Steve Nyerere: Sing'oki kihuni, kikao chao ni kinyume na Katiba. Nampa Mbunge saa 48 aombe radhi

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,462
Steve Nyerere anazungumza na waandishi wa habari leo Jumanne Machi 22, 2022

“Nawashukuru wasanii wenzangu na Watanzania wote kwa mchakato ambao ulikuwa unaendelea na bado utaendelea.

“Muungano na ushirikiano wetu ndiyo utatutoa na kutufikisha mbali, kama tukishikamana tukatoa mioyo yetu chuki tutapiga hatua mbele…

"Mwaka 1992 wakati mwalimu Nyerere aliporuhusu upigwaji kura wa taifa kuingia kwenye vyama vingi au kubaki na mfumo mmoja, baada ya kura wale waliopiga kura asilimia 20 ndiyo waliopewa nafasi kwa kuwa aliona mbali.

"Sijawahi kwenda kuomba kazi Shirikisho, Bodi na uongozi na Rais ndiyo walikuwa wakinifuatilia na wao ndiyo walioniambia mimi, nikakataa kwa kuwa nimeishi maisha ya muziki na sinema ninajua.

"Walinifuata mara mbili nikakataa, ya tatu walimtumia rafiki yangu ambaye wanajua aniweza, ndipo nikakubali lakini mkumbuke sikuomba kazi.

"Kazi ya usemaji ni kutumwa siendi kuzungumza ya kwangu, kazi yangu ni kupewa na kuboresha kidogo kisha ndiyo nayazungumza, pia mkumbuke kazi hii haina mshahara.

"Shirikisho hili siyo jambo la kitoto, kuna matatizo mengi, mfano Muziki wa Dansi kuna matatizo mengi. Bongo Fleva ilipata bahati, Rais Kikwete aliwahi kusema anaupenda muziki huo, sasa hivi Taarab imepata bahati Rais Samia anapenda Taarabu, lakini Taarabu yenyewe iko wapi?

"Yaliyoongelewa jana ni maoni, maoni yanapokelewa. Nilimshangaa Mbunge yule, cha kwanza alichotakiwa ni kuwaunganisha watu siyo kuwagawa watu.

"Mbunge anazungumza kugawa watu 'Hatumtaki huyu, kama huyo wanamtaka Dansi wamchukue wao'. Huyo mbunge hatufai.

"Wabunge wa Darasa la Sba ndiyo wanaofanya vizuri kuliko wewe msomi, usisahau ulipotoka, mshindi wa sita ndiyo unakuja kuliongoza Jimbo, hatutaki ubunge wa vimemo, hii ni awamu ya sita.

"Binadamu akisahau unatakiwa kumkumbusha, yeye aliwahi kusema yeye ni 'Mtoto wa baba, mama hamjui'.

"Ukiangalia wale wote wanaonipinga mfano Nay wa Mitego ni Chadema, yule mwingine ni ACT, yule mwingine ni CUF unadhani watanikubali, sikutaka kuingiza uchama.

"Kikao kilichofanyika jana kimevunja katiba, Shirikisho wanachama wake ni vyama siyo watu wanamuziki binafsi, walivyokuwa wakiongea walikuwa wakijifurahisha tu.

"Sisi wengine ilikuwa ni kwa ajili ya kuhamasisha. Walitakiwa wapeleke malalamiko yao kwenye vyama vyao, na je ni wanachama? Siyo kwa kuwa ni mwanamuziki basi unakenua domo.

"Nikiwauliza hapa CEO wa Simba amecheza mpira? Waziri Ummy Mwalimu ni Dokta? Ritha Poulsen ni msanii?

"Mimi niliamini kikao kile kama kimeongozana na mtu ambaye ana nguvu, maana yeye ni Mbunge na katika Jimbo lake kuna wasanii wa Taarab, Dansi.

"Mimi siwezi kung'oka kwa saa 48, siwezi kung'oka kihunihuni. Masaa 48 ya nini?

"Tuna matatizo mengi, mfano bima za afya, studio, mirabaha... vitu kama hivyo ndivyo vya kukaa na kuzungumza.

"Nazungumza kama Msemaji wa Shirikisho Tanzania, hatoki mtu hapa, napongeza BASATA kwa kuandaa tuzo, tulitakiwa tukae tujiulize vitu kama tuzo tuwashirikishe Wazanzibar, siyo mambo kama yake, poor kabisa.

"Nilitegemea nguli kama wale waniite waniulize mipango yangu.

"Nitajiuzulu kama Mwenyekiti, Bodi na uongozi wataniita kama walivyonifuata na kuniambia kuhusu hilo. Jana nilipata misukosuko kutoka kwa watu wangu wa karibu kuhusu hili.

"Nimewaambia ndugu zangu kuwa SITOKI, tukianza kuulizana hapa nasi tutaanza kuuliza alishinda?

"Niwaombe radhi wanamuziki wa Dansi, jana walidhalilishwa sana, watu wanajiona wenyewe ndiyo wenyewe, wakati wengine mmewapokea nyinyi

"Wamekosa nidhamu ya kukaa chini na kuzungumza, wakati nyie mliwapokea na wengine wakiomba watumbuize jukwaani.

"Unamuita Katibu wako Rasta, huu ni ukosefu wa nidhamu.

"Nampa masaa 48 awaombe radhi Bongo Fleva, amuombe radhi kiongozi aliyemuita Zumaridi, amuombe radhi Steve Ake, Aombe radhi kwa Taarabu na aombe radhi kwa Shirikisho la Muziki. Nitashangaa uongozi wa Shirikisho kama hawatachukua hatua.

