Spika Ndugai: Wabunge 19 waliofukuzwa CHADEMA wapo kwenye mikono salama

Nape zamu hii lazima avuliwe uanachama wa ccm, apoteze na hako kaubunge kake, akaungane na wenzake chadema. He is too much. Zamu ile aliomba samahani na akasamehewa (kwa mazungumuzo yake kwenye simu yaliyodukuliwa, wakimsema vibaya aliyekuwa rais wa JMT wakipanga mipango mibaya dhidi ya serikali).

Avuliwe uanachama wake wa ccm na tuone kama atang'ang'ania huo ubunge.
Juzi tulimwona akiwa na akina Lissu kwenye zoom wakiisema vibaya serikali ya awamu ya 6 chini ya mama yetu SSH!
Wewe ni mgonjwa, aliowasema Nape wamevuliwa uanachama lakini bado wanaendelea na ubunge. Sasa wewe unataka avuliwe uanachama yeye. Ndiyo sheria ya kupoteza ubunge itumike kwake. Kwa manufaa yako!
 
Eti Chadema kuna mfumo Dume. Atuambie chama gani kinachosimamishaga Wagombea Ubunge wengi Wanawake Majimboni kuliko Chadema
 
Hivi nchi hii hakuna vyombo vya ulinzi na usalama vyenye jukumu la kulinda katiba hasa wanapojitokeza wendawazimu kama huyu nduguyai wanaonajisi sheria kiasi hiki asee.
 
Kama hakuvuliwa wakati wa Jiwe ndio imetoka hiyo,hatavuliwa tena kwanza Chama kimerudi upande wao.
Wewe subiri utaona. Tena ni rahisi tu kwani kwenye katiba ya ccm mamlaka ya kumvua mwanachama uanachama yako kwenye ngazi ya tawi tu au NEC basi.
 
Wewe ni mgonjwa, aliowasema Nape wamevuliwa uanachama lakini bado wanaendelea na ubunge. Sasa wewe unataka avuliwe uanachama yeye. Ndiyo sheria ya kupoteza ubunge itumike kwake. Kwa manufaa yako!
Kwa manufaa ya chama. Huyu mtu ameshindwa kujirekebisha. Sasa hivi anafanya kazi na Tundu Lissu kupitia zoom kutupaka matope. Mbona mwenzake January Makamba katulia baada ya msamaha. Huyu Nape bado chuki na hasira ya kukosa uwaziri bado imemuganda.
 
Kwa tabia yako ni kama vile watokea kwao akina Bashiru
Ona sasa wana chadema walioko huku Jf wanavyomtetea Nape. Hii inadhihirisha Nape ni mwenzao. Ni kati ya watu wanaompelekea taarifa Tundu Lissu huko Ubeligiji ili aendelee kuichafua nchi yetu.
 
Leo Ndugai ndo anajifanya mtetezi wa hao wanawake!!! Inawezekana Kuna jambo nyuma ya pazia juu ya hawa wabunge
 
Leo Bungeni baada ya kipindi cha maswali na majibu, Spika wa Bunge Job Ndugai amesimama na kumkemea Nape Nauye, Mbunge wa Mtama ambaye hivi karibuni alitoa maoni yake binafsi kuwa wale wabunge 19 waliotimuliwa na CHADEMA sio wabunge halali.

Ndugai, akonekana mwenge wasiwasi na aliyepoteza mwelekeo akaanza kwa kujisifu kuwa yeye ni mzoefu, hivyo asipangiwe cha kufanya.

Ameenda mbali zaidi kwa kutaka kuonesha kuwa akina mama hao 19 wanaonewa na mfumo dume uliopo CHADEMA. Ndugai anasahau yeye na Profesa Lipumba walichowafanyia akina mama wa CUF walipovuliwa ubunge kwa kimemo cha Lipumba.

Mzee Ndugai atabaki katika historia kama SPIKA DHAIFU kuwahi kutokea. Tunazitaka Mamlaka za kulinda Katiba kuhakikisha KATIBA inalindwa.

