Spika Job Ndugai: Matatizo yetu na Prof. Mussa Assad ni kutuita dhaifu, alitakiwa ajiuzulu. Hatuna tatizo na ripoti yake, tutaifanyia kazi

Kama tunaliona bunge.dhaifu yeye analazimisha tubadili mawazo yetu ama ya CAG?
Inashangaza sana. Mtu akikuita mjinga, kama wewe siyo mjinga je utakuwa mjinga kwa kuwa tu umeitwa mjinga? This.is all too silly.
 
Spika wa Bunge Job Ndugai, leo Aprili 14 atazungumza na waandishi wa habari jambo muhimu kuhusu bunge.

Mazungumzo hayo yatafanyika katika ofisi ndogo ya bunge jijini Dar es salaam majira ya saa sita na nusu mchana.

=====

UPDATES:

View attachment 1071319

=> Spika Ndugai: CAG anaposema mbele ya umma kuwa ataendelea kutuita 'dhaifu' wakati ni jina ambalo hatulipendi na tumelikataa, tunashindwa kumuelewa kama analipenda sana ajiite yeye. Sasa kusema unaendelea kutumia endelea na nitakuita tena na safari hii itakuwa mbaya zaidi"

=> Spika Ndugai: "Namwambia ndugu yangu Prof. Assad hilo neno aliache, sisi taarifa tumeipata na tutaifanyia kazi. Msisitizo wetu ni mmoja, kwakuwa bunge lilishapitisha uamuzi wa kutofanya kazi na Prof. Assad ni uamuzi halali"

=> Spika Ndugai: "Sina chuki binafsi na Prof. Assad, yule ni ndugu yangu na ni mtanzania mwenzangu tatizo ni lugha anayoitumia na nisinhependa itufikishe hapa kama taifa."

=> Spika Ndugai: "Tunataka tumuoneshe Prof. Assad kuwa Bunge halichezewi, simuelekezi kazi ila anatakiwa ajiongeze kama ni kujiuzulu au laaa!. Maana tushamwambia hatumtaki, anavyoendelea kubaki ofisini ni kumpa tu wakati mgumu Rais

=> Spika Ndugai: Zipo njia za kumaliza mambo kama haya, mojawapo aende kwa Rais akajieleze kwamba mimi nimepima nimeona nimekosea hapa na pale. Maana Rais ni sehemu yetu sisi (Bunge) hatuwezi kupitisha sheria bila yeye kupitisha mkono wake,

=> Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai amewahakikishia watanzania kuwa bunge linaendelea vizuri na kazi yake ya kutunga sheria, uwakilishi, kuisimamia Serikali pamoja na mipango ya nchi ikiwemo suala la bajeti ambalo linaendelea bungeni.

=> Spika Ndugai:“Sasa kumekuwa na ufafanuzi usiokuwa sawa sawa, kilichowekwa mezani ni ‘Audit Queries’ …kilichowekwa mezani sio ukweli wenyewe kwamba aliyetajwa mule sasa huyo mwizi… ‘Audit queries’ zile zikishawekwa mezani kazi yetu ni kuwaita mezani na kuwasikiliza

=> Spika Ndugai:Tunataka tumuoneshe Prof. Assad kuwa Bunge halichezewi, simuelekezi kazi ila anatakiwa ajiongeze kama ni kujiuzulu au la! maana tushamwambia hatumtaki, anavyoendelea kubaki ofisini ni kumpa tu wakati mgumu Rais

=> Spika Ndugai:Hatuna tatizo na ripoti ya CAG…tatizo letu ni maneno ambayo Profesa Mussa Juma Assad ameyatoa akiwa Marekani, na alipoita waandishi akarudia tena, maneno yale sie tumeyakataa sio ya kistaarabu.

=> Spika Ndugai:Sisi kama Bunge hatutaki hilo neno dhaifu, kwa sababu Bunge kama Bunge halifanyiwi tathmini na ofisi ya CAG ila wanaofanyiwa tathmini ni watendaji wa Ofisi hiyo hivyo hawakupaswa kudhihakiwa na lugha hiyo inayotajwa kuwa ya kihasibu.

=> Spika Ndugai: “Hata katika maisha ya kawaida, we unamuita mtu jina flani, anakwambia bwana tafadhali jina hili silipendi, lakini unaendelea kumuita na kuahidi utaendelea kulitumia, ni ustaarabu duniani?”

=> Spika Ndugai: “Katika kutekeleza majukumu yake #CAG hakupaswa na hapaswi kulitukana #Bunge kwa lugha zile za rejareja. Bunge huangalia taratibu zake na kuendesha mambo yake kufuatana na kanuni za Bunge…lile Bunge lenyewe hawezi kulikagua”

=> Spika Ndugai: Hatuna tatizo na ripoti ya CAG…tatizo letu ni maneno ambayo Profesa Mussa Juma Assad ameyatoa akiwa Marekani, na alipoita waandishi akarudia tena, maneno yale sie tumeyakataa sio ya kistaarabu.

=> Spika Ndugai: “Sasa kumekuwa na ufafanuzi usiokuwa sawa sawa, kilichowekwa mezani ni ‘Audit Queries’ …kilichowekwa mezani sio ukweli wenyewe kwamba aliyetajwa mule sasa huyo mwizi… ‘Audit queries’ zile zikishawekwa mezani kazi yetu ni kuwaita mezani na kuwasikiliza”

"Nilipokuwa sipo kuna mambo mengi yamezungumzwa, na mengine yameandikwa kuhusu Ripoti ya CAG. Nitakapokuwa Dodoma nitaagiza ripoti ipelekwe kwenye kamati za PAC na LAC"

Zaidi soma.....

Dar es Salaam. Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amemshauri Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad akamwone Rais John Magufuli ili mzozo wake na Bunge uishe.

Kauli ya Spika inakuja wakati tayari Bunge limeshapitisha azimio la kutofanya kazi na Profesa Assad bali ofisi ya CAG.

Spika Ndugai aliyekuwa ziarani nchini Sweden wiki iliyopita ameyasema hayo leo Jumapili Aprili 14, 2019 akieleza kusikitishwa na hatua ya Profesa Assad kurudia neno udhaifu kwa Bunge alipotoa taarifa yake hivi karibuni.

"Zipo njia za kumaliza mambo kama haya, mojawapo aende kwa Rais akajieleze kwamba mimi nimepima nimeona nimekosea hapa na pale. Maana Rais ni sehemu yetu sisi (Bunge) hatuwezi kupitisha sheria bila yeye kupitisha mkono wake," alisema Ndugai.

Ameongeza kuwa hata bajeti inayojadiliwa na Bunge lazima ipitishwe na Rais. Amesema kwa kuwa Bunge limeshapitisha azimio la kutofanya kazi na Profesa Mussa Assad alitakiwa ajiuzulu.

"Kwa kuwa Bunge likishaaamua kuwa halifanyi kazi na mtu, ni uamuzi halali. Katika nchi zote Bunge likishakosa imani na wewe unajiuzulu," amesema.

Ameongeza, "Sasa hatumfundishi kazi Mussa Assad, anampa wakati mgumu Rais tu. Tutafanya kazi na ofisi ya wananchi."

Spika Ndugai amemsifu Profesa Assad kwa ujasiri wake huku akiufananisha na ujasiri wa mbwa kumtukana mtu anayemlisha.

"Unatukana hadi mkono unaokulisha, inahitaji ujasiri na jamaa ana ujasiri. Ila ni ujasiri ule wa mbwa anayemtukana anayemlisha," amesema.

Hata hivyo, Ndugai amesema hana chuki binafsi na Assad bali tatizo ni lugha tu aliyotumia ya kuliita Bunge dhaifu.

Huna aibu Ndugai?wa kujiuzulu ni wewe kwa sababu wew ndio dhaifu maana umshindwa kusimamia mhimili ambao unaisimamia serikali.kwa jinsi mambo yanavyoenda huko bungeni tunakushangaa unang'anga'nia ofisi nyeti kama hiyo.THE CITIZENS OF TANZANIA WANT YOU TO STEP DOWN AND NOT THE CAG.
 
Kumbe lengo lenu lilikuwa ni CAG ajiuzulu?, ukweli ni kwamba watanzania ni tunaelewa mbivu na mbichi kwenye sakata hili. Na Leo ndugai amedhihirisha kuwa bunge ni mhimili unaotekeleza maagizo toka juu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee...amekuwa kama mwehu!On a.Alito. badilisha gear angani. Professor Assad ni mtu wa dua. He knows exactly what he's doing.Ni mtu makino sana na mzalendo aliyetukuka.
Wachamungu wote wa dini zote na wa makabila yote na wa vyama vyote wamesimama na Mtu wa Mungu Prof.Assad mteule wa Rais anayelindwa na Katiba.

