Spika Ndugai afunguliwa kesi ya kikatiba kwa kumtambua Mwambe kuwa Mbunge halali licha ya kujivua uanachama Chadema

Wanashinda mchana kweupe!
Hii kesi inafanana na kesi ya Mwenyekiti wa CUF, prof Lipumba kujivua uenyekiti CUF Kwa maneno, na Chama kutofuata katiba yake kwa wakati. Mwisho akarudi mkibaki mnalalama.
Kila kitu kina taratibu na sheria . Tatizo vyama vyetu vina- katiba lakini havifuati.
Vyama vya kihuni! Heri zimwi likujualo.
Tunahitaji kuona mbadala ulio bora zaidi ya Ccm. Sio huu wakihuni usio fuata hata katiba na taratibu zao walizojiwekea wenyewe. Je katba ya TZ wataiweza?
Wabunge walitangaza kwamaneno kujitoa, je chama kilichukua hatua gani?
Katiba ya chama inasemaje kuhusu mtu anaetangaza kuhama, je baada yakutangaza ndio anakuwa kahama kweli? Wapinzani bongo ni wajasiliasiasa tu. Natamani kusikia tena hoja za kisiasa na ushawishi km za Dr Slaa. 'hazina yetu iliyopigwa teke!
 
MWAMBE-NDUGAI.jpg

WAKILI wa Mahakama Kuu ya Tanzania amefungua kesi ya kikatiba dhidi ya Spika wa Bunge Job Ndugai (MB) na aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Ndanda kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Cecil Mwambe, na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Katika kesi hiyo ya kikatiba namba 10 ya mwaka 2020, Wakili Paul Kaunda anaiomba Mahakama Kuu kutengua amri ya spika ya kumtambua Mwambe kama mbunge halali, ilhali mbunge huyo (Mwambe) aliushautangazia umma kwamba amejivua uanachama wa Chadema na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Kaunda amesema, kitendo cha spika kumtambua Mwambe kama mbunge halali wakati ameshajivua uanachama wa chama kilichomdhamini ni ukiukwaji wa ibara ya 71(1)(f) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977, na hakuna mamlaka yoyote nchini, yenye uwezo wa kumrudisha bungeni mbunge ambaye kwa hiari yake mwenyewe ameamua kujivua uanachama wa chama cha siasa kilichomdhamini kupata ubunge.

Kesi hiyo ya kikatiba imepangwa kusikilizwa Mei 21, 2020 na jopo la majaji watatu litakaloongozwa na Jaji Issa Maige. Majaji wengine ni Stephen Kirimi Magoiga na Seif Kulita.

Katika kesi hiyo, atawakilishwa na jopo la mawakili sita litakaloongozwa na Wakili Mwandamizi Mpale Mpoki akisaidiwa na mawakili Daimu Halfani, Fulgence Massawe, Prisca Chogero, Stephen Msechu pamoja na Stephen Ally Mwakibolwa.

Credit: LHRC.
Mwambe ajiandae kurejesha pesa za umma. Asipoweza ndugai atamlipia.
Spika amezoea kufuja fedha za umma.
Waswahili tunasema "usirushe mawe wakati umo kwenye nyumba ya kioo".
Aliwabana wabunge wa cdm aliokuwa kwenye karantini ya hiari kama vile walikuwa hawakulipwa kwa taratibu za bunge.
 
Nyarandu anatamani kurudi ila hajui aanzie wapi,
Ina maana wewe unajua afanye nini ili arudi bungeni mtu ambaye hujawahi kuwa hata kuwa kiranja wa chooni shule na yeye ambaye amewahi kuwa kada wa CCM kwa miaka mingi, mbunge na waziri hajui? duuuh!

na uchaguzi ukiisha unaweza msikia karudi ubelgiji,
Haituhusu.

kuhusu katiba ya chadema walitakiwa kuandika barua kwa spika kumjulisha kuwa sasa huyo sio.mbunge wao, lakini wakakaa kimya walipomuona bungeni ndo wanastuka kumbe kumekucha.
Nipe ushahidi wa barua ya CHADEMA kwenda kwa spika kuwa Mwambe si mwanachama wao baada ya Lispika kumuita Bungeni.

