Stendi kuu ya mkoa wa Kagera inahitaji marekebisho

instanbul

JF-Expert Member
Jun 26, 2016
11,359
14,087
Wakazi million tatu na laki mbili wanaoishi katika mkoa huu wa kagera hasa mji mkuu wake bukoba wanazidi kushangaa ukimya wa viongozi wa mkoa, wanasiasa, wasomi nk ambao hupita kila siku katika hii stendi (maana ipo katika barabara kuu iingiayo mjini) wanavyojikausha kama haiwahusu vile hiki kichochoro kinachoitwa stendi.

Toka mwaka 2008 mchakato wa ujenzi wa stendi ya bukoba ulianza na hatimae mwaka 2012 ujenzi wake kuanza eneo la kyakairabwa lililopo km 8 kutoka katika mji barabara ya Uganda.lakin migogoro ya wanasiasa na viongozi wa mji huu mkongwe ilisababisha ujenzi kusimama.

Kwa sababu uongozi wa mji yaani jimbo la bukoba ulikuwa chini ya CCM wananchi wakaamua kuibwaga na kuwaachia migogoro Yao.
Ndipo 2015 upinzani yaani chadema walichukua Jimbo yes walijitahidi wakaweka Hadi lami stendi ya kyakairabwa ingawa kwa kusuasua na walitaka kuamishia stendi kule but uongozi wa wilaya hukutaka stendi iamishiwe kule kwa sababu baadhi ya huduma kama jengo la wasafiri lilikuwa bado na ishu ni nyingine ni siasa za mwendazake kuacha majimbo ya upinzani refer kawe na kibamba kwa Dar.

2020 CCM imechukua mji tena, lakin Hadi Leo na wala bajeti ya tamisemi hakuna ilipoongelewa stendi hii finyo na mbovu ya bukoba.

Waganda, wanyarwanda wengi ambao hutumia au upita katika stendi hii hutusimanga Sana wabongo kwa kichochoro hiki.

Yes najua mtaanza kuwasema wahaya, kuwakejeli nk but hapa nchini sidhani kama kuna kabila lishawahi jenga stendi.

Wadau tazameni kichochoro hiki, stendi imezidiwa Hadi magari mengine hushushia magari barabarani.

FB_IMG_16197250342307593.jpg
FB_IMG_16197256724445829.jpg
FB_IMG_16197256658785428.jpg
FB_IMG_16197256853419645.jpg
 
Huwa mnapost majumba majumba mazuri uko migombani kumbe mna stand kama vichochoro vya wahaya

Ngoja watu wa Kilimanjaro waje tuone watasemaje
Hapa sio ligi. Yap wahaya watajenga vijijini kwao but sidhani kabila la wahaya litajenga stendi . Kabila halihusiki kabisa na stendi ya bukoba.


Ni wap bongo hii ulishaona kabila linajenga stendi hato huko Kilimanjaro sidhani kama kabila la wachaga limejenga stendi
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom