Spika Job Ndugai: Matatizo yetu na Prof. Mussa Assad ni kutuita dhaifu, alitakiwa ajiuzulu. Hatuna tatizo na ripoti yake, tutaifanyia kazi

Kwa watu makini wanajua Report ya CAG ndio kitu kilichotawala week hii yote lakini pia kuna ufisadi wa kutisha ndani ya Report Ile.

Zitto katoa takwimu za uhakika kwamba pesa zaidi ya 4.6 trion zilitumika kiholela...

Pia ameonyesha jinsi gani ambavyo CAG kaogopa kiasi kusema kwamba pesa zaidi ya bilion 800 zimechotwa na kupotea.

Huu ni mkakati wa Serikali kumtumia Job Ndungai ili sisi tuendelee kum discuss yeye na kuacha report ya CAG..

Jamani tuache siasa za matukio serikali waje na majibu ya maana kutokana na Report ya CAG ambayo inaonyesha kuna ufisadi wa kutisha kuliko report zote kuanzia mwaka 1961 tulipopata uhuru.

Bilion 800 zipo wapi ? Pesa ya kujenga shule zaidi ya 800 za bilion 1 nchi nzima ma kununua madawati zinapotea bila kujibiwa zipo wapi halafu tunaenda kufatilia upuuzi wa job Ndungai?.

Ili kuzima mjadala lazima kwanza pesa zetu zijulikane zilipo bilion 800 ukiunganisha na Ile 2.4 trion tutakuwa tumepoteza pesa zaidi ya trion 3.2 ndani ya miaka 2 je baada ya miaka 10 tutakuwa tumepoteza pesa kiasi gani..

Serikali ya kifisadi,Bunge dhaifu CAG ndiye mshindi kwa hili

Jibuni hoja za CAG kwanza .
 
Apathy
Hakuniongezei kitu. Vipi we kunakuongezea nn?

We think too small, like the frog at the bottom of the well. He thinks the sky is only as big as the top of the well. If he surfaced, he would have an entirely different view.
 
Spika wa Bunge Job Ndugai, leo Aprili 14 atazungumza na waandishi wa habari jambo muhimu kuhusu bunge.

Mazungumzo hayo yatafanyika katika ofisi ndogo ya bunge jijini Dar es salaam majira ya saa sita na nusu mchana.


=====

UPDATES:

View attachment 1071319

=> Spika Ndugai: CAG anaposema mbele ya umma kuwa ataendelea kutuita 'dhaifu' wakati ni jina ambalo hatulipendi na tumelikataa, tunashindwa kumuelewa kama analipenda sana ajiite yeye. Sasa kusema unaendelea kutumia endelea na nitakuita tena na safari hii itakuwa mbaya zaidi"

=> Spika Ndugai: "Namwambia ndugu yangu Prof. Assad hilo neno aliache, sisi taarifa tumeipata na tutaifanyia kazi. Msisitizo wetu ni mmoja, kwakuwa bunge lilishapitisha uamuzi wa kutofanya kazi na Prof. Assad ni uamuzi halali"


=> Spika Ndugai: "Sina chuki binafsi na Prof. Assad, yule ni ndugu yangu na ni mtanzania mwenzangu tatizo ni lugha anayoitumia na nisinhependa itufikishe hapa kama taifa."

=> Spika Ndugai: "Tunataka tumuoneshe Prof. Assad kuwa Bunge halichezewi, simuelekezi kazi ila anatakiwa ajiongeze kama ni kujiuzulu au laaa!. Maana tushamwambia hatumtaki, anavyoendelea kubaki ofisini ni kumpa tu wakati mgumu Rais

=> Spika Ndugai: Zipo njia za kumaliza mambo kama haya, mojawapo aende kwa Rais akajieleze kwamba mimi nimepima nimeona nimekosea hapa na pale. Maana Rais ni sehemu yetu sisi (Bunge) hatuwezi kupitisha sheria bila yeye kupitisha mkono wake,

=> Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai amewahakikishia watanzania kuwa bunge linaendelea vizuri na kazi yake ya kutunga sheria, uwakilishi, kuisimamia Serikali pamoja na mipango ya nchi ikiwemo suala la bajeti ambalo linaendelea bungeni.

=> Spika Ndugai:“Sasa kumekuwa na ufafanuzi usiokuwa sawa sawa, kilichowekwa mezani ni ‘Audit Queries’ …kilichowekwa mezani sio ukweli wenyewe kwamba aliyetajwa mule sasa huyo mwizi… ‘Audit queries’ zile zikishawekwa mezani kazi yetu ni kuwaita mezani na kuwasikiliza

=> Spika Ndugai:Tunataka tumuoneshe Prof. Assad kuwa Bunge halichezewi, simuelekezi kazi ila anatakiwa ajiongeze kama ni kujiuzulu au la! maana tushamwambia hatumtaki, anavyoendelea kubaki ofisini ni kumpa tu wakati mgumu Rais

=> Spika Ndugai:Hatuna tatizo na ripoti ya CAG…tatizo letu ni maneno ambayo Profesa Mussa Juma Assad ameyatoa akiwa Marekani, na alipoita waandishi akarudia tena, maneno yale sie tumeyakataa sio ya kistaarabu.

=> Spika Ndugai:Sisi kama Bunge hatutaki hilo neno dhaifu, kwa sababu Bunge kama Bunge halifanyiwi tathmini na ofisi ya CAG ila wanaofanyiwa tathmini ni watendaji wa Ofisi hiyo hivyo hawakupaswa kudhihakiwa na lugha hiyo inayotajwa kuwa ya kihasibu.

=> Spika Ndugai: “Hata katika maisha ya kawaida, we unamuita mtu jina flani, anakwambia bwana tafadhali jina hili silipendi, lakini unaendelea kumuita na kuahidi utaendelea kulitumia, ni ustaarabu duniani?”

=> Spika Ndugai: “Katika kutekeleza majukumu yake #CAG hakupaswa na hapaswi kulitukana #Bunge kwa lugha zile za rejareja. Bunge huangalia taratibu zake na kuendesha mambo yake kufuatana na kanuni za Bunge…lile Bunge lenyewe hawezi kulikagua”

=> Spika Ndugai: Hatuna tatizo na ripoti ya CAG…tatizo letu ni maneno ambayo Profesa Mussa Juma Assad ameyatoa akiwa Marekani, na alipoita waandishi akarudia tena, maneno yale sie tumeyakataa sio ya kistaarabu.

=> Spika Ndugai: “Sasa kumekuwa na ufafanuzi usiokuwa sawa sawa, kilichowekwa mezani ni ‘Audit Queries’ …kilichowekwa mezani sio ukweli wenyewe kwamba aliyetajwa mule sasa huyo mwizi… ‘Audit queries’ zile zikishawekwa mezani kazi yetu ni kuwaita mezani na kuwasikiliza”

"Nilipokuwa sipo kuna mambo mengi yamezungumzwa, na mengine yameandikwa kuhusu Ripoti ya CAG. Nitakapokuwa Dodoma nitaagiza ripoti ipelekwe kwenye kamati za PAC na LAC"




Zaidi soma.....

Dar es Salaam. Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amemshauri Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad akamwone Rais John Magufuli ili mzozo wake na Bunge uishe.

Kauli ya Spika inakuja wakati tayari Bunge limeshapitisha azimio la kutofanya kazi na Profesa Assad bali ofisi ya CAG.

Spika Ndugai aliyekuwa ziarani nchini Sweden wiki iliyopita ameyasema hayo leo Jumapili Aprili 14, 2019 akieleza kusikitishwa na hatua ya Profesa Assad kurudia neno udhaifu kwa Bunge alipotoa taarifa yake hivi karibuni.

"Zipo njia za kumaliza mambo kama haya, mojawapo aende kwa Rais akajieleze kwamba mimi nimepima nimeona nimekosea hapa na pale. Maana Rais ni sehemu yetu sisi (Bunge) hatuwezi kupitisha sheria bila yeye kupitisha mkono wake," alisema Ndugai.

Ameongeza kuwa hata bajeti inayojadiliwa na Bunge lazima ipitishwe na Rais. Amesema kwa kuwa Bunge limeshapitisha azimio la kutofanya kazi na Profesa Mussa Assad alitakiwa ajiuzulu.

"Kwa kuwa Bunge likishaaamua kuwa halifanyi kazi na mtu, ni uamuzi halali. Katika nchi zote Bunge likishakosa imani na wewe unajiuzulu," amesema.

