Waziri Mhagama aagiza kujengwa stendi yenye ubora kijiji cha Lundusi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944

WAZIRI JENISTA MHAGAMA AAGIZA KUJENGWA STENDI YENYE UBORA KIJIJI CHA LUNDUSI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama amezitaka Idara zinazohusika na ujenzi katika Halmashauri kuhakikisha zinajenga stendi ya mabasi yenye ubora unaoendana na thamani ya fedha zilizotolewa ili kujenga Stendi hiyo katika Kijiji cha Lundusi, Halmashauri ya Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma .

Mhe. Jenista ametoa maagizo hayo wakati akizindua mradi wa ujenzi wa Stendi ya kisasa ya magari katika kijiji hicho unaotekelezwa na Ofisi ya Rais kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) utakaogharimu shilingi Milioni 482 ukitarajiwa kukamilika katika kipindi cha miezi sita tangu kuanza kwa mradi .

Amesema katika awamu ya kipindi cha pili cha utekelezaji, TASAF imejikita katika masuala ya kuwezesha Kaya kutumia fursa za kukuza Uchumi na kuongeza kipato kwa kaya zenye walengwa pamoja na kuboresha upatikanaji wa huduma za Afya, Elimu na Maji Safi na Salama pamoja na miundo mbinu ya kukuza uchumi ngazi ya jamii .

" Wananchi wanasubiri Stendi bora ya kisasa na siyo stendi mbovu,idara zinazohusika na ujenzi kwenye Halmashauri sasa kumekucha na hatutarajii eneo la manunuzi ya ujenzi yakawa ni kichaka cha upotevu wa fedha kutoka Ofisi ya Rais kupitia Mfuko wa TASAF hivyo matumizi sahihi ya fedha yajidhihirishwe katika mradi huu," Amesema Mhe. Jenista .

Aidha Mhe. Jenista ametoa wito kwa wataalam kutekeleza majukumu yao kama inavyotakiwa hasa maafisa wa Idara ya Ujenzi, Manunuzi na Fedha ili kuepuka kusuasua kwa mradi huo pamoja na kuimarisha usimamizi na ufuatiliaji katika ngazi zote kuanzia hatua ya awali hadi hatua ya mwisho ya ukamilishaji wa mradi .

" TASAF ni chombo cha Serikali ambacho kinasaidiana na vyombo vingine kusaidia jitihada za kuondoa kero ya umaskini, upatikanaji wa maji safi na salama, elimu na afya ili kujenga Jamii iliyo bora, ambayo sisi sote ni mashahidi. TASAF imeleta mafanikio makubwa katika Nchi yetu kama ilivyoainishwa katika Mpango wa pili wa Taifa wa Maendeleo wa 2020/2025 kwa kutumia dhana ya ushirikishwaji wa Jamii ,"Amebainisha Waziri huyo.

F6OX2y9W4AA7dhS.jpg
WhatsApp Image 2023-09-18 at 14.24.27(2).jpeg
WhatsApp Image 2023-09-18 at 14.24.27.jpeg
 
Kabla ya stendi, fanyeni mchakato wa Elimu, Maji na Zahanati kwanza.
 
Back
Top Bottom