Nadhani hata Rais amekua Mara kwa Mara akisema tumuombee ili atende kwa kumtanguliza Mungu.
Prof.Assad Anatenda kwa kumtanguliza Mungu.
Ndugai anatanguliza kujipatia sifa na Heshima kwa kuwalinda Madisadi kupitia bunge

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaan una nyumba, ukaweka watumishi na wawakilishi...
Ila kwa ajili ya uongozi wa kiutendaji , ukamuweka msimamizi mkuu.
Huyo msimamizi mkuu ukampa mamlaka ya kukutafutia mkaguzi wa mahesabu ya vitengo vya watumishi wako.
Huyo mkaguzi akasema wawakilishi wako ni dhaifu.
Kisha akatoa report kwako, kwa wakilishi wako na kwa msimamizi mkuu kuhusu ukaguzi wa nyumba yako nzima.

Sasa mtumishi wako mmoja analalamika ameambiwa kuwa yeye ni dhaifu. Anasema hataki kufanya kazi na mkaguzi wako kisa kasema yeye na kitengo chake ni dhaifu katika majukumu yao.

Unafanyaje. Wakati kazi ya mkaguzi wako ni kutoa maoni kuhusu hao hao watumishi. Hivyo mtumishi wako huyo amekasirikia maoni ya mkaguzi wako wakati ndio kazi ya huyo mkaguzi (kutoa maoni).

Again, unafanyaje?

Sent using LF Electromagnetic Waves
 
Nijuavyo Mimi katika uhasibu kuna vikao maalumu ambavyo uhusiana na majibu ya hoja kwa hoja pamoja na kutoa vielelezo., kikao Cha mwisho ambacho ni exit meeting ufanyika kwa pande zote mbili kusuluhisha maeneo yenye matatizo ya ushahidi au vielelezo.

Hadi inaandikwa taarifa ya ukaguzi lazima auditor na mkaguliwa wanakuwa wameafikiana kwamba tatizo lipo wapi.

So spika kutumia AUDIT QUERIES ni neno sahihi na lenye maana ya maeneo dhaifu au yaliyo na mapungufu. Aidha, spika kwa nafasi yake anaanzaje kupingana na hoja za wakaguzi wakati hata field akwenda?Hizo kamati zake zinaenda kufanya ukaguzi upya na kuja na taarifa zao zenye vielelezo? Ni kazi ya BUNGE kutoa majibu ya hoja za CAG au ni wajibu wa serikali?

Je,spika anataka kutuambia kwamba tafsiri ya Audit Queries kwa kiswahili ni Nini? Au ametumia kiingereza kuwapumbaza Wasiokijua?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mheshiwa , ukitaka usionekane dhaifu acha kujifanya Bunge dhaifu....,... hayo maneno yako yanadhihirisha kuwa Wewe na Bunge unaloliongoza ni fhaifu
Pili.... Huo udhaifu unatokana na vigezo, Hata ukiwaita KPMG Au professional coy yoyote Kwa vigezo hivyo wewe na Bunge lako ni dhaifu na Najua unajua ndivyo ilivyo, ila unajikakamua tu....,,
 
Kwa alichofanya Ndugai ni wazi kwamba muhimili wa Bunge na Seriakali kwa Tanzania ni kitu kimoja. Ndugai Kama spika anapinga taarifa za kitaalaamu anazopewa na ambazo zinatakiwa kupatiwa majibu ya hoja na mawaziri kwa upande wa serikali.

Kama mwamuzi ameshaonyesha anasimamia wapi kuna umuhimu Tena wa kujadili taarifa hizo?

Naamini hata kwenye vikao vya ndani vya chama yanaweza kutoka maelekezo ya wabunge wa CCM kusimama na serikali kuipinga ripoti ya CAG.

Bunge limeacha kusimamia na kuikosoa seriakali badala yake limesimama na seriakali kwa umoja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa watu makini wanajua Report ya CAG ndio kitu kilichotawala week hii yote lakini pia kuna ufisadi wa kutisha ndani ya Report Ile.

Zitto katoa takwimu za uhakika kwamba pesa zaidi ya 4.6 trion zilitumika kiholela...

Pia ameonyesha jinsi gani ambavyo CAG kaogopa kiasi kusema kwamba pesa zaidi ya bilion 800 zimechotwa na kupotea.