Ikiwezekana kila NDUGAI atakapoonekana hadharani azomewe kwa aibu anayoiletea Taifa.
Spika ni mwongo tena msahaulifu au anafanya kazi kwa double standards. Nakumbuka mwaka 2017, yeye mwenyewe tena siku moja tu baada ya kupokea barua kutoka kwa Mwenyekiti wa CUF Taifa aliyekuwa akitambuliwa na Ofisi ya Msajili wa vyama, kipindi hicho kuna mgogoro wa ndani, Prof. Ibrahim Lipumba inayoeleza kuwafukuza uanachama Wabunge wanane wa Viti Maalum na Madiwani wawili, Bunge likaridhia kufukuzwa kwao na akasisitiza kwamba ameridhia kufutwa uanachama kwa Wabunge hao na hivyo nafasi zao ziko wazi.
Prof. Lipumba alitangaza kuwafuta uanachama Wabunge wanane na Madiwani wawili kwa makosa mbalimbali yakiwemo ya kinidhamu, kukihujumu chama, Kumkashifu na kumdhalilisha Mwenyekiti.
Tena nainukuu taarifa iliyotolewa: "Spika Ndugai amejiridhisha kuwa Wabunge hao wamefutiwa uanachama kulingana na taratibu za chama hicho na hivyo hawana sifa za kuendelea na Ubunge. Hivyo kwa mamlaka aliyonayo kwa kuzingatia kifungu cha 67(1)(b) cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 kikisomwa pamoja na kifungu 37(3) cha Sheria ya Uchaguzi Sura ya 343 kama ilivyojadidiwa Mwaka 2015, Spika ametangaza nafasi hizo kuwa wazi na kumuandikia Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi aendelee na hatua zinazostahili kujaza nafasi hizo kwa mujibu wa Sheria. Waliovuliwa ubunge ni Mheshimiwa Severina Silvanus Mwijage, Mheshimiwa Saumu Heri Sakala, Mheshimiwa Salma Mohemed Mwassa, Mheshimiwa Riziki Shahari Mngwali, Mheshimiwa Raisa Abdallah Mussa, Mheshimiwa Miza Bakari Haji, Mheshimiwa Hadija Salum Ally al Kassmy na Mheshimiwa Halima Ali Mohamed.
Hebu sasa tujiulize, mbona wote hawa walikuwa ni wanawake hapo hakusema kwamba walionewa na mfumo dume ndani ya CUF? Alipewa maelekezo kutoka juu afanye hivyo ili kukivuruga CUF? Tatizo hilo na la sasa tofauti yake ni nini mbona sasa hivi hachukui maamuzi akijifanya kuwatetea wabunge wa viti maalumu wa Chadema? Au tatizo la spika ni kwamba hataki kusikia jambo lolote kutoka Chadema na akakubaliana nalo? Hebu tujadiliane hapo kwanza.
 
Ccm ni ile ile hamna jipya. Wapo radhi wavunje katiba na sheria za nchi kwa maslahi yao binafsi
 
Spika Ndugai amejiridhisha kuwa Wabunge hao wamefutiwa uanachama kulingana na taratibu za chama hicho
Hujaelewa kitu gani hapo? Spika lazima ajiridhishe kuwa kufutiwa uanachama wa wabunge umefuata taratibu na katiba ya chama husika. Spika aliridhika CUF ilifuata kanuni na taratibu za katiba yake kuwafukuza uanachama wabunge wake. Chadema haikufuata kanuni na taratibu za katiba yake. Chadema haikutaka hata kusikiliza utetezi wa wahusika kabla ya kuwaadhibu, hivyo ilikiuka misingi ya natural justice. Kwa mjibu wa katiba ya chadema, baraza kuu la chama ndilo lenye mamlaka ya mwisho kwenye maamuzi ya kufukuzwa uanachama. Kwa sababu ya ukwasi baraza hilo limeshindwa kukutana. Taarifa kwa spika ya kufukuzwa uanachama wa wabunge hiyo aliipata kwa njia ya kipeperushi cha katibu mkuu, hivyo kushindwa kuridhika nacho kama kanuni na taratibu zote za katiba ya chadema zilifuatwa kuwafukuza wabunge hao.

Fuateni taratibu na kanuni za katiba yenu. Baraza la chama likae kutoa maamuzi yake. Wahusika kama hawataridhika wanaweza kukata rufaa mahakama kuu. Uamuzi wa mwisho kwenye suala hilo ni mahakama. Hivyo wahusika wataendelea kuwa wabunge hadi pale mahakama itakapoamua vinginevyo. Hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa Zitto Kabwe alipotimuliwa chadema, kwa nini iwe tofauti kwa hawa akina mama?
 
