Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,517
- 113,647
Mkuu Fundi Mchundo, naomba kukiri wewe ni mmoja wa watu ambao you command highly respect kutoka kwangu hivyo criticism kutoka kwako, I take them very serious. Thanks for this.Paskali, ukiona wakati mwingine wanaJF wanakusema kwa lugha hasi, fahamu kwamba hawakuchukii wewe mwenyewe binafsi, bali wanaonyesha hasira zao kwa Waandishi wa Habari kupitia kwako kwa sababu mbele ya macho yetu, wewe ni Mwandishi Jasiri.
Tunapoona ujasiri umeyeyuka miongoni mwa Waandishi wa Habari, we have been channeling our disappointments and frustrations through you.
And I believe you know this.
Paskali, you are a flag bearer.
Na umeendelea kulithibitisha hili pale ulipokaribishwa Star TV ukaupiga mwingi kwa kutema madini yasiyo ya kawaida.
Nina ombi maalum kwako, ambalo litajibu tatizo la hawa Wabunge 19.
Ninakuomba ufanye mahojiano mahsusi na Mwenyekiti au Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, ili kupitia majibu utakayopewa, Watanzania tujue ni kwa namna gani Tume ilipeleka Majina ya akina Halima Mdee kwa Spika wa Bunge.
Watanzania wanamtuhumu Spika badala ya kutuhumu Tume ya Uchaguzi.
Tunajua Tume ya Uchaguzi ikiingia kwenye 18 za 'Paskali', Watanzania tutajua pia 'logic behind' ukataji wa majina ya Wagombea wa Upinzani tu, kwa kukosea kujaza Fomu za kuomba kugombea, wakati kwa Wagombea wa CCM, HAKUNA HATA MMOJA ALIYEKOSEA KUJAZA FOMU.
Yaani, asilimia zaidi ya 95 ya Wapinzani walikosea kujaza Fomu, wakati Wagombea wa CCM walipatia kwa ASILIMIA 100.
Paskali, tusaidie tafadhali.
Please, fahamu kuwa, hapa JF, Paskali, au P. ni 'brand'
Asante sana kwa ushauri kuhusu hayo mahojiano, naomba nisiahidi kitu chochote kwa sasa ila...
Nimalize kwa kukushukuru tena.
P