Spika Ndugai afunguliwa kesi ya kikatiba kwa kumtambua Mwambe kuwa Mbunge halali licha ya kujivua uanachama Chadema

Kama hakuna documents zozote zinazoonyesha Mh. Mwambe siyo mwanachadema tena basi hiyo kesi itapigwa chini kirahisi tu.

Kutegemea vyombo vya habari tu haisaidii lazima process ya kuondolewa uanachama kama ilivyo kwenye Katiba ya Chadema ifuatwe kama haikufuatwa basi hakuna kesi hapo. Hao wanasheria wanakula pesa za bure tu ama wanania ya kujitangaza ili wajulikane wapo!

Naamini Spika atakuwa alipata ushauri kwanza toka kwa Mwanasheria wa Bunge akiwemo Katibu wa Bunge ambaye naye ni mwanasheria kabla ya kuchukua uamuzi huo.
Watatumia sheria ya mtandao. Hii kesi inaweza weka taratibu mpya. Ngoja tuone.

Sent using iphone pro max
 
Bunge ni mhimili Spika hawezi kuhukumiwa na muhimili wa Mahakama.

Kesi hii ilipaswa kusikilizwa na kamati ya haki na maadili ya bunge na kwa kuwa anayelalamikiwa ni Spika basi kikao cha kamati kingeongozwa na Naibu Spika Dr Tulia!
Kesi hii ni muhimu sio kwa swala la mwambe tu bali, itasaidia pia kuuanika zaidi hata udhaifu wa katiba yetu uliyojificha.
 
Tawi la chadema kazini
Ni time.wastage na ku exhaust pesa za wafadhili.
Kisheria kama process ya kujivua uanachama haikukamilika huyo bado ni mbunge
Uhalali wa mbunge kukosa sifa,unatokana.na.mchakato kuwa halali,vinginevyo kama.mchakato ulikua,batili,status itatakiwa isomeke ni mbunge halali
Kama ilivyokuwa kwa Nyalandu.
 
Ubunge alisaini bungeni sio kwa bashiru, kuondoka ilibidi atoe taarifa bungeni tena sio kwa bashiru,
Kule kwa bashiru anaweza kusema alikuwa a act filamu utakataa?
Bashe hawezi kutoka Lumumba akaenda Ufipa kuigiza filamu never!

Na kile alichoutangazia umma kilikuwa ni nini?
Katiba ya Chadema inazungumza nini kuhusu kiongozi kukiuka miiko ya Chama?

Lazaro Nyalandu mbona yeye hakurudishwa na tena huyu alitangaza IG 😝😝
 
SURA YA KUMI NA MOJA MENGINEYO Maelezo ya mambo yanayohusika na madaraka ya Kazi mbalimbali zilizoanzishwa na Katiba hii Sheria za 1980 Na.1 ib.16; na Sheria ya 1984 Na.15 ib.52 Sheria ya 1992 Na.4 ib.37 149.-(1) Mtu yeyote mwenye dhamana ya kazi yoyote iliyoanzishwa na Katiba hii (pamoja na kazi ya Waziri, Naibu Waziri au Mbunge, isipokuwa Mbunge ambaye ni Mbunge kwa mujibu wa madaraka ya kazi yake, aweza kujiuzulu kwa kutoa taarifa iliyoandikwa na kutiliwa sahihi kwa mkono wake, kwa kufuata masharti yafuatayo: (a) iwapo mtu huyo aliteuliwa au alichaguliwa na mtu mmoja, basi taarifa hiyo ya kujiuzulu atawasilisha kwa mtu huyo aliyemteua au aliyemchagua, au iwapo aliteuliwa au alichaguliwa na kikao cha watu, basi taarifa hiyo ya kujiuzulu ataiwasilisha kwenye kikao hicho; (b) iwapo mtu huyo ni Rais, basi taarifa hiyo ya kujiuzulu ataiwasilisha kwa Spika; (c) iwapo mtu huyo ni Spika au Naibu wa Spika wa Bunge, basi taarifa hiyo ya kujiuzulu ataiwasilisha kwenye Bunge; na (d) iwapo mtu huyo ni Mbunge, basi taarifa hiyo ya kujiuzulu ataiwasilisha kwa Spika. (2) Mtu aliyetoa taarifa ya kujiuzulu kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (1) ya ibara hii, atahesabiwa kuwa amejiuzulu tangu siku ile ambayo taarifa yake ya kujiuzulu itakapopokelewa na mtu anayehusika au kikao kinachohusika na itakapopokelewa na mtu yeyote aliyeruhusiwa kuipokea taarifa hiyo na mtu anayehusika au kikao kinachohusika, lakini kama taarifa hiyo ya kujiuzulu imeeleza kwamba mtu huyo atajiuzulu tangu siku nyingine baada ya taarifa hiyo kupokelewa na mtu anayehusika au kikao kinachohusika, basi mtu huyo atahesabiwa kuwa amejiuzulu tangu siku hiyo nyingine ya baadaye.

sijui nitumie kifungu kidogo ''d'' na sheria Na 1 vinaweza kumpa ushindi spika kwa uelewa wangu mdogo
 
Bashe hawezi kutoka Lumumba akaenda Ufipa kuigiza filamu never!

Na kile alichoutangazia umma kilikuwa ni nini?
Katiba ya Chadema inazungumza nini kuhusu kiongozi kukiuka miiko ya Chama?

Lazaro Nyalandu mbona yeye hakurudishwa na tena huyu alitangaza IG 😝😝

Nyarandu anatamani kurudi ila hajui aanzie wapi, na uchaguzi ukiisha unaweza msikia karudi ubelgiji,
kuhusu katiba ya chadema walitakiwa kuandika barua kwa spika kumjulisha kuwa sasa huyo sio.mbunge wao, lakini wakakaa kimya walipomuona bungeni ndo wanastuka kumbe kumekucha.
 
