Hii nayo ni usanii mtupu, jamaa wamebadilisha tu jina la "Advanced Diploma" kuwa "Higher Diploma", ati wanadai wamefuta kiwango hicho cha elimu! Usanii!
Stashahada za Juu zafutwa
na Salehe Mohamed
SERIKALI imefuta mfumo wa elimu wa stashahada ya juu (Advanced Diploma) nchini kutokana na kutoendana na vyuo vikuu vya Afrika Mashariki sambamba na kuboresha elimu ya juu inayotolewa na vyuo vikuu.
Waziri wa Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Peter Msolla, alitangaza uamuzi huo jana alipokuwa akifunga kongamano la wakuu wa vyuo vikuu na vitivo kwa nchi za Afrika Mashariki lililofanyika jijini Dar es Salaam, kwa wiki moja.
Alisema, kutokana na kufutwa kwa mfumo wa stashahada hiyo, wanafunzi wenye vyeti vya stashahada ya juu hawatoweza kuendelea na shahada ya uzamili (Masters) mpaka watakaposoma mwaka mmoja zaidi.
Msolla, alibainisha kuwa, mfumo huo ulitumika nchini pekee hali iliyochangia kutofautisha kati ya elimu ya Tanzania na nchi nyingine, lakini kutokana na makubaliano yaliyofikiwa na wakuu wa vyuo vikuu vya Afrika Mashariki, Tanzania imefuta kiwango hicho cha elimu ili kujenga wigo mpana zaidi wa elimu ya juu.
Tumefuta mfumo huu, sababu kubwa ya kufanya hivi ni kuboresha elimu ya juu ili kuendana na nchi jirani ambazo hazina utaratibu tuliokuwa tukiutumia hapa nchini, hivyo kuanzia sasa hautambuliki, alisema Professa Msolla.
Alisema, si kweli kuwa mwanafunzi aliyetunukiwa stashahada ya juu (Advance Diploma) ni sawa na aliyetunikiwa shahada (Degree), hivyo ni vema wananchi waelewe ukweli huo ili wasichanganye viwango hivyo vya kitaaluma.
Alibainisha kuwa, kutokana na kufutwa kwake, sasa utatumika mfumo mpya wa higher diploma ambao pia haulingani na shahada.
Kuhusu kongamano hilo, alisema lengo lake ni kuweka mikakati ya kuhakikisha ubora na taaluma inayotolewa katika vyuo vyote vikuu vya Afrika Mashariki unalingana kwa lengo la kumpatia mhitimu ufahmu wa kutosha utakaomwezesha kukabiliana na changamoto za dunia.
Profesa Msolla pia alisema, anategemea kongamano hilo litatoka na njia muafaka za kuwabana watu wanaoghushi vyeti ili kujipatia kazi au kujiendeleza zaidi na elimu ya juu kwa kutumia vyeti hivyo.
Alisema, ni vema mamlaka husika za elimu ya juu kuangalia kwa ukaribu tatizo hilo linazidi kukua kila kukicha na kutafuta njia muafaka za kulidhibiti ili kuwa na wataalamu waliofanya juhudi za dhati walipokuwa wanasoma.
Tanzania, Uganda na Kenya nina hakika zitakuwa mashahidi wazuri wa kukithiri kwa matumizi ya vyeti vya kughushi na kuvuja mitihani, ni changamoto kwetu kulitatua tatizo hili na ikiwezekana kulizuia kabisa kwani linatia aibu, alisema Professa Msolla.
Hivi sasa kumekuwa na ongezeko kubwa la wanafunzi wanaofaulu kupitia mpango wa Elimu katika Shule za Msingi na Sekondari (MMEM na MMES), hivyo ni vema vyuo vikuu vishiriki vijitahidi kutoa elimu bora ili vipande na kuwa vyuo vikuu na kuongeza nafasi za wanafunzi.
Naye Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu (TCU), Profesa Mayunga Nkunya, alisema takribani vyuo vyote vilivyohudhuria mkutano huo, vimeukubali mfumo wa kuhakiki ubora wa elimu na tayari vimeanza kuutumia.
Malengo tuliyojiwekea katika kongamano hili yamefikiwa, cha msingi tulitaka kujua ni hatua gani vyuo vikuu vitachukua kuhusiana na mfumo huu mpya ambao nina imani utasaidia sana kuboresha elimu, alisema Profesa Nkunya.
Alisema wamekubaliana kuwa kila chuo kiweke utaratibu utakaohakikisha taaluma inayotolewa ni ya ustadi wa hali ya juu inayoendana na hadhi ya kimataifa.
Source: Tanzania Daima