Spika Ndugai afunguliwa kesi ya kikatiba kwa kumtambua Mwambe kuwa Mbunge halali licha ya kujivua uanachama Chadema

... Spika anashtakiwa kwa kuvunja Katiba (jinai kuu) sio makosa ya mijadala ndani ya Bunge bwasheee elewa somo kwanza.
Ni nani kati ya wafuatao aliyemwandikia rasmi Spika kwamba Mwambe amejiuzuru
1. Mwambe
2. CHADEMA
3. Msajili wa vyama vya siasa
4. Tume ya uchaguzi
5. CCM
 
Ni nani kati ya wafuatao aliyemwandikia rasmi Spika kwamba Mwambe amejiuzuru
1. Mwambe
2. CHADEMA
3. Msajili wa vyama vya siasa
4. Tume ya uchaguzi
5. CCM
1. Mwambe asingeweza kufanya hivyo kwa sababu most likely alikuwa anawatega Chadema.
2. Chadema; based on what ground? Hii nayo ngumu.
3. Msajili; hahusiki na issues za wabunge kubadili vyama.
4. NEC; wao hupewa taarifa na sio mtoa taarifa kwa taarifa za aina hiyo.
5. CCM; lao na Mwambe moja; kuitega Chadema.
 
Kwanza tuanze ligi aliitamkia wapi? Bungeni ana immunity Huwezi chukulia chochote serious Cha bungeni Wana kinga ndio.maana hata chadema hawana ubavu wa kufukuza uanachama wabunge wao waliokuwa bungeni !!! High profile case unatakiwa kujipanga waweza ua jina lako la uwakili forever!! Ukishindwa
Haya walitamka wPi huyu wakili Koko yuko silent!!!!! Mengine nitamshukia Kama mwewe ajibu hili kwanza
 
1. Mwambe asingeweza kufanya hivyo kwa sababu most likely alikuwa anawatega Chadema.
2. Chadema; based on what ground? Hii nayo ngumu.
3. Msajili; hahusiki na issues za wabunge kubadili vyama.
4. NEC; wao hupewa taarifa na sio mtoa taarifa kwa taarifa za aina hiyo.
5. CCM; lao na Mwambe moja; kuitega Chadema.
Basi Mwambe bado ni Mbunge!
 
..watapiga danadana na mwisho wake watatoa uamuzi ambao unainajisi mahakama.

..mimi nawashauri mawakili wafute kesi hiyo, ili waiepushe mahakama yetu kufanya maamuzi ya hovyo.

.

We ndo hujui, hiyo taasisi imekosa weledi imebaki kama chama cha siasa, mahakama itawaomba barua ya mwambe kujivua uanachama kwenda chadema, watakoswa, barua ya mwambe kwenda kwa spika wa bunge hawana, barua ya maamuzi ya chama kwenda kwa spika au msajiri hawana, hapo itatupiliwa mbali,
 
Hata wanaweza wasihangaike kufukunyua barua za Chadema, ni very easy kupata ushahidi tena wa picha tu hata haisumbui akili.

Bashiru anapomkabidhi Mwambe Kibogoyo kadi za CCM huwezi kupokea kadi za chama A ilihali wewe bado ni mwanachama wa chama B!

Ubunge alisaini bungeni sio kwa Bashiru, kuondoka ilibidi atoe taarifa bungeni tena sio kwa Bashiru,
Kule kwa Bashiru anaweza kusema alikuwa a act filamu utakataa?
 
Tusubiri maamuzi ila sioni mantiki ya kesi. Huyo amechaguliwa na Wananchi
Dah... una kazi kaka... kwani katiba inasemaje? Unakumbuka Mrema alifanyiwa nini alipohama chama..?? Unajua alinyang'anywa nini mara tu baada ya kutangaza kuhama CCM?
 
Ubunge alisaini bungeni sio kwa bashiru, kuondoka ilibidi atoe taarifa bungeni tena sio kwa bashiru,
Kule kwa bashiru anaweza kusema alikuwa a act filamu utakataa?

..hudhani kwamba kuiheshimu na kuihifadhi katiba ni muhimu kuliko kulazimisha maamuzi ya spika yasiyo na busara?
 
..hudhani kwamba kuiheshimu na kuihifadhi katiba ni muhimu kuliko kulazimisha maamuzi ya spika yasiyo na busara?

Sheria inaenda kwa kufata kanuni haifuati utashi wa mtu au huruma,
Ukikosea tu unashindwa, vielelezo wanavyo? Kumbuka mwambe aliapa mbele ya bunge kuchukua dhamana ya jimbo hakuapa kwa Bashiru.
Hivyo.pale bungeni alikuwa ni mtoro tu.
 
MWAMBE-NDUGAI.jpg

WAKILI wa Mahakama Kuu ya Tanzania amefungua kesi ya kikatiba dhidi ya Spika wa Bunge Job Ndugai (MB) na aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Ndanda kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Cecil Mwambe, na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Katika kesi hiyo ya kikatiba namba 10 ya mwaka 2020, Wakili Paul Kaunda anaiomba Mahakama Kuu kutengua amri ya spika ya kumtambua Mwambe kama mbunge halali, ilhali mbunge huyo (Mwambe) aliushautangazia umma kwamba amejivua uanachama wa Chadema na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Kaunda amesema, kitendo cha spika kumtambua Mwambe kama mbunge halali wakati ameshajivua uanachama wa chama kilichomdhamini ni ukiukwaji wa ibara ya 71(1)(f) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977, na hakuna mamlaka yoyote nchini, yenye uwezo wa kumrudisha bungeni mbunge ambaye kwa hiari yake mwenyewe ameamua kujivua uanachama wa chama cha siasa kilichomdhamini kupata ubunge.

Kesi hiyo ya kikatiba imepangwa kusikilizwa Mei 21, 2020 na jopo la majaji watatu litakaloongozwa na Jaji Issa Maige. Majaji wengine ni Stephen Kirimi Magoiga na Seif Kulita.

Katika kesi hiyo, atawakilishwa na jopo la mawakili sita litakaloongozwa na Wakili Mwandamizi Mpale Mpoki akisaidiwa na mawakili Daimu Halfani, Fulgence Massawe, Prisca Chogero, Stephen Msechu pamoja na Stephen Ally Mwakibolwa.

Credit: LHRC.
Ndugai anatakiwa kufungwa kwa matumizi mabaya ya fedha za umma,kitendo cha kuendelea kumlipa mwambe mshahara na marupurupu wakati alishajivua uanachama ni makosa!! Hata mahakama ikitengua ubunge wa mwambe inabidi spika naye ashitakiwe kwa matumizi mabaya ya ofisi za umma...hiyo ni uhujumu uchumi.
 
Back
Top Bottom