Pia nipe ushahidi wa barua ya ccm kwenda bungeni ikieleza Nyalandu si mwanachama wao tena.

Kumbuka, Nyalandu alijitoa Instagram na ubunge wake ulikoma siku ileile, Mwambe aliitisha press Conference na ubunge wake ulikoma siku ileile ndio maana hakurejea bungeni!

Hivi wewe shule ulienda kusomea nini?
 
Hii kesi inafanana na kesi ya Mwenyekiti wa CUF, prof Lipumba kujivua uenyekiti CUF Kwa maneno, na Chama kutofuata katiba yake kwa wakati. Mwisho akarudi mkibaki mnalalama.
Kila kitu kina taratibu na sheria . Tatizo vyama vyetu vina- katiba lakini havifuati.
Vyama vya kihuni! Heri zimwi likujualo.
Tunahitaji kuona mbadala ulio bora zaidi ya Ccm. Sio huu wakihuni usio fuata hata katiba na taratibu zao walizojiwekea wenyewe. Je katba ya TZ wataiweza?
Wabunge walitangaza kwamaneno kujitoa, je chama kilichukua hatua gani?
Katiba ya chama inasemaje kuhusu mtu anaetangaza kuhama, je baada yakutangaza ndio anakuwa kahama kweli? Wapinzani bongo ni wajasiliasiasa tu. Natamani kusikia tena hoja za kisiasa na ushawishi km za Dr Slaa. 'hazina yetu iliyopigwa teke!
So kwa akili zako unaweza kutuambia kwanini baada ya Mwambe kutangaza kujitoa Chadema hakurejea tena bungeni hadi alipoitwa?

Unaweza kuniambia waliopita kama Waitara, Molleli na wengineo kwanini baada ya kujitoa walichaguliwa upya?

Ina maana wewe unajua sana sheria za bunge, vyama vya siasa na CHADEMA ambao wako ndani ya huo mchezo hawajui lakufanya? Hahaha haki Tanzania sirudi i better die in America
 
Je hukumu ya mvunja katiba ninini?
Hawa walitakiwa kunyongwa kabisa au kifungo cha maisha gerezani. Kama hakuna hukumu matokeo ya watu hawa wataendelea na kuvunja katiba.
Utawala wa wapenda haki kama Mungu jalia basi watunge sheria hiyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mahakama hizi haziaminiki hata kidogo,natabili hukumu itatolewa kuwa mahakama imeogopa kugongana na maamuzi ya muhimili wa bunge
 
So kwa akili zako unaweza kutuambia kwanini baada ya Mwambe kutangaza kujitoa Chadema hakurejea tena bungeni hadi alipoitwa?

Unaweza kuniambia waliopita kama Waitara, Molleli na wengineo kwanini baada ya kujitoa walichaguliwa upya?

Ina maana wewe unajua sana sheria za bunge, vyama vya siasa na CHADEMA ambao wako ndani ya huo mchezo hawajui lakufanya? Hahaha haki Tanzania sirudi i better die in America

Maamuzi ya spika kumuita mwambe ni pale alipoona udhaifu wa vyama kutofata sheria na kanuni, hapo anawakumbusha wasome katiba zao vizuri wazielewe wasiwe wanasubiri huruma, linapotokea jambo wawe wanachukua hatua mapema, kumbuka Pf Ripumba na CUF.
 
Tusubiri maamuzi ila sioni mantiki ya kesi. Huyo amechaguliwa na Wananchi

Ujinga ni mzito mkubwa sana. Kwani ukiondoa wabunge wa kuteuliwa na Rais, wabunge wengine hawakuchaguliwa na wananchi??

Walio na uelewa wa sheria na taratibu zinasema nini tunataka tafsiri ya mambo hayo kutoka mahakamani. Ili siku nyingine mbunge akijiuzulu chama tujue kama utaratibu wa Mwambe utaendelea.

Mantiki ya kesi ni hii - wabunge wote waliojiuzulu kutoka vyama vyao, walistahili kuwa bungeni sasa??? Au hili la Mwambe limefanyika kwa sababu CCM hawezi kuitisha uchaguzi mdogo na kufaidi kupata mbunge mwingine?