MWAMBE-NDUGAI.jpg

WAKILI wa Mahakama Kuu ya Tanzania amefungua kesi ya kikatiba dhidi ya Spika wa Bunge Job Ndugai (MB) na aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Ndanda kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Cecil Mwambe, na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Katika kesi hiyo ya kikatiba namba 10 ya mwaka 2020, Wakili Paul Kaunda anaiomba Mahakama Kuu kutengua amri ya spika ya kumtambua Mwambe kama mbunge halali, ilhali mbunge huyo (Mwambe) aliushautangazia umma kwamba amejivua uanachama wa Chadema na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Kaunda amesema, kitendo cha spika kumtambua Mwambe kama mbunge halali wakati ameshajivua uanachama wa chama kilichomdhamini ni ukiukwaji wa ibara ya 71(1)(f) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977, na hakuna mamlaka yoyote nchini, yenye uwezo wa kumrudisha bungeni mbunge ambaye kwa hiari yake mwenyewe ameamua kujivua uanachama wa chama cha siasa kilichomdhamini kupata ubunge.

Kesi hiyo ya kikatiba imepangwa kusikilizwa Mei 21, 2020 na jopo la majaji watatu litakaloongozwa na Jaji Issa Maige. Majaji wengine ni Stephen Kirimi Magoiga na Seif Kulita.

Katika kesi hiyo, atawakilishwa na jopo la mawakili sita litakaloongozwa na Wakili Mwandamizi Mpale Mpoki akisaidiwa na mawakili Daimu Halfani, Fulgence Massawe, Prisca Chogero, Stephen Msechu pamoja na Stephen Ally Mwakibolwa.

Credit: LHRC.

Ntamani ningekuwa tz nije kumwakilishwa mahakamani Cecil Mwambe bure, ningefanya pro borno kabisa wallah
 
Safi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo mahakama itapewa maagizo jinsi ya kuamua hiyo kesi. Sioni mahakama ya kuenda kinyume na genge la watawala.
kuna kifungu cha katiba kinampa ushindi spika,hivyo ni vizuri wananchi kujenga mazoea ya kusoma katiba na kuielewa
 
Marichris said:
Ntamani ningekuwa tz nije kumwakilishwa mahakamani Cecil Mwambe bure, ningefanya pro borno kabisa wallah
Huyo "bulai" sasa ale jeuri yake!
 
Mahakama ya kibiongo huogopa bonge kisa kuambiwa imeingilia mhimili mwingine!!
Ogopa kunamhimili mkuu wake alisema mahakama hata ikihukumu tofauti na alivyoagiza yeye polisi niwakwake haiwezi kuwatuma kwenda kutekeleza hukumu. Viongozi wa ajabu hawa wanaidharau katiba na sheria sijui haki itatolewa wapi!!
Iwapo amemlipa allowances ama mishahara spika ashtakiwe kwauhujumu uchumi,fojari,matumizi mabaya ya ofisi,kuvunja katiba nk.
Kiongozi hajali hata kiapo chake cha hadharani mbele ya watz huku kashika biblia na kulitaja jina la bwana kwamba "nitailinda na kuitetea katiba ... eeh bwana unisaidie"??
 
Wanashinda mchana kweupe!
Watashindwa kwa agizo toka juu kama tulivyozoea kuona kesi nyingi zinazohusu wapinzani zikishindwa mapema kweupe na mahakimu kupandishwa vyeo na mamlaka ya juu kama zawadi kwa kazi nzuri. Awamu hii haina habari na Katiba wala Utawala wa Sheria katika kuongoza nchi, bunge na mahakama ni idara tu za mamlaka ya uamuzi. Kill red-handed and the dead will be punished for getting killed by an untouchable.
 
MWAMBE-NDUGAI.jpg

WAKILI wa Mahakama Kuu ya Tanzania amefungua kesi ya kikatiba dhidi ya Spika wa Bunge Job Ndugai (MB) na aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Ndanda kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Cecil Mwambe, na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Katika kesi hiyo ya kikatiba namba 10 ya mwaka 2020, Wakili Paul Kaunda anaiomba Mahakama Kuu kutengua amri ya spika ya kumtambua Mwambe kama mbunge halali, ilhali mbunge huyo (Mwambe) aliushautangazia umma kwamba amejivua uanachama wa Chadema na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Kaunda amesema, kitendo cha spika kumtambua Mwambe kama mbunge halali wakati ameshajivua uanachama wa chama kilichomdhamini ni ukiukwaji wa ibara ya 71(1)(f) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977, na hakuna mamlaka yoyote nchini, yenye uwezo wa kumrudisha bungeni mbunge ambaye kwa hiari yake mwenyewe ameamua kujivua uanachama wa chama cha siasa kilichomdhamini kupata ubunge.

Kesi hiyo ya kikatiba imepangwa kusikilizwa Mei 21, 2020 na jopo la majaji watatu litakaloongozwa na Jaji Issa Maige. Majaji wengine ni Stephen Kirimi Magoiga na Seif Kulita.

Katika kesi hiyo, atawakilishwa na jopo la mawakili sita litakaloongozwa na Wakili Mwandamizi Mpale Mpoki akisaidiwa na mawakili Daimu Halfani, Fulgence Massawe, Prisca Chogero, Stephen Msechu pamoja na Stephen Ally Mwakibolwa.

Credit: LHRC.
Awamu ya 5 inatia aibu mno !
 
Back
Top Bottom