Ushauri kwa Waziri Mchengerwa wa namna ya TAMISEMI kudhibiti mapato ndani ya Halmashauri zote za mitaa nchini

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
14,939
20,400
Moja kwa moja kwenye mada.

Haya madini ntayokupa hapa hutapata popote maana weye natambua una "potential" kubwa huko mbele ya safari.

Kama kawaida yangu jana baada ya kusikiliza ulokisema nikaingia kwenye dawati langu la uchambuzi hapa Kibaigwa na nikachambua ulokisema jana ili kupata mawili matatu na ndo nikaja na huu ushauri.

Mheshimiwa Mchengerwa jana nimekusikiliza uzuri sana kuhusu maamuzi yako yanowataka makandasi wakamilishe miradi ya ujenzi kwa haraka na wawe wazimaliza kwanza kazi kaboa ya kupewa kazi zingine.

Pia katika hotuba yako ukaongelea suala la wakurugenzi wa halmashauri kukaa na fedha za mapato ya halmashauri kwa miaka miwili bila ya kuzitumia wakisubiria muda muafaka wa kuzipiga.

Kuna mada humu nimekupongeza kwa kuwataka Wakurugenzi hao wakazitumie fedha hizo kwa uangalifu na kwa malengo yalokusudiwa. Nikakusifu kwa hatua hizo za kimamlaka ambazo zitakuweka kwenye nafasi ya kuwa kiongozi ambae utachukua hatua kali kwa wale wote wapigaji na wapambe wao endapo watatumia vibaya fedha na mali za umma.

Lakini kile ambacho khasa kimenipa msukumo wa kuandika ushauri huu kwako ni kujaribu kuleta mabadiliko ya kiutendaji pamoja na kifikra kwamba viongozi wana dhamana ya wananchi wao katika kuongoza na wao ni kioo cha jamii wanoingoza.

Serikali za mitaa ni maeneo muhimu sana kwa uchumi wa nchi na ukuaji wake yaani kwa kiingereza twaita "Local Growth". Ndo maana mimi ni muumini mkubwa wa madaraka mikoani au "local democracy" kwamba tawala za mikoa zinakuwa na uwezo wa kujiamulia kupanga mipango yake ya kimaendeleo kwa kutumia mapato yanotokana na kodi khasa za biashara ambazo sehemu fulani hutengwa kwa ajili ya kuendeleza halmashauri.

Hivyo utakuta halmashauri yakusanya mapato lakini halmashauri hiyohiyo inakuwa na uwezo wa kuamua ni kiasi gani kiende serikali kuu na kiasi gani kibakie kwenye halmashauri ambapo kiasi hichi kitaenda kuboresha masuala kama miundombinu, huduma za Afya na Elimu.

Itafika wakati utakuta halmashauri zina uwezo wa kuchukua asilimia hadi 50 ya mapato hayo ili kuyatumia katika kujileletea maendeleo.

Suala jingine la kuliangalia ni namna ya udhibiti wa vyanzo vya mapato vya halmashauri za miji au "Revenue source". Tukitaka tutoboe kama nchi ni lazima tuangalie namna ya kudhibiti mapato haya khsa kutoka kwenye kodi za maendeleo, kodi za biashara kubwa, biashara ndogo na kodi zingine ndogondogo.

Ushauri mwingine katika kutafuta na kuboresha vyanzo vya mapato katika miji na majiji, TAMISEMI ni lazima iangalie maeneo yafuatayo.

1. Katika miji mikubwa ambayo ipo ndani ya eneo la kati yaani "central financial district" nyumba za makazi ni lazima ziwe na kiwango fulani cha kodi ambayo ni ya kila mwezi kwa wananchi waishio katika eneo hilo pamoja na laisifi na majengo mbalimbali ndani ya eneo hilo.

