Tabutupu
JF-Expert Member
- Nov 26, 2010
- 13,111
- 18,327
Serikali imewekeza fedha nyingi sana kutoa huduma bora kwa wananchi hasa kwenye secta ya usafiri..
Ila Halmashauri ambazo zimepewa jukumu la kuzisimamia stand za mabasi zimekua zikichukua fedha na kuziacha stand zikiwa chafu hadi zinahatarisha maisha ya wananchi.
Madharani stand ya Dodoma ambayo ni moja ya stand za gharama kubwa Africa, ukipita sasa viti vimevunjika, vyoo vichafu, maeneo ya nje ya ya hovyo, restaurant zote zimevungwa, kimekua kijiwe cha wahuni tuu..
Stand ya Magufuli Mbezi Luis ni hivyo hivyo, wakati ilitakiwa hizi stand ziwe ni maeneo mazuri hata watu kwenda kutembea..
Kwanini Airports hata zile ambazo zinaingiza fedha chache kiliko hizi stand zipo well maintained, zina garden safi, vyoo safi, miti ya vivuli , walking ways safi etc..
Cha pili kwanini stand hizi zina toza fedha abiria wanao safiri wakati airports hazitozi?
Kwani wasiregemee tuu wanao toa huduma?
Tunahitaji serikali iliangalie swala hili maana stand ya bil 55 kuwa kijiwe cha wahuni ni.bora wangejenga hospitali.
Mapendekezo
1. Stand zote zisimamiwe na chambo kimoja.. na fedha zinazopatikana zigawanywe kuhudumia stand na halmashauri husika ..
2. Serikali iunde chombo cha kusimamia stand hizi kama ilivyo kwenye usafiri wa anga. Let say chombo hicho kiitwe BUS TERMIANLS AUTHORITY (BUTA). chombo hiki kitakua na jukumu la kuhakikisha stand zinakua ni sehemu nzuri na salama kwa raia kupata huduma pamoja na kuendeleza na kujenga stand za mabasi nchi nzima.
Kinacho tokea kwenye stand ndicho kinatokea kwenye hospitali zote zinazo simamiwa na halmashauri.. sio kwamba hawana pesa ila pesa zote zinaishia kulipana posho.
Ikiwezekana hospitali zote sisimamiwe na wizara husika pamoja na shule zote zisimamiwe na wizara ya elimu.
Kuna matatizo mengi sana kuachia halmashauri majukumu makubwa.
Mungu ibariki Tanzania na naamini siku moja usafiri wa ardhini utapata msimamizi wa stand za mabasi (BUTA)