Tatizo la ujenzi wa uwanja wa ndege Mwanza nini hasa, tuelezeni

dndagula

JF-Expert Member
Jul 24, 2016
1,461
1,445
Sisi wazalendo tunakerwa sana na uzembe wa TAA kuanza ujenzi wa jengo la uwanja wa ndege wa Mwanza, wameahidi mara kadhaa kwa Mkuu wa Mkoa, kuwa pesa imetolewa na Rais bilioni 30 sasa.

Kinachochelewesha ni nini? Songwe imeishakamilika, Tabora, Iringa, Tanga, Msalato, Arusha, Moshi vinajengwa au michakato ya ununuzi kukamilika Kiwanja cha Mwanza kuna nini, nadhani kuna namna Rais suala hili lichukue mwenyewe binafsi kuna mchezo na figisu zinachezwa na kudhalilisha mamlaka.
 
Inasikitisha kwakweli binafsi nimefatilia karibu wakuu wa mikoa watatu walioletwa Mwanza wameusemea sana huu uwanja lakini wapi, Amosi Makalla kila siku ndio kiitikio chake kwenye mikutano mingi lakini wapi, Tatizo ni nini is it fare minofu ya Samaki kupelekwa Nairobi na Entebe, ni mara ngapi Wafanyabiashara wa madini wa kanda ya ziwa wakitaifishwa dhahabu zao hapo Nairobi, Mama Samia tunakuomba sana mama lichukulie hili kwa uzito maana wasaidizi wako wameshindwa!!
 
Mimi nikipita pale Airport aibu huwa naona mimi maana sio kwa upuuzi ule.

Yaani miaka nenda rudi ujenzi unasuasua sijui nini kinaendelea pale yaani ni kituko kabisa.

Labda Mama Samia ahamishie shughuli zake pale ndo utaisha vinginevyo tutazeeka ukiwa haujakamilika wakati umeanza kuujengwa tukiwa vijana.
 
Kwani lile jengo kubwakubwa pale pembeni halijaisha kama limetelekezwa flani hivi huwa linamaanisha nini? Mbona kama limekatiwa tamaa.
 
Huyu jamaa@ChoiceVariable yaani analeta chuki mpaka kwenye vitu vyenye impact kwa taifa sijui anahisi mwanza ipo Kongo sio poa bro sie wote Watanzania kuwepo huo uwanja hakutakupunguzia chochote sana naamin utakunafaisha mwa namna moja ama nyingine madamu upo Tanzania
 
Kiwanja cha Chato ni cha mkoa wa Geita, mbona hamsemi cha Shinyanga, Bukoba ama Musoma, au kama vipi waboreshe hicho cha Chato kikubwa tuwe na International Airport kama tatizo ni hilo.
 
Kwanza twambie kile kibamba cha abiria kimesha isha..

Stand ya mabasi nyegezi ni nzuri kuliko hicho kibanda
 
Inasikitisha kwakweli binafsi nimefatilia karibu wakuu wa mikoa watatu walioletwa Mwanza wameusemea sana huu uwanja lakini wapi...
Mkuu niliona taarifa mkuu wa mkoa wa mwanza akilikaribisha shirika la NSSF kuwekeza katika uwanja wa ndege wa mwanza.
 
Mkuu niliona taarifa mkuu wa mkoa wa mwanza akilikaribisha shirika la NSSF kuwekeza katika uwanja wa ndege wa mwanza.
Ndugu yangu enzi za Adam Malima alihaidi mengi mno ziara za viongozi wa wizara ya uchukuzi zikibamba kwa sana lakini wapi, Mh Amosi Makalla je, ilikuwa mwezi wa 12, ikasogezwa mwezi wa pili, imesogezwa wa 3 nao ndo huu unaendelea kuyoyoma au labda wanasubilia bunge la bajeti?
 
Huu mchezo wa kuchelewesha ujenzi wa jengo la abiria airport Mza alaumiwe nani Wizara,TAA ya bw Mussa, au PPRA nani hasa iwapo Rais kishatoa maelekezo na pesa,Makalla naye kila siku hulisemea mpaka sasa NSSF nao wamealikwa, hapa kuna mchezo mchafu wa kuchelewesha. Kanda ya Ziwa tuamke,wananchi,wabunge na viongozi wa dini tulisemee kwa sauti kubwa kwa manufaa mapana ya taifa, miradi ya kimkakati kanda ya ziwa iko shida. Fikra potofu kuwa kanda ya ziwa ilipendelewa awamu ya 5 ni potofu na ni kichaka cha kujificha kuihujumu Mwanza angalia miradi ya DSm,Arusha,Dodoma Pwani Rufiji nk mbona haisemwi ni mingi na mikubwa na sasa Samiah Stadium inaanza kujengwa keshokutwa Arusha. Airport MWANZA ni mradi wa siku nyingi umezungumzwa zaidi ya miaka 30.Mama shtuka wanakuangusha kimkakati baadhi ya watendaji hususani kwa hili. Tatizo la uwanja huu Linafahamika,halibishaniwi. inasikitisha na kutia hasira kuzuia uchangiaji mkubwa wa mapato kupitia uwanja huu
 
Back
Top Bottom