2. Ushuru wa barabara yaani pamoja na ushuru wa kuingiza gari katikati ya jiji, na ushuru wa hewa safi ili kuboresha mazingira ni lazima mapato yafanywe kwa njia ya kieletroniki ambapo fedha huenda moja kwa moja kwenye akaunti ya halmashauri lakini waziri na timu yake wawe na uwezo wa kutambua maingizo ya kila siku ili kuweka kumbukumbu sawa.

3. Maegesho ya magari ndani ya eneo la katikati ya jiji pia ni vyanzo vingine vya mapato kwa halmashauri kwani fedha hupatikana kwa kuwekeza kwenye mashine maalum Pay Stations ambapo wamiliki wa magari huweza kufanya malipo kwa kutumia kadi zao za benki.

Njia hii itaondoa wizi unofanywa na wakusanyaji wa mapato hayo ya maegesho na utashangaa kiasi cha fedha ambazo zitakuwa zaingia kwenye akaunti kutegemea na miji husika maana si miji yote watu huendesha magari. Ila ni lazima miji yote izuie kuingiza magari katikati ya mji na iwe ni free zone kwa ajili ya biashara mbalimbali kama maduka na kadhalika.

3. Kodi za kiwanja na majengo au Stamp Duty hizi kodi zote ni lazima ziwe ni za kielektroniki ili kuweza kudhibiti ukusanyaji. Njia sahihi au mechanism ya kuhakikisha fedha hizi zakusanywa kwa wakati ni kuhakikisha kila ofisi ya halmashauri ina dwati maalum la ukusanyaji kwa kila mwezi ili kila mwananchi ambae ni subject kwa kulipa hizi kodi analipa kwa wakati na mapatoi kupatikana kwa wakati.

4. Mapato yatokanayo na Utalii pia ni mapato ambayo hupaswa kupigwa panga na halmashauri kabla ya kupelekwa serikali kuu kwani hivi ni vyanzo ambavyo vipi katika kila mkoa au halmashauri. Ingawa vyaweza kuwa ni ndogo kodi hii yaweza kutumika (locally) kuboresha miundombinu ya kiutalii. Kwa mafno maeneo ya utalii ambayo yanahitaji njia bora za kupita ama kwa magari au kwa watembea kwa miguu, alama maalum za kuongozoea njia hizo na miundombinu kama madaraja na huduma za dharura.

Haya yote ni baadhi tu ya maeneo ambayo serikali kupitia TAMISEMI yaweza kuyafanya ili kuleta mabadiliko ya kiuchumi na hatimae kuleta maendeleo kwenye ngazi za halmashauri za manispaa na majiji. Maendeleo hayaji kwa kuketi tu ofisi kwa hawa wakurugenzi na kuoiga madili yan namna ya kupiga fedha za walipa kodi bali hutokana na jitihada na mikakati maalum.

Kwa mfano uboreshaji wa kodi za biashara au business rates waweza kuleta mabadiliko makubwa kwa kuongeza idadi wa wafanyabiashara wakubwa na wadogo na pia kuvutia wawekezaji kutoka ndani na nje ambao watavutiwa na miundombinu bora na umeme wa uhakika.

Kodi za viwanja, ardhi na mauzo ya viwanja na shughuli kama hizi zitaweza kuhamashisha shughuli za kiuchumi kukua "business growth" hivyo maendeleo kuanza kushika kasi.

Mwisho, usiishie kusimama tu majukwaani na kuzungumza bali uhakikishe wawafuatilia hawa vijana wenzio ambao bado waendekeza tamaa na kuvutwavutwa mashati na wapigaji na mwishoe kuishia kuiba fedha za walipa kodi bali wafuatilie na uwe na kikosi kazi ambacho kazi yake ni kufanya kitu chaitwa "check the checkers".

"Checkers" ni wahasibu na wakaguzi wa mahesabu lakini nawe wajiongeza kwa kuwa na "checkers" wako weye mwenyewe.


Ijumaa Karim.
 
Back
Top Bottom