Kesi hii inaenda kuweka sawa swala la udhamini wa chama. Tungekuwa tunajali sana - chama cha siasa kilichoshinda kingekuwa kinatoa mbunge bila kuhitaji uchaguzi mdogo ktk kipindi cha miaka mitano - kwa sababu yoyote ile. Pesa za uchuguzi mdogo ni nyingi sana na tungeepuka matumizi ya namna hiyo.
 
So kwa akili zako unaweza kutuambia kwanini baada ya Mwambe kutangaza kujitoa Chadema hakurejea tena bungeni hadi alipoitwa?

Unaweza kuniambia waliopita kama Waitara, Molleli na wengineo kwanini baada ya kujitoa walichaguliwa upya?

Ina maana wewe unajua sana sheria za bunge, vyama vya siasa na CHADEMA ambao wako ndani ya huo mchezo hawajui lakufanya? Hahaha haki Tanzania sirudi i better die in America
Ina maana wewe unajua sana sheria za bunge kuliko spika wa bunge?
Kwa akili hiyo ya mihemko ni kweli bora ufie huko huko kwa mabeberu.
Huku tunahitaji watu makini wasio na mihemko.
 
Kwamba katika utetezi atasema, yeye bado ni mwanachadema na atakana kujiondoa chamani?!

Ok...nimekumbuka lipumba!

Ngoja tuone hii itakuwaje"
... tatizo ni ushahidi kwamba Mwambe alishajivua uanachama wa chama kilichomdhamini; shida iko kwenye ku-prove hilo. Kumbuka Ofisi ya Spika haindeshi mambo yake kupitia taarifa za media; inaendeshwa kwa taratibu na nyaraka rasmi za kiofisi.

Hivyo hata kama Mwambe alionekana majukwaani akijivua uanachama wa Chadema bado hiyo sio basis ya Ofisi ya Spika ku-rule out kwamba sio mbunge kwani majukwaa ya kisiasa sio official kwa maamuzi rasmi ya kiofisi kufanyika. Kwa Mfano, Spika angeiandikia NEC kwamba Jimbo la Mwambe liko wazi based on what evidence? Kwamba alionekana akikabidhiwa kadi ya CCM na Bashiru? Hicho kitu hakipo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MWAMBE-NDUGAI.jpg

WAKILI wa Mahakama Kuu ya Tanzania amefungua kesi ya kikatiba dhidi ya Spika wa Bunge Job Ndugai (MB) na aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Ndanda kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Cecil Mwambe, na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Katika kesi hiyo ya kikatiba namba 10 ya mwaka 2020, Wakili Paul Kaunda anaiomba Mahakama Kuu kutengua amri ya spika ya kumtambua Mwambe kama mbunge halali, ilhali mbunge huyo (Mwambe) aliushautangazia umma kwamba amejivua uanachama wa Chadema na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Kaunda amesema, kitendo cha spika kumtambua Mwambe kama mbunge halali wakati ameshajivua uanachama wa chama kilichomdhamini ni ukiukwaji wa ibara ya 71(1)(f) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977, na hakuna mamlaka yoyote nchini, yenye uwezo wa kumrudisha bungeni mbunge ambaye kwa hiari yake mwenyewe ameamua kujivua uanachama wa chama cha siasa kilichomdhamini kupata ubunge.

Kesi hiyo ya kikatiba imepangwa kusikilizwa Mei 21, 2020 na jopo la majaji watatu litakaloongozwa na Jaji Issa Maige. Majaji wengine ni Stephen Kirimi Magoiga na Seif Kulita.

Katika kesi hiyo, atawakilishwa na jopo la mawakili sita litakaloongozwa na Wakili Mwandamizi Mpale Mpoki akisaidiwa na mawakili Daimu Halfani, Fulgence Massawe, Prisca Chogero, Stephen Msechu pamoja na Stephen Ally Mwakibolwa.

Credit: LHRC.

Good move.
Tunasubiri Leo.

Long live huyo wakili!!!

Nampa Kongole Wakili msomi Paul Kaunda. Hii ndiyo akili inayoweza kufanya Reformation ya Sheria na Mambo ya kijinga yayayofanyika ndani ya nji hii!

