Stanslaus Mabula umesema vema kuhusu uwanja wa ndege Mwanza na barabara kuu njia nne

dndagula

JF-Expert Member
Jul 24, 2016
1,460
1,444
Mimi nianze kwa kumpongeza mbuge wa nyamagana na aliyekuwa mkuu wa mkoa wa mwanza bw adam malima kwa kusemea kwa nguvu kubwa ukamilishaji wa uwanja wa ndege wa mwanza, jengo la abiria na miundo mbinu yake.

Suala la uwanja wa ndege ni la muda mrefu sana kila mara hupigwa chenga,hata bajeti ya ujenzi ya mwaka huu haumo, je kuna nini?

Uwanja huu una manufaa makubwa kwa kanda ya ziwa, nchi za maziwa makuu na taifa kwa ujumla. Nadhani sasa, serikali ikamilishe uwanja huu sambamba na viwanja vingine ili kuliwezesha taifa kunufaika zaidi kimapato kwa vile ndege za kimataifa zitatua na kulipia paking, mizigo n.k aidha barabara unganishi na jiji nazo ziwekwe kwenye bajeti ya mwaka 2023/2024.

Miundo mbinu ya daraja, barabara, meli, reli na ndege ziwe unganishi(interlinked). Miradi hii ya kimkakati ni ya kuangalia kwa umakini mkubwa na kwa jicho la kiuzalendo kwa vile impact yake ni kwa taifa zima.

Watu wangapi wanapitia uwanja huu wakiwemo viongozi wa kitaifa na kimataifa lakini ajabu hata vip lounge ni aibu. Uwanja huu unaliaibisha taifa kwa sasa.

Wizara ya ujenzi isichenge chenge na kuuruka kwenye bajeti kumwangusha mama. Juzi km eng aisha alipita pale kukagua na akakubaliana na mapendekezo ya upanuzi wa jengo. Sasa imekuwaje tena?

Naibu waziri wa ujenzi akiwa na waziri mkuu walitoa ahadi ya kuanza ujenzi wa barabara ya upanuzi kenyatta road. Wananchi tulisikia sasa kulikoni!
 
Back
Top Bottom