel 77, Namanga na Merererani.
Lakini wakiwa kwangu nilimwomba Hidaya, aliyekuwa bingwa wa Misosi ya kiswahili Kaloleni na Arusha, anisaidie kuupikia ugeni huu.
Lakini baada ya siku 4 Pepe akahamia kwa Hidaya mpaka tour ilivyokwisha, na wakaondoka kwenda kupiga Mbeya kwa mkwe wa Mbandwa.
Hidaya akabaki.
Miezi miwili baadaye nikaletewa CD 2 kupitia ubalozi wa Zaire nchini za wimbo wa Hidaya.
Nikamwomba DJ wangu Ijumaa ahakikishe Hidaya atakuwepo. Hakujua kwa nini, Ila tulipopiga muziki huo Hidaya alitaka kuzimia na sisi tukamkabidhi CD copy yake, na tukalewa mpaka asubuhi, courtesy ya wadau wa muziki Arusha.
Bahati mbaya Hidaya ameshakufa, ila mbaya zaidi ni kifo cha mtoto wake wa kike aliyeuawa na mme ambaye yeye alimleta kuja kuishi naye London...
Cave Disco, Safari Hotel
Nilivyoanzisha Disco Cave hapo New Safari Hotel ikabidi kumtafuta Dj wa nguvu.
Vyombo vya Disco, mimi na John Manyama, promoter wa Athlets, hasa wa mbio ndefu, vilinunuliwa ulaya kutokana na awards za akina Nyambui na Shahanga.
Na tukaunda kampuni ya Dawnbreakers - wanaowahi mapambazuko.
Dj Marck Hope
Katika utafiti nikaambiwa kuna kijana mdogo anafanya kazi Msajili wa Majumba Dar kama Plumber, lakini ni Dj mzuri vilevile na anapiga bar za Nyani na Ngedere na Nyika na Vome huko Temeke
Tulimtafuta tukampata na kumhamishia Arusha.
Ingawa ilikuwa kazi kubwa ila tulivyomwahidi kuwa ataishi New Safari Hotel, akakubali.
Alifika KIA amevaa pensi na fulana nyeupe ya kuchezea Lawn Tennis na Racket yake bila mzigo wowote.
Na kweli haikuchukua muda akashika soko la Disco Arusha lililokuwa linashikiliwa na Ali Manyege,
New Arusha Hotel na Mallya hapo Arusha by Night, hoteli ya Mzee Ulotu , ambako siku hizi imegeuzwa Hospitali.
Kwa kuwa mimi nilikuwa nasafiri sana ulaya hasa Brussels nilikuwa naleta latest za Congo kutoka Gallerie de Excelles - Quartier ya Matonge, ambako kulikuwa na studio nyingi zikitoa nyimbo za Wacongo.
Tukawa popular sana hadi wapenzi wa muziki toka Nairobi, pamoja na huyu Kenyatta, wakawa wateja wetu wakuu.
MacHope alifariki mwanzoni mwa miaka ya 90 na nikaenda kumzika Mikese, Morogoro.
Pichani ni Hidaya, dj Mack Hope na leyla