Spika Ndugai, suala la akina Halima Mdee bado unavunja Katiba

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,505
51,109
Ningeomba kumkumbusha Spika Ndugai kiapo alichokula, cha kuongoza bunge kwa kufuata kanuni na sheria za nchi.

Ningependa kumkumbusha Ndugai kuwa alikula kiapo hicho huku ameshika biblia na huku akilitaja jina la Mwenyezi Mungu.

Ningependa kumkumbusha Ndugai kuwa kila siku kabla ya bunge kuanza kuna sala ya kuliombea bunge huku Jina la Mungu likitajwa

Sasa kwa muktadha huo, Ndugu Spika ajitafakari, Je wakati anakula kiapo kizito namna ile huku analitaja jina la Mwenyezi Mungu haogopi?, Yaani ni mkavu kabisa na moyoni mwake ana amani kabisa kuwa alilofanya ni sawa?

Mzee Msekwa amesema kuwa uwepo wa akina Halima Mdee bungeni ni uvunjifu wa katiba ya nchi, Je Ndugai ameziba masikio kabisa na kushiriki uvunjifu mkubwa huu wa katiba bila wasiwasi wowote?

Nimkumbushe tu Ndugai, Jina la Mwenyezi Mungu huwa halichezewi, Hicho kiapo ulichokula kuwa utaheshimu sheria za nchi halafu ukazivunja makusudi huku Ukijua, basi jua Biblia uliyoikamata wakati unaapa na Mungu alishuhudia. Na imeandikwa katika maandiko USILITAJE BURE JINA LA MUNGU wako!

Ndugai, Waondoe hao wabunge 19 ambao unajua wazi wamo bungeni kinyume cha katiba, nje ya hapo kumbuka kiapo chako ulichoapa kwa kulitaja jina la Mungu.

Ndugu Ndugai, Mungu huwa hataniwi!
 
Kwa nini unamtaja Halima? wengine hujawaona? au unataka uzi wako utrend?
 
Shetani hawezi kusikia maneno bila vitendo. huyu ni shetani atasikiaje maneno matupu?
 
Kiongozi anayeweza kuvunja katiba ya nchi waziwazi kama alivyofanya Ndugai, sijui system inawezaje kumvumilia kuendelea kukalia kiti kikubwa kama hicho cha Uspika
 
Ndugai aliletewa majina ya akina Halima Mdee na NEC

NEC imedai ilipokea majina hayo kutoka kwa J J Mnyika.

Nani wa kulaumiwa hapo!
 
Ningeomba kumkumbusha Spika Ndugai kiapo alichokula, cha kuongoza bunge kwa kufuata kanuni na sheria za nchi.

Ningependa kumkumbusha Ndugai kuwa alikula kiapo hicho huku ameshika biblia na huku akilitaja jina la Mwenyezi Mungu...
We mwache atakufa huko ameachama.
 
IMG_20210415_094924.jpg
IMG_20210415_093612.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ningeomba kumkumbusha Spika Ndugai kiapo alichokula, cha kuongoza bunge kwa kufuata kanuni na sheria za nchi.

Ningependa kumkumbusha Ndugai kuwa alikula kiapo hicho huku ameshika biblia na huku akilitaja jina la Mwenyezi Mungu....
Walifikiri wanaikomoa CDM, kumbe ni kodi za umma wanafisidi! Hebu tuone watawakumbatia mpaka lini!
 
Huyu jamaa hivi anafikiri hatujui ama msiba umetusahaulisha namna anavyoichezea katiba yetu eee - TUNAMUONYA KWA MARA YA MWISHO... upepo ushageuka mwendazake kashakwenda alikotaka sasa sisi tuliobaki tujisahihishe vinginevyo tusije kulaumiana - KATIBA ni suala NYETI sana.... papasa popote ruksa ila KATIBA tuachie wenyewe watanzania.
 
Ningeomba kumkumbusha Spika Ndugai kiapo alichokula, cha kuongoza bunge kwa kufuata kanuni na sheria za nchi.

Ningependa kumkumbusha Ndugai kuwa alikula kiapo hicho huku ameshika biblia na huku akilitaja jina la Mwenyezi Mungu....
Ikiwa mwenyekiti wao na katibu mkuu hawaongelei hilo swala la kina Halima mdee, ww ni nani hadi uje kuongea hilo swala hapa? Hilo swala mwenyekiti wa chama.

Ndugai na kina Halima Mdee wameshalimaliza juu kwa juu na sasa mwenyekiti anavuta chake kila mwezi kupitia ruzuku yao ndio maana unaona hakuna anaefungua kopo lake huko chamani kuuliza juu ya ubunge wao.

Afu wewe unakurupuka from nowhere kuja kuandika utumbo wako hapa JF.
 
Ndugai aliletewa majina ya akina Halima Mdee na NEC

NEC imedai ilipokea majina hayo kutoka kwa J J Mnyika.

Nani wa kulaumiwa hapo!
Ishu ni kwamba wamefukuzwa na chama chao, hivyo hawana chama kwa sasa, hiyo inawaondolea haki ya kuwa wabunge
 
Hivi hili swali halitakiwi kuulizwa na mbunge bungeni humo,likatolewa Majibu na Wizara husika[Sijui ni Ipi msaada?].
 
Ningeomba kumkumbusha Spika Ndugai kiapo alichokula, cha kuongoza bunge kwa kufuata kanuni na sheria za nchi.

Ningependa kumkumbusha Ndugai kuwa alikula kiapo hicho huku ameshika biblia na huku akilitaja jina la Mwenyezi Mungu...
Mtoa hoja kumbuka kuwa Mwenyekiti mwenyewe wa CHADEMA hajasema kitu ila wewe unakomaa. Acha ruzuku tuendelee kuipata kwani ofisi inafaa iendelee.
 
Back
Top Bottom