CHADEMA wako wapi katika hili? Wao ndio walitakiwa wawe wa kwanza kumshtaki Spika Ndugai kwa kuvunja Katiba ya JMT kwa kumrudisha Cecil Mwambe Bungeni kupitia mgongo wa CHADEMA wakti huyu jamaa ni MWANACHAMA WA CCM!

Watz tunajua jinsi Sheria na Katiba ya Tanzania inavyochezewa na kupindishwa tangu Magufuli awe Rais wa nji hii. Yote hii Ni jeuri ya kipengele Cha kihuni kwenye Katiba yetu kinachomlinda Rais kutoshtakiwa kwa MAKOSA yoyote aliyofanya akiwa Mkuu wa nji!

Kesi hii inaweza kumfanya Spika Job Ndugai kurudi kwene mstari! Lakini Magufuli katika kesi hii kwa HULKA yake anaweza kutoa maelekezo/maagizo kwa Majaji watoe hukumu kinyume na matarajio ya wengi ya kumtia hatiani Spika Ndugai katika juhudi za kumnusuru/kumlinda!
 
Spika anasumbua majaji...hii kesi hata mimi naiamua tu fastaa ipo wazi..

Haya ma vyama na maitikadi yasituharibie umoja wetu na kutuvunjia katiba yetu.

CCM nyie ni wakongwe badala ya kuvisimamia vyama hivyo vinavyokua nyie ndio wagwiji wa kuibaka katiba.

Msiwasumbue Majaji, Mawakili na sisi watanzania kwa mambo yasiyo ya msingi.
 
... tatizo ni ushahidi kwamba Mwambe alishajivua uanachama wa chama kilichomdhamini; shida iko kwenye ku-prove hilo. Kumbuka Ofisi ya Spika haindeshi mambo yake kupitia taarifa za media; inaendeshwa kwa taratibu na nyaraka rasmi za kiofisi.

Hivyo hata kama Mwambe alionekana majukwaani akijivua uanachama wa Chadema bado hiyo sio basis ya Ofisi ya Spika ku-rule out kwamba sio mbunge kwani majukwaa ya kisiasa sio official kwa maamuzi rasmi ya kiofisi kufanyika. Kwa Mfano, Spika angeiandikia NEC kwamba Jimbo la Mwambe liko wazi based on what evidence? Kwamba alionekana akikabidhiwa kadi ya CCM na Bashiru? Hicho kitu hakipo.
Mwambe mwenyewe alijua kwamba alishajivua ubunge baada ya kuhama chama kilichomdhamini ndiyo maana hakurudi bungeni,mpaka alipoitwa na Ndungai.
Chadema walimwandikia spika wakimjulisha kuwa Mwambe sio mwanachama wao kwa vile amejiunga na CCM,lakini Ndungai akasema haitambui kwa vile haina viambatanisho ilihali alitambua barua kama hizo alizoandikiwa kuhusu wabunge wa Chadema waliounga mkono juhudi za mkulu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama hakuna documents zozote zinazoonyesha Mh. Mwambe siyo mwanachadema tena basi hiyo kesi itapigwa chini kirahisi tu.

Kutegemea vyombo vya habari tu haisaidii lazima process ya kuondolewa uanachama kama ilivyo kwenye Katiba ya Chadema ifuatwe kama haikufuatwa basi hakuna kesi hapo. Hao wanasheria wanakula pesa za bure tu ama wanania ya kujitangaza ili wajulikane wapo!

Naamini Spika atakuwa alipata ushauri kwanza toka kwa Mwanasheria wa Bunge akiwemo Katibu wa Bunge ambaye naye ni mwanasheria kabla ya kuchukua uamuzi huo.
Wasomi wa Tz ni kama nyani tu,ila hawana mkia.

Mtu na akili zake anajua wazi kwamba mtu kujivua uanachama wa chama cha siasa anakosa sifa ya kuwa mbunge,unalazimishaje aendelee kuwa mbunge ili hali hana chama kilichomdhamini.
Tulikuta msomi uchwara itakuwa ni tusi kwako?

Watu wanaumwa corona,wewe unapima wanyama na matunda,tukupe jina gani linalolingana na sifa yako?

Tukikosea kupewa uhuru mapema,ilikuwa tupate uhuru mwaka 2030

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom