Kati ya Spika mstaafu Msekwa na Halima Mdee nani yuko sahihi juu ya uhalali wa Wabunge 19 wa CHADEMA?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,850
141,769
Spika mstaafu mzee Msekwa anasema wale wabunge 19 walioko bungeni yaani Halima Mdee na wenzake siyo halali waliingia bungeni kinyume cha katiba kwani siyo wanachama wa Chadema.

Halima James Mdee anasema wao ni wabunge halali wa Chadema kwani wako bungeni kwa baraka za chama chao.

Hili swala unaweza kuliona dogo lakini ni kubwa sana.

Huyu Msekwa ndiye aliyetengeneza katiba ya JMT ya 1977 inayotumika sasa hivyo kauli yake siyo ya kupuuzwa kabisa.

Lakini Halima James Mdee alikuwa mwenyekiti wa Bawacha taifa chombo kinachoratibu majina ya wagombea ubunge wa viti maalumu Chadema, kwahiyo kauli yake ina uzito pia.

Ikumbukwe Halima James Mdee hii siyo mara ya kwanza kuwa mbunge wa viti maalumu alishakuwa mwaka 2005.

Swali la msingi ni kwanini Chadema hawaitishi kikao cha baraza kuu/ mkutano mkuu kusikiliza rufani za covid 19?

Kwanini Chadema hawaendi mahakamani kama alivyoshauri Spika mstaafu anayeheshimika sana mzee Pius Msekwa?

Maendeleo hayana vyama.

Mungu wa mbinguni awabariki nyote!

Pia soma
 
Kwa nchi yenye misimamo ya dimokurasia, au yenye wasomi walio jifunza hao wabunge 19, ni aibu kubwa sana kuendelea kuka humo bungeni, hata Kenya tu hilo lisingetokea ila hi Tz ni ya kisani chochote kinawezakana, kama mtu kichaa anaweza kua Raisi kipi kinashindikana.
 
Kwa nchi yenye misimamo ya dimokurasia, au yenye wasomi walio jifunza hao wabunge 19, ni aibu kubwa sana kuendelea kuka humo bungeni, hata Kenya tu hilo lisingetokea ila hi Tz ni ya kisani chochote kinawezakana, kama mtu kichaa anaweza kua Raisi kipi kinashindikana
Kenya wako mbali sana bwashee kwenye haya mavitu!
 
Spika mstaafu mzee Msekwa anasema wale wabunge 19 walioko bungeni yaani Halima Mdee na wenzake siyo halali waliingia bungeni kinyume cha katiba kwani siyo wanachama wa Chadema..
Hiyo ndio siasa mkuu wale wabunge walipelekwa na chama.pale wameegeshwa tu ukiwatoa wale wabunge chadema sio chama kikuu cha upinzani kwa hiyo usishangae siku ikatoka taarifa kuwa wamesamehewa.

Si umeona mwenyewe Sumaye na Lowassa wako wapi pamoja na kauli nzuri walizotoa kwa upinzani na kejeli kwa chama tawala.Lisikuhangaishe hilo wenzako wameona mbali na siku wakiwasamehe akina Mdee watapata malimbikizo kibao ya ruzuku.aluta continua.
 
Hiyo ndio siasa mkuu wale wabunge walipelekwa na chama.pale wameegeshwa tu ukiwatoa wale wabunge chadema sio chama kikuu cha upinzani kwa hiyo usishangae siku ikatoka taarifa kuwa wamesamehewa.si umeona mwenyewe Sumaye na Lowassa wako wapi pamoja na kauli nzuri walizotoa kwa upinzani na kejeli kwa chama tawala.Lisikuhangaishe hilo wenzako wameona mbali na siku wakiwasamehe akina Mdee watapata malimbikizo kibao ya ruzuku.aluta continua.
Nami naamini hivo! Mtu anawatukana wakina Mdee unafikiri wameenda pale bila baraka za mwenyekiti? Pale zinapigwa fix tu kwani kile kikao cha kusikiliza rufaa zao kilishakaa? Ilibidi kikae lini? Walipoba wapeleke muhtasari wa kikao cha kamati tendaji kilicho wafukuza walipeleka? Kwaiyo unaweza kuona pale wapo kwa baraka za nani!
 
Hiyo ndio siasa mkuu wale wabunge walipelekwa na chama.pale wameegeshwa tu ukiwatoa wale wabunge chadema sio chama kikuu cha upinzani kwa hiyo usishangae siku ikatoka taarifa kuwa wamesamehewa...
Ndugu,

Naona wakijani mwajitahidi kujipa raha na faraja za bei rahisi.

Dhambi ya kuendelea kuwakumbatia bungeni hata wasio na chama inazidi kuwala na kama ilivyomtokea Ndugai itazidi kuwarudia tu mmoja baada ya mwingine.
 
Prioroties! Kuna ya msing zaidi kuliko upuuzi wa Mzee Mdee. Shida iko wapi, wanakula pesa ya bunge na maisha yanaendelea....
Hili la akina Halima Mdee ni la kikatiba.

Au Chadema katiba yenu haiheshimiki?!!
 
Hiyo ndio siasa mkuu wale wabunge walipelekwa na chama.pale wameegeshwa tu ukiwatoa wale wabunge chadema sio chama kikuu cha upinzani kwa hiyo usishangae siku ikatoka taarifa kuwa wamesamehewa.si umeona mwenyewe Sumaye na Lowassa wako wapi pamoja na kauli nzuri walizotoa kwa upinzani na kejeli kwa chama tawala.Lisikuhangaishe hilo wenzako wameona mbali na siku wakiwasamehe akina Mdee watapata malimbikizo kibao ya ruzuku.aluta continua.
Ndugu,
Naona wakijani mwajitahidi kujipa raha na faraja za bei rahisi.
Dhambi ya kuendelea kuwakumbatia bungeni hata wasio na chama inazidi kuwala na kama ilivyomtokea Ndugai itaendelea kuwarudia tu mmoja baada ya mwingine kila mtu peke yake. AMEN
 
Ndugu,
Naona wakijani mwajitahidi kujipa raha na faraja za bei rahisi.
Dhambi ya kuendelea kuwakumbatia bungeni hata wasio na chama inazidi kuwala na kama ilivyomtokea Ndugai itaendelea kuwarudia tu mmoja baada ya mwingine kila mtu peke yake. AMEN
Aibu sn
 
Basi itisheni baraza kuu msikilize rufaa zao.

Mnaogopa nini?!!
Hivi hata Sheria kidogo hata za Mahakama ya Kuku hizijui au? Mtu akifungwa jela akikata rufaa kabla rufaa yake haijasikilizwa anakuwa huru?
Covid 19 walivuliwa Uanachama, wamekata rufaa. Kabla ya rufaa kusikilizwa wanakuwa wanachama au siyo wanachama?
Baada ya mfano huo linganisha Sasa akili za Msekwa na za Mdee.
 
Back
Top Bottom