Star TV na ITV kujitoa rasmi Startimes muda si mrefu!

Star TV na ITV kujitoa rasmi Startimes muda si mrefu!

Sheria inasemaje au ndiyo mnataka kutulazimisha sisi walaji tununue decoder 50.

amakweli hapa sheria inabidi iingilie kati, otherwise tutanunua ving'amuzi kila leo kuzifuata hizo chanel zinazotukimbia!
 
Kwenye hiki king'amuzi cha kikulima cha Star Times kuna tangazo linapita kuwa Star TV wanataka kujitoa kwa Star Times,Sijui wanafikiria nini wakati coverage yao ni ndogo sana hasa kwa kupitia king'amuzi chao cha CONTINENTAL.
Nafikiri hawajajifunza kwa CLOUDS TV ambao walijifanya wanakimbia Star Times wakati hata watazamaji hawana,
Nafikiri wakae chini waangalie suala hili vizuri kabla ya kukurupuka.

tayari startv washasign mkataba na dstv coverage yao sasa ni world wide.
 
Statv nawapata kupitia dishi. Hawana vipindi vya mana, ukiangalia taarifa yao ya habari hawana mvuto kabisa, nadhani wadau hamtapungukiwa sana kama hawa jamaa watajitoa!
 
Si walituambia kuwa
ving'amuzi vyote vitakua vinaonyesha 5 local channels bure including
itv, star tv, tbc 1,chanel 5 na channel 10?
There you are. Hiyo ndiyo sheria, ila sijui inakuwaje pale mtoa huduma anaposhindwa kutosheleza mahitaii ya wateja kama Startimes.
 
Habari nilizozipata, mda mfupi ulio pita ni kuwa mwanasheria wa continental ametuma barua ya kuitaarifu startimes kujitoa kwa startv rasmi startimes, na mda simrefu Itv nao wanatuma rasmi barua kama hiyohiyo, huk startimes mashop yote ya dar ya startimes yameambiwa yawataarifu wateja kuhusu kutoka kwa hizo channel mbili.

NTAENDELEA KUWA UPDATE.....

Source mimi mwenyewe toka maeneo ya hapa bamaga startimes, nimepata habari hizi nikiwa ndani ya duka lao mda huu..wakijadiliana watafanyaje???

Star Tv ..tayari washatoka mpaka sasa ...ITV Bado .
 
TCRA kwa kuwa ni Wana jf tafadhalini
njooni kwenye hii thread ili mtupe ufafanuzi.




Cc TCRA
 
Kwakweli ningeshangaa kama kusingekuwa na mtu kama wewe wa kuwaelezea haya. Bravoooooo
 
Mkuu bampami, kwani tatizo ni nini hasa linalowafanya Startv na ITV wajitoe? Kumbe ndio maana Startv hawapo hewani! Nimehangaika sana kusearch nikawa najiuliza kuna tatizo gani? ITV bado wapo hewani. Ama kweli mafisadi wanatisha! Wametulazimisha tuingie kwenye digitali kwa manufaa yao! Bila shaka kuna biashara inaandaliwa!!!
 
Majanga tikila aka TCRA wamelala tu usingizi wa pono.
 
Last edited by a moderator:
mamaaaaaaaaaa wapi startv ndo wametoka nini? mbona hatujaandaliwa na kesho ni j2 mijadala ya kisiasa jamani nitaimis! pia magazeti asubuhi!
 
TCRA wapo humu ndani, tafadhali tupeni ufafanuzi, sheria ya kuonyesha chaneli Tano za ndani kwa kila king'amuzi imebadilishwa.?
 
Last edited by a moderator:
Statv nawapata kupitia dishi. Hawana vipindi vya mana, ukiangalia taarifa yao ya habari hawana mvuto kabisa, nadhani wadau hamtapungukiwa sana kama hawa jamaa watajitoa!
mkuu tutapungukiwa sana. ni local tv pekee inayojiunga na bbc swahili tv kila baada ya taarifa ya habari.vilevile ni local TV yenye reporter mzuri sana wa Habari za kimataifa Mr. SAMADU HASSAN.Ni tv iliyokuwa inajitahidi kuonyesha baadhi ya mechi za mpira wa miguu,ni tv pekee yenye kipindi cha viroja cha pika bomu na futuhi
 
Back
Top Bottom