Mkuu, kumbuka Prof Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi, Dr John Samwel Malecela, Lusinde Kibajaji, wasanii na wanamuziki kama marehemu Patrick Balisidya na hata marehemu Dr/Prof. Hugo Zawose na wengine kibao wote walikua ni Wagogo. Je na hao pia wanaingia katika fungu hilohilo ulilosema?
Hivi Prof palamaganda kumbe ni Mgogo?!
Ndio maana kama dishi limecheza kidogo.
There something wrong with these people from Capital City
 
Hujaelewa kitu gani hapo? Spika lazima ajiridhishe kuwa kufutiwa uanachama wa wabunge umefuata taratibu na katiba ya chama husika. Spika aliridhika CUF ilifuata kanuni na taratibu za katiba yake kuwafukuza uanachama wabunge wake. Chadema haikufuata kanuni na taratibu za katiba yake. Chadema haikutaka hata kusikiliza utetezi wa wahusika kabla ya kuwaadhibu, hivyo ilikiuka misingi ya natural justice. Kwa mjibu wa katiba ya chadema, baraza kuu la chama ndilo lenye mamlaka ya mwisho kwenye maamuzi ya kufukuzwa uanachama. Kwa sababu ya ukwasi baraza hilo limeshindwa kukutana. Taarifa kwa spika ya kufukuzwa uanachama wa wabunge hiyo aliipata kwa njia ya kipeperushi cha katibu mkuu, hivyo kushindwa kuridhika nacho kama kanuni na taratibu zote za katiba ya chadema zilifuatwa kuwafukuza wabunge hao.

Fuateni taratibu na kanuni za katiba yenu. Baraza la chama likae kutoa maamuzi yake. Wahusika kama hawataridhika wanaweza kukata rufaa mahakama kuu. Uamuzi wa mwisho kwenye suala hilo ni mahakama. Hivyo wahusika wataendelea kuwa wabunge hadi pale mahakama itakapoamua vinginevyo. Hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa Zitto Kabwe alipotimuliwa chadema, kwa nini iwe tofauti kwa hawa akina mama?
Labda nikukumbushe na kwa Ishu ya Tundu Lisu, mbona alifutiwa ubunge wake na Spika huyo huyo bila kufuata Natural Justice, tena huku Spika akijua kwa 100% yuko wapi lakini akajitoa ufahamu. Pia unakumbuka suala la Sophia Simba? Alifukuzwa na Kikao cha Kamati Kuu tu ya CCM, Halmashauri Kuu ikfanya kama rubber stamp lakini kwa kuwa alikuwa amepewa maelekezo kutoka juu, fasta tu akavuliwa ubunge na hakusubiri Mkutano Mkuu wala cha kwenda Mahakamani.
 
TLS na mzee Warioba na Jenerali Ulimwengu nyie ni wabobezi wa sheria inakuwaje mnakaa kimya kuona chombo muhimu kama bunge linachezewa na mtu mmoja tu. Hili sakata la kufukuzwa uanachama wabunge 19 wa Ndugai ndani ya CDM linapoteza kbs umuhimu wa kufuata sheria na katiba.

Hili la wabunge 19 ni dhahiri kuwa mpira huu upo kwa Ndugai na anaona aibu kuwatoa. Maana waanzilishi wa uchafuzi wa mfumo wa vyama vingi hawapo. JPM kachukuliwa na mungu. Kakuwa na Polepole hawapo tena sasa hili pira kwake ni la moto.

Ukimsikiliza anavyoongea na kuingiza maneno ya uchochezi eti ooh kuna vyama vina mfumo dume kwa kuonea wanawake unaona kbs hali kwake sio njema.

Anaenda mbali mpaka anadai kupewa katiba ya CHADEMA, hivi kweli JOB hana katiba ya CHADEMA!, huyu mtu ni wakuombewa tu. Anahitaji mpaka adidu rejea za kikao cha CHADEMA kajigeuza kuwa msajili wa vyama. Wabobezi wa sheria, pamoja na wabunge wa CCM hakikisheni mnawazomea hawa wezi wa fedha za umma ambao wameajiriwa na NDUGAI wanatoka.
 
Labda nikukumbushe na kwa Ishu ya Tundu Lisu, mbona alifutiwa ubunge wake na Spika huyo huyo bila kufuata Natural Justice, tena huku Spika akijua kwa 100% yuko wapi lakini akajitoa ufahamu...
Kwa alichokifanya na anachoendelea kufanya Tundu Lissu hakupaswa tu kufukuzwa ubunge bali pia uraia wa Tanzania. Kenya walishamfukuza uraia wa Kenya Bw. Miguna Miguna aliyeikimbilia kuishi nchini Canada.
 
Back
Top Bottom