Huu ni mkakati wa Serikali kumtumia Job Ndungai ili sisi tuendelee kum discuss yeye na kuacha report ya CAG..

Jamani tuache siasa za matukio serikali waje na majibu ya maana kutokana na Report ya CAG ambayo inaonyesha kuna ufisadi wa kutisha kuliko report zote kuanzia mwaka 1961 tulipopata uhuru.

Bilion 800 zipo wapi ? Pesa ya kujenga shule zaidi ya 800 za bilion 1 nchi nzima ma kununua madawati zinapotea bila kujibiwa zipo wapi halafu tunaenda kufatilia upuuzi wa job Ndungai?.

Ili kuzima mjadala lazima kwanza pesa zetu zijulikane zilipo bilion 800 ukiunganisha na Ile 2.4 trion tutakuwa tumepoteza pesa zaidi ya trion 3.2 ndani ya miaka 2 je baada ya miaka 10 tutakuwa tumepoteza pesa kiasi gani..

Serikali ya kifisadi,Bunge dhaifu CAG ndiye mshindi kwa hili

Jibuni hoja za CAG kwanza .
Tunakosea kuihusihusisha serikali na Ubinafsi wa Nduu gay .
Spika anatumiwa na mafisadi na mafisadi wezi wanaochota fedha za umma.

Kumbuka Sakata la Jairo ala kuhonga wabunge wa CCM .
Miaka nenda rudi Wakaguzi wamekua wakihongwa ili wafukiefukie madudu ya Wizara na taasisi za umma huku watu wachache wakijilimbikizia Mali kupitia ofisi za umma. Wameshindwa kumhonga Prof. Assad sasa ameamua kulitumia bunge.

Rais wala mawaziri hawajahusika kabisa japo mawaziri wamezembea kwenye usomamizi. Ndio maana Rais amesema mawaziri wawe wakali ikiwezekana wavute hata bangu mana kuna pesa zinachezewa.

Rais amesimama na Uadilifu wa CAG.
CAG aendelee kujitolea kuwatumikia watanzania. Hiyo nafasi angeitumia kwa malengo binafsi bila shaka naye angewaza kujilimbikizia Mali za ufisadi zinazopatikana toka kwa mafisadi wanaoliibia taifa letu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nijuavyo Mimi katika uhasibu kuna vikao maalumu ambavyo uhusiana na majibu ya hoja kwa hoja pamoja na kutoa vielelezo., kikao Cha mwisho ambacho ni exit meeting ufanyika kwa pande zote mbili kusuluhisha maeneo yenye matatizo ya ushahidi au vielelezo.

Hadi inaandikwa taarifa ya ukaguzi lazima auditor na mkaguliwa wanakuwa wameafikiana kwamba tatizo lipo wapi.

So spika kutumia AUDIT QUERIES ni neno sahihi na lenye maana ya maeneo dhaifu au yaliyo na mapungufu. Aidha, spika kwa nafasi yake anaanzaje kupingana na hoja za wakaguzi wakati hata field akwenda?Hizo kamati zake zinaenda kufanya ukaguzi upya na kuja na taarifa zao zenye vielelezo? Ni kazi ya BUNGE kutoa majibu ya hoja za CAG au ni wajibu wa serikali?

Je,spika anataka kutuambia kwamba tafsiri ya Audit Queries kwa kiswahili ni Nini? Au ametumia kiingereza kuwapumbaza Wasiokijua?

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kazi ya bunge kutoa majibu ya hoja za CAG au ni wajibu wa serikali?

Hili ni swali la msingi sana!
 
Niliota ndoto moja ivi juzi nikajiuliza why!nilipooota tu ile ndoto nikajua mwisho wa huu mtanange nani atashinda
 
lakini pia amesema neno likitamkwa kwa kiingereza au kwa kiswahili linaleta uzito tofauti.
amesema wao hawalitaki hilo neno, kama CAG analipeeenda sana basi ajiite yeye Prof. Dhaifu, bunge wamekataa hilo jina la kejeli.
Lakini pia amezungumzia kasumba ya wasomi wa kibongo kujiita prof, Dr, NK kila sehemu kuwa ni ushamba, pia kujiona wewe mjuaji saana kwakua tu ni profesa huo ni undezi.
(nadhani dakta JPM pia aache kuitwaitwa Dr, ni ulimbukeni)
busara ni CAG kuwaomba radhi wabunge kwa kuwakwaza kisha maisha yaendelee.
 
Back
Top Bottom