"Kama wangekuwa wanashiriki katika vikao, mimi nisingekuwa Msemaji, wao ndiyo wangekuwa wasemaji, lakini hawashiriki vikao.

"Ubunge una mwisho, muda wa vikaratasi 'namtaka huyo' umepita.

"Sijaanza kazi wanapuyanga, je nikianza kazi? Hata ofisi sijakabidhiwa na sijui iko wapi.

"Muda ukifika nitaondoka, nipo tayari kujiuzulu lakini siyo kwa kuondoka na watu, nataka niwaache wakiwa na umoja.

"Kama mwanashirikisho una hoja ya msingi nenda kwenye chama chako ukatoe maoni yatafanyiwa kazi. Namalizia kwa kusema nampa Mbunge saa 48 aombe radhi kwa kauli zake, NIMEMALIZA SIHITAJI MASWALI."

Stevee.JPG
 
Wabunge wa Darasa la Sba ndiyo wanaofanya vizuri kuliko wewe msomi, usisahau ulipotoka, mshindi wa sita ndiyo unakuja kuliongoza Jimbo, hatutaki ubunge wa vimemo, hii ni awamu ya sita. Automatic Hii ni personal attack aliyofanya Steve Mengere Kwa Hamis MwiniJuma, nadhani yeye alipashwa adeal na Kile alichokizungumza MwanaFA na Sio Jinsi ya MwanaFA alivyopatikana Kuwa Mbunge.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anaongeatu kujifurahisha CCM haina ubavu wa kuwafanya bongo fleva kuwa kati ya maadui zao kwa sababu ya Stefu Nyerere.

Huyo Stefu kwa kumtazama lugha ya mwili muda si mrefu anajua atarudi kutangaza kujiuzulu. Hao bongo fleva wakitoka kwenye hilo shirikisho litakuwa tayari limekufa natural death. Veto ya shirikisho la muziki ni bongo fleva.

Kaihepa hoja ya shuleless kama ukoma. Mtu asiye jua mseamaji wa shirikisho ni taaluma yenye kigezo cha kielimu yaani ni pua, pua pua kabisa.
 
Wabunge wa Darasa la Sba ndiyo wanaofanya vizuri kuliko wewe msomi, usisahau ulipotoka, mshindi wa sita ndiyo unakuja kuliongoza Jimbo, hatutaki ubunge wa vimemo, hii ni awamu ya sita. Automatic Hii ni personal attack aliyofanya Steve Mengere Kwa Hamis MwiniJuma, nadhani yeye alipashwa adeal na Kile alichokizungumza MwanaFA na Sio Jinsi ya MwanaFA alivyopatikana Kuwa Mbunge.

Sent using Jamii Forums mobile app
Tunataifa la vijana wa hovyo sana

USSR
 
Mshindi wa sita ndiyo unakuja kuliongoza Jimbo, hatutaki ubunge wa vimemo, hii ni awamu ya sita.

Mshindi wa sita kwa kigezo cha kuhonga wajumbe anaweza kuwa ndiye wa kwanza kwenye fair practice za kiuchaguzi. Mh Rais mwenyewe kakiri hadharani jana akipokea ripoti ya tume. Kwamba rushwa iko kwenye siasa na chaguzi Tanzania. Vimemo ni mfumo upo ambao hakuna awamu itaukwepa. Sitashangaa hata yeye Stefu nafasi ya usemaji alipata kwa kimemo. Nguvu inayotumika kumtetea pengine inadhihirisha hilo.

Kajitahidi kuongea sana huku akionesha hiyo pete yake ya ndoa kwamba ni family man. Ajue nguvu ya pete bila vyeti ni useless. Usemaji ni taaluma ya habari inayosomewa darasani, hivyo tu. Bongo fleva wanamtaka aoneshe vyeti vyake vya darasani si pete maana wao wanayo mpaka macheni ya mafuvu shingoni
 
Steve Nyerere ametoa tamko rasmi kujibu kikao cha wanamuziki kilichofanyika 21/03/2022 kilichowakutanisha Shirikisho la Muziki Tanzania na Wanamuziki wa miondoko mbalimbali. Katika kikao hicho wasanii wengi walilipa Shirikisho la Muziki Tanzania kumuondoa Steve Nyerere katika nafasi ya Msemaji Mkuu. Leo hii 22/03/2022 Steve Nyerere amewajibu wasanii wanaotaka ang'oke katika nafasi kama ilivyonukuliwa hapo chini

"Kikao kilichofanyika jana kimevunja katiba. Shirikisho wanachama wake ni vyama, sio individual musician [mwanamuziki mmoja mmoja]. Wanavyoongea hapa wanamuziki wanajifurhisha tu, walitakiwa kupeleka malalamiko kwenye vyama vyao."

"Mimi siwezi kung'ooka kihuni kuhuni tu eti umekuja, 'natoa saa 48,' poor. Sisi tunahitaji saa 48 za kufanya kazi. Hatuwezi [tasnia ya muziki] kugawanyishwa na mtu, labda nisiwepo duniani. Wale wooote yale maoni yao Shirikisho limeyachukua, mimi siwezi kung'oka kihunihuni eti kwa sababu Watu eti masaa 48, kamfanyie Bibi yako masaa 48 huko, eti uning'oe kihuni tu"

"Atakayeleta chokochoko za kutaka kutugawanyisha [Tasnia ya muziki], viherehere tupo, tutamgawana yeye."-

"Nitajiuzulu kama mwenyekiti, makamu mwenyekiti, bodi ya shirikisho watakaa kama walivyoni-approach [fuata] kuniletea barua, tukakaa vikao. Nitatoka hadharani kusema, hili ndugu zangu naachia ngazi."
 
Back
Top Bottom