Ameongeza, "Sasa hatumfundishi kazi Mussa Assad, anampa wakati mgumu Rais tu. Tutafanya kazi na ofisi ya wananchi."

Spika Ndugai amemsifu Profesa Assad kwa ujasiri wake huku akiufananisha na ujasiri wa mbwa kumtukana mtu anayemlisha.

"Unatukana hadi mkono unaokulisha, inahitaji ujasiri na jamaa ana ujasiri. Ila ni ujasiri ule wa mbwa anayemtukana anayemlisha," amesema.

Hata hivyo, Ndugai amesema hana chuki binafsi na Assad bali tatizo ni lugha tu aliyotumia ya kuliita Bunge dhaifu.


KAMA PROF. ASSAD HATAKI KUJIUZURU, BASI NDUNGAI JIUZURU.

PROF. ASSAD NIMUHIMU SANA KULIKO HUO UDHAIFU, TENA NI LULU YA TAIFA
MKWELI NA MUWAZI.TAALUMA NA SIASA VITU VIWILI TOFAUTI.
 
Mkuu naheshimu maoni yako,basi huna budi pia kuheshimu hisia zangu,
Unaomba arudishe roho, hivi unadhani nani kapanic hapa.hakuna aliepanic.


Unamkwazaje mtu kwa kumwambia ukweli kuwa huu ni udhaifu.

Usitake kuamsha hasira za watu.

Tumekaa kimya msidhani kwamba sisi wananchi ni wapumbavu.


Nina rafiki zangu wakristu na waislam wanateseka ka sababu ya maaazimio ya kipumbavu yaliyopitishwa na hilo BUNGE.

BUNGE NI DHAIFU.



Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugai aachie Uspika yeye kwa kulikosesha Bunge letu heshima na kuliongoza kufanya azimio feki/batili dhidi ya CAG.

Ndugai kavunja Katiba ya nchi.
 
Ndugai hana sifa za kuwa kiongozi, kiongozi lazima uwe na hekima na busara,...lakini kwa Ndugai hakuna yote hayo.
 
kwa unyenyekevu. Mh. Ndugai ndo naona anampa wakati mgumu mh. Rais kwenye hili swala. Asipo angalia ataleta constitutional crisis asiyo itarajia.
 
Naamini profesa wewe ni muumini na unafahamu kabisa mafunzo ya dini ya kiislam barabara, inahimiza kusameheana,kuombana radhi ,unyenyekevu ,kuhurumiana ,kutokukwazana, kujishusha na mengine mengi yametajwa katika Quran tukufu.

Nakuomba kwa kuwa kauli hiyo imekwaza Bunge na wewe umesema maana ya hilo neno kihasibu na bunge limekataa,nashauri uitishe media ukubali kuliomba Bunge samahani kwa kukwazika na kauli hiyo ambayo hukutegemea ya kuwa wataipokea namna hivyo.

Mshikane mikono maisha yaendelee, ila watanzania kwa mitizamo yao kila mmoja kalibeba kwa namna inavyompendeza.

Kwetu sisi watu wa imani tumekatazwa kukwazana.

Achana na mihemuko ya mitandaoni kwani wabaya wa watu ni watu wenyewe,wanakuza mgogoro huu kwa maslahi binafsi na chuki zao.

Nakuomba rudisha roho limalize hili kwa namna nilivyokuomba,ili kama kuna lingine watanzania tutajua,

Rejea Quran tukufu isome ikuongoze kutatua mtanziko huu.

Wabillah Taufiq

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi aliyekwazwa kauli ya "Dhaifu" ni Bunge au ni Ndugai?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Simple logic, bunge letu lina uwezo wa kuharamisha jambo, ila halina uwezo wa kuharamisha jambo lililokuwa ni halali. Kwa mfano bunge lina uwezo wa kusema kuanzia sasa neno dhaifu ni haram, ikawa sahihi kisheria. Ila bunge haliwezi kusema kuanzia mwaka jana neno dhaifu ni haram ikawa sahihi kisheria.
 
Jamaa ni kama anamwambia CAG "So ujiuzulu tuu?" Kama Magufuli alibyomwambia Bashite alipe kodi makontena yake bandarani "Si ulipe tuu hiyo kodi?" Mambo ya kuombwa nkhoi!
 
